J. Mnyika: Tunajiandaa kuwafikisha Membe na Simba Mahakamani

- Chadema wangejiepusha na this kind of politics, wajikite kwenye kuwahamasisha wananchi kuhusu mapungufu ya watawala na what are the solutions, kama walivyofanya kwenye ishu ya Buzwagi. tunajua kwamba vyama vyote vya siasa nchini vinafadhiliwa na mataifa ya kigeni wala sio siri na infact wala sio kuvunja any sheria ya Jamhuri kwa sababu hatuna!

- So Chadema as much as some of us ndani ya CCM tunaheshimu sana kazi mnayoifanya sasa hivi kuwakosesha usingizi tembo huku CCM, ni vyema mkaelewa tofauti ya propaganda na policies, hii ya hela kutoka nje ni none-ishu!

William, @ NYC, USA.

a question outside of the main issue. Kwa nini wewe ni mwanachama wa CCM?
 
Siasa za Tanzania hizi bwana hakuna ACTION...maneno mengi na vitisho halafu baadae kimya.

Juzi juzi tu nimemsikia mkulu kwenye ile hotuba yake ya mwisho wa mwezi hakuna jawabu lolote lile la matatizo ya nchi...zaidi analalamikia chadema na mvua.

Miaka mingi nunatumia hydro power kwa hiyo ni lazima iko risk analysis yaani kama mvua ikikosekana...Rais mzima analalamika tu na hakuna hata njia yoyote ile aliyosema ya kutatua matatizo.

Nao CHADEMA wamempa tisa siku na sasa zeshapita masiku kadhaa....hii ndio siasa zetu.

Nimesema mara nyingi tu hakuna nchi rahisi kuongoza kama TZ, bahati mbaya hatujampata mzalendo wa kutuongoza...hata wabunge wetu hawa wote ni wabinafsi wametumia 'mavijisenti' mengi kuupata huo ubunge sasa wako pale kurudisha gaharama zao na kuvuna na wengine sasa hivi wanajitayarisha kwa chaguzi za mwaka 2015.

Yaani kila kukicha wananchi wazidi kudidimia na wachache wanazidi kutanua...Je hali hii itaendelea mpaka lini?

point mkuu. Yani kila siku ni maneno ya kijinga wanatupiana. Sasa wanaenda kumshaki kwa kuvunja kosa gani?
 
Legal inshu ni kuchafua chama,chadema wanaweza wakataka udhibiti au sofia simba akisafishe chama
 
That is GOOD! I like that. Chama chao wote ni waropokaji. Hakuna msemaji wa chama. Wanachofanya ni kupokezana. Mara Chiligati, mara Makamba, Tambwe, JK, Wasira, sasa ni Membe na SS! Dawa ni hiyo. Wapelekwe kortini ili wathibitishe na wakishindwa waadhibiwe. Viongozi wanatakiwe wajue kuwa wao sio waimba taarabu. Mipasho wawaachie akina Hadija Kopa na Mzee Yusuf
 
Jamani kama ni Asofia Simba hakuna haja ya kumshitaki,huyu mama ana ugonjwa wa kichaa ndicho kinamsumbua jasa pale anapoacha kumeza dawa

kwa hiyo ina maana serikali ya tz ina mawaziri vichaa nasikia homa kali jamani
 
Nikinukuu gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 14 Machi 2011, yenye kichwa cha habari ‘ Chadema kumburuza kortini Waziri Simba’. Kwenye taarifa hiyo Mnyika anasema wanataka kumburuza kortini Mh. Waziri, Sofia Simba kwa kauli ya kukipaka matope chama hicho kutokana na tuhuma za kufadhiliwa na nchi za nje kufanya maandamano.

Leo hii Chadema ndio wanajifanya kuitambua mahakama, kwani kwenye suala la Arusha mbona mahakama mliikataa kuwa haiwezi kutoa haki, sasa mnategemea haki safari hii mtaipata au mambo ya mfa maji haishi kutapa tapa ?.
 
Ndugu kumbuka pamoja na udhaifu wote huo sio kila Jaji ama Hakimu amelewa U-CCM. Na kila jambo linaaina yake ya mtazamo na hatua za kuchukuliwa kutokana na uzito wake.
 
Huyo usidhani jina lake ni sawa na yeye jina kajipa tuuuu! Ila nikilaza mkubwa saana sijui ni tambwe hiza!
 
Nikinukuu gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 14 Machi 2011, yenye kichwa cha habari ' Chadema kumburuza kortini Waziri Simba'. Kwenye taarifa hiyo Mnyika anasema wanataka kumburuza kortini Mh. Waziri, Sofia Simba kwa kauli ya kukipaka matope chama hicho kutokana na tuhuma za kufadhiliwa na nchi za nje kufanya maandamano.

Leo hii Chadema ndio wanajifanya kuitambua mahakama, kwani kwenye suala la Arusha mbona mahakama mliikataa kuwa haiwezi kutoa haki, sasa mnategemea haki safari hii mtaipata au mambo ya mfa maji haishi kutapa tapa ?.

kuna kase za kwenda mahakamani na basis zake. wanachadema wengi ni wanasheria na wanajua maana ya mahakama. kwenda kaandae maandamano na watoto wa mafisadi!
 
Nikinukuu gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 14 Machi 2011, yenye kichwa cha habari ‘ Chadema kumburuza kortini Waziri Simba’. Kwenye taarifa hiyo Mnyika anasema wanataka kumburuza kortini Mh. Waziri, Sofia Simba kwa kauli ya kukipaka matope chama hicho kutokana na tuhuma za kufadhiliwa na nchi za nje kufanya maandamano.

Leo hii Chadema ndio wanajifanya kuitambua mahakama, kwani kwenye suala la Arusha mbona mahakama mliikataa kuwa haiwezi kutoa haki, sasa mnategemea haki safari hii mtaipata au mambo ya mfa maji haishi kutapa tapa ?.

kulikuwa na uhaba wa mahindi ..... naona umerudia uzalishaji wa pumba
 
Nikinukuu gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 14 Machi 2011, yenye kichwa cha habari ‘ Chadema kumburuza kortini Waziri Simba’. Kwenye taarifa hiyo Mnyika anasema wanataka kumburuza kortini Mh. Waziri, Sofia Simba kwa kauli ya kukipaka matope chama hicho kutokana na tuhuma za kufadhiliwa na nchi za nje kufanya maandamano.

Leo hii Chadema ndio wanajifanya kuitambua mahakama, kwani kwenye suala la Arusha mbona mahakama mliikataa kuwa haiwezi kutoa haki, sasa mnategemea haki safari hii mtaipata au mambo ya mfa maji haishi kutapa tapa ?.

mara ya mwisho kunywa TOGWA ni lini!!!
 
Chadema kinaandaa hatua za kisheria za kumchukulia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba kwa kauli zake ambazo amekuwa akizirudia rudia kwamba chama hicho kimekuwa kikifadhiliwa na balozi tano za nchi za Ulaya ili kufanya maandamano ya kuvunja amani nchini.

Pia chama hicho kimemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Bernard Membe kuzitaja balozi hizo zinazofadhili chama hicho na kiasi cha fedha kinachotolewa.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mnyika katika mkutano wake na wanahabari.

Mnyika alisema Simba amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba maandamano ya Chadema ambayo yalikuwa yakifanyika katika Kanda ya Ziwa yamekuwa yakifadhiliwa na Balozi za nchi za Ulaya.

“ Lakini jana (juzi) Waziri Membe aliulizwa kuhusu kuwapo kwa tuhuma za Balozi za Ulaya zinazowakilisha nchi zao hapa nchini kikifadhili chama kimoja cha siasa bila kukitaja, akajibu kuwa anafahamu suala hilo na vyombo vya usalama vinachunguza,”alisema Mnyika.

“Kwa kuwa Waziri mwenzake Simba alishakitaja chama chetu kuwa ndicho kinachofadhiliwa na nchi za Ulaya ili kufanya maandamano ya kuvunja amani, tunaomba sasa azitaje nchi hizo na fedha zinazotolewa,”alisema Mnyika na kuongeza.

“Hakuna sababu kwa Waziri Membe kukaa kimya kuhusu tuhuma zinazofahamika ambazo Waziri mwenzake amekwishaweka hadharani, aueleze umma ili Balozi hiyo ziweze kueleza kuhusu tuhuma hizo,” alisema.

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alisema chama hicho hakipewi ufadhili wowote kutoka nje ya nchi kwa lengo la kufanya maandamano ya kuvunja amani.

“Maandamano yale na mikutano ni ya wananchi, wamehamasika baada ya Serikali yao kushindwa kuwatekelezea mahitaji yao muhimu,” alisema.

Aidha, alisema wananchi wanaohudhulia maandamano hayo hawalipwi, wanahamasika baada Serikali yao kushindwa kutekeleza ahadi zake.

Aliongeza kuwa Serikali baada ya kujikita katika kutatua kero za wananchi, wanajikita kwenye propaganda ambazo zitapaswa kufanywa na CCM.

“Mwanzo walieneza propaganda kwamba chama chetu ni cha kikabila wananchi wakapuuza, baadaye wakasema kina udini wakapuuza, sasa wanasema kinapata ufadhili kutoka katika balozi,”alisema.

“ Kutokana na kauli za Waziri Simba, sasa wanasheria wa chama Tundu Lisu na Mabere Marando wanaandaa taratibu za kisheria za kumchukulia,” alisema.

Alisema wanasheria hao wakishaandaa hatua za kuchukua, waandishi wa habari watafahamishwa.

Wakati huo huo, Mnyika amesema kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho, baada ya kumaliza mikutano katika Kanda ya Ziwa, kitaelekea katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

“ Ingawa bado haijafahamika ni lini ratiba hiyo itaanza, itajulikana baada ya viongozi wakuu wa kitaifa watakaporejea nchini kutoka Liberia wanakohudhuria mkutano wa vyama vya siasa,” alisema.

source: Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
 
atajuta...

kila kitu kipo kuanzia human resource mpaka financial resource.

wabunge 80*90, 000 000 = 7,200,000,000

plus 20 000 000 000 alizosema chadema tumepewa.

plus support ya waTZ.

kama ana mimba 'itatoka'

Hee inatoa mimba hii mambo ya kushtakiwa?
 
safi sana CDM kwani huyu mama analeta habari zake za kishangingi na haya ndio madhala ya kutokujibu hoja husika na kukimbilia kuropoka ropoka na kusahau kama nchi inaongozwa na utawala wa sheria...
 
Nikinukuu gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 14 Machi 2011, yenye kichwa cha habari ‘ Chadema kumburuza kortini Waziri Simba’. Kwenye taarifa hiyo Mnyika anasema wanataka kumburuza kortini Mh. Waziri, Sofia Simba kwa kauli ya kukipaka matope chama hicho kutokana na tuhuma za kufadhiliwa na nchi za nje kufanya maandamano.

Leo hii Chadema ndio wanajifanya kuitambua mahakama, kwani kwenye suala la Arusha mbona mahakama mliikataa kuwa haiwezi kutoa haki, sasa mnategemea haki safari hii mtaipata au mambo ya mfa maji haishi kutapa tapa ?.
Chadema ina wanasheria wake na wengi wamekubuhu wanajua wachokifanya halafu kumbuka si kila kosa linapelekwa mahakamani inategemea na evidence ulizonazo.
 
Chadema kinaandaa hatua za kisheria za kumchukulia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba kwa kauli zake ambazo amekuwa akizirudia rudia kwamba chama hicho kimekuwa kikifadhiliwa na balozi tano za nchi za Ulaya ili kufanya maandamano ya kuvunja amani nchini.

Pia chama hicho kimemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Bernard Membe kuzitaja balozi hizo zinazofadhili chama hicho na kiasi cha fedha kinachotolewa.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mnyika katika mkutano wake na wanahabari.

Mnyika alisema Simba amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba maandamano ya Chadema ambayo yalikuwa yakifanyika katika Kanda ya Ziwa yamekuwa yakifadhiliwa na Balozi za nchi za Ulaya.

" Lakini jana (juzi) Waziri Membe aliulizwa kuhusu kuwapo kwa tuhuma za Balozi za Ulaya zinazowakilisha nchi zao hapa nchini kikifadhili chama kimoja cha siasa bila kukitaja, akajibu kuwa anafahamu suala hilo na vyombo vya usalama vinachunguza,"alisema Mnyika.

"Kwa kuwa Waziri mwenzake Simba alishakitaja chama chetu kuwa ndicho kinachofadhiliwa na nchi za Ulaya ili kufanya maandamano ya kuvunja amani, tunaomba sasa azitaje nchi hizo na fedha zinazotolewa,"alisema Mnyika na kuongeza.

"Hakuna sababu kwa Waziri Membe kukaa kimya kuhusu tuhuma zinazofahamika ambazo Waziri mwenzake amekwishaweka hadharani, aueleze umma ili Balozi hiyo ziweze kueleza kuhusu tuhuma hizo," alisema.

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alisema chama hicho hakipewi ufadhili wowote kutoka nje ya nchi kwa lengo la kufanya maandamano ya kuvunja amani.

"Maandamano yale na mikutano ni ya wananchi, wamehamasika baada ya Serikali yao kushindwa kuwatekelezea mahitaji yao muhimu," alisema.

Aidha, alisema wananchi wanaohudhulia maandamano hayo hawalipwi, wanahamasika baada Serikali yao kushindwa kutekeleza ahadi zake.

Aliongeza kuwa Serikali baada ya kujikita katika kutatua kero za wananchi, wanajikita kwenye propaganda ambazo zitapaswa kufanywa na CCM.

"Mwanzo walieneza propaganda kwamba chama chetu ni cha kikabila wananchi wakapuuza, baadaye wakasema kina udini wakapuuza, sasa wanasema kinapata ufadhili kutoka katika balozi,"alisema.

" Kutokana na kauli za Waziri Simba, sasa wanasheria wa chama Tundu Lisu na Mabere Marando wanaandaa taratibu za kisheria za kumchukulia," alisema.

Alisema wanasheria hao wakishaandaa hatua za kuchukua, waandishi wa habari watafahamishwa.

Wakati huo huo, Mnyika amesema kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho, baada ya kumaliza mikutano katika Kanda ya Ziwa, kitaelekea katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

" Ingawa bado haijafahamika ni lini ratiba hiyo itaanza, itajulikana baada ya viongozi wakuu wa kitaifa watakaporejea nchini kutoka Liberia wanakohudhuria mkutano wa vyama vya siasa," alisema.

source: Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza

Mnyika,

Acha kuuhadaa umma. kama mmekusudia kwenda mahakama mnasubiri nini mbona mnatia tisha toto hapo.

Kumbukeni Mama Soffia Simba ni mwanasheria pia kwa hiyo kila amnalolisema anafahamu vilivyo .

Enendeni Mahakamani mkavuliwe nguo.
 
Back
Top Bottom