J Mnyika afafanua....

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Kuhusu Kauli za Sekretariati
ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Kufuatia Sekretariati ya
Maadili ya Viongozi wa Umma
kutangaza katika vyombo
mbalimbali vya habari tarehe
15 Februari 2012 kwamba
wameanza kuhakiki fomu za tamko la mali na madeni kwa
baadhi ya viongozi tuliojaza
fomu husika, mjadala
umeibuka jimboni na katika
jamii kuhusu suala hilo na
baadhi mmeomba maoni yangu juu ya mchakato huo. Umma ufahamu kuwa
nilitimiza masharti ya
kuwasilisha fomu kwa wakati
na kutoa tamko kwa mujibu
wa sheria, uhakiki ni utaratibu
wa kawaida. Pamoja uhakiki, natoa mwito kwa Sekretariati
kufanya uchunguzi juu ya
viongozi wa umma wenye
tuhuma mbalimbali ambao
tumewataja kwa majina kwa
nyakati mbalimbali. Aidha, kuhusu kufanya marekebisho
ya sheria ya maadili ya umma
kwa ajili ya kuweka mipaka
kati ya biashara na siasa,
sekretariati badala ya kurudia
tena kufanya utafiti irejee kauli ya serikali bungeni kuwa
waraka wa marekebisho
ulishaandaliwa tayari na itoe
mapendekezo kwa serikali
yenye kuwezesha muswada
kuwasilishwa katika mkutano ujao wa bunge. Pamoja na uhakiki wa kawaida, sekretariati ifanye uchunguzi kwa watuhumiwa: Ni vizuri ikazingatiwa kuwa
nilitimiza masharti
yanayotakiwa kwa mujibu
kifungu cha 9 cha Sheria ya
maadili ya viongozi wa umma
namba 13 ya mwaka 1995 ya kujaza fomu za tamko la mali
na madeni na ni jambo la
kawaida kwa sekretariati
kufanya uhakiki wa fomu
tajwa na kabla ya kuwa
mbunge nimekuwa nikitoa mwito wa mara kwa mara
kwa sekretariati kutimiza
wajibu husika. Ni muhimu sekretariati ya
Maadili ya Viongozi wa Umma
ikapanua wigo wa uhakiki
iongeze orodha ya viongozi
wa umma ili walau kwa
mwaka iweze kuhakiki sampuli isiyopungua 10% ya
viongozi wote wa umma na
taarifa ya uhakiki huo iweke
wazi kwa umma kuhusu wote
wasiotangaza mali kwa
mujibu wa sheria au ambao watabainika kutoa taarifa
zenye kasoro. Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Ibara
ya 132 imeweka msingi wa
kuundwa kwa Sekretariati ya
Maadili ya Viongozi wa Umma
na kwamba Ibara ya 70 kuwasilisha taarifa ya mali na
kifungu cha 71 kinataja
sababu za kukoma kuwa
mbunge kutokana na kukiuka
masharti ya Sheria ya Maadili
ya Viongozi wa umma; hivyo sekretariati inapaswa
kupanua wigo wa kutimiza
majukumu husika ya kikatiba. Kwa hiyo, pamoja na kufanya
zoezi la kawaida la kuhakiki
fomu za tamko la mali na
madeni kwa viongozi wa
umma; kwa kuwa sekretariati
imetangaza kuwa itafanya kazi kwa uwazi na kwa
kuzingatia sheria basi iweke
kipaumbele katika kutumia
mamlaka iliyonayo kwa
mujibu wa sheria husika
vifungu 18(4) na 22 (4) kufanya mchakato muhimu
zaidi wa kufanya uchunguzi
wa tuhuma juu ya ufisadi
uliofanywa na unaoendelea
kufanywa na viongozi wa
umma ambao wametajwa kwa nyakati mbalimbali
kwenye mikutano na katika
vyombo vya habari. Izingatiwe kuwa pamoja na
uchunguzi wa awali
unaoweza kufanywa na
Sekretariati kwa mujibu wa
Sheria ya Maadili ya Viongozi
wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 kifungu 22(2);
uchunguzi kamili unafanywa
na baraza ambalo kwa mujibu
wa kifungu 26(5) linapaswa
kufanya uchunguzi wake
hadharani ili umma uweze kufahamu. Kuibuka kwa mjadala huu
kumenifanya nikumbuke
mjadala mwingine ambao
uliibuka ulijitokeza mwanzoni
mwa mwaka 2010 baada ya
kauli zangu nilizotoa kwenye kipindi cha Kipima Joto
kilichorushwa katika kituo cha
luninga cha ITV ijumaa tarehe
19 Februari 2010 na
kunukuliwa na baadhi ya
vyombo vya habari tarehe 21 Februari 2010. Mjadala huo uliongezeka zaidi
kufuatia tarehe 24 Februari
2010 Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Ofisi ya Rais-
Sekretariati ya Maadili ya
Viongozi wa Umma kutoa taarifa kwa umma kujibu kauli
zangu nilizotoa na kuchapa
matangazo kwenye vyombo
mbalimbali vya habari kuanzia
tarehe 26 Februari 2010
mpaka tarehe 5 Machi 2010. Kutokana na taarifa hiyo
tarehe 7 Machi 2010 nilitoa
tamko ambalo linaweza
kurejewa kupitia: http://
www.chadema.or.tz/habari/
habari.php?id=111 ambalo nilihimiza masuala ambayo
Sekretariati ya Maadili ya
Viongozi wa Umma inapaswa
kuyazingatia na kurejea
kuweka mkazo wa kauli
ambazo nilitoa awali kuhusu ufisadi na hatua ambazo
zinapaswa kuchukuliwa kwa
viongozi wenye tuhuma
ambao niliwataja kwa majina. Waraka ulishaandaliwa; muswada wa marekebisho ya sheria uletwe bungeni Kwa upande mwingine,
Sekretariati ya Maadili ya
Viongozi wa Umma
imenukuliwa na baadhi ya
vyombo vya habari leo tarehe
15 Februari 2012 ikileza kuwa ‘itafanya utafiti kabla ya kutoa
mapendekezo ya kubadili
sheria inayotenganisha
biashara na uongozi ili
kuweka nidhamu kwa
viongozi wa umma’. Ni vyema Sekretariati ifanya
mawasiliano na mamlaka
zingine za kiserikali ili
kuepusha kurudia utafiti
ambao umekwishafanyika na
badala yake ikaelekeza nguvu zake kwenye kutoa
mapendekezo ya kuwezesha
marekebisho ya sheria husika
yakawasilishwa katika
mkutano wa saba wa bunge
unaotarajiwa kuanza tarehe 10 Aprili 2012. Sekretariati ya Maadili ya
Viongozi wa Umma izingatie
kuwa suala ililolizungumzia
lilishajadiliwa bungeni na
bunge kupitisha azimio no. 11
mwezi Februari 2008 kwamba “Sheria ya Maadili ya Viongozi
wa Umma ya Mwaka 1995
(The Public Leadership Code of
Ethics Act), ifanyiwe
marekebisho makubwa ili
kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida
sasa wa Viongozi Waandamizi
wenye dhamana ya kisiasa
kuendelea na biashara zao
binafsi wakiwa madarakani,
jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze
rasmi maandalizi ya
majadiliano ya kina kuhusu
suala hili ndani na nje ya
Bunge kwa kuwashirikisha
wadau mbalimbali.” Mwezi Februari 2010 Bunge
lilitaarifiwa kuhusu
utekelezaji wa Serikali juu ya
marekebisho ya sheria husika
kwamba kikundi kazi (Task
Force) kiliundwa ambacho kiliandaa waraka wenye
mapendekezo ya kurekebisha
Sheria ya Maadili ya Viongozi
wa Umma, (Sura 398) ambao
ulikuwa katika ngazi ya
kujadiliwa na Kamati ya Makatibu Wakuu (IMTC). Aidha,
Bunge lilielezwa kuwa serikali
ilitarajia kuwasilisha
muswada husika katika
mkutano wa kumi na tisa wa
Bunge la tisa hali ambayo ilionyesha serikali na vyombo
vyake tayari walishakamilisha
utafiti kuhusu suala husika.
Hata hivyo, Muswada huo
haukupitishwa katika Bunge
la tisa kama ilivyoshauriwa na kamati na mpaka sasa
muswada huo bado
haujawasilishwa kwa bunge
la kumi. Hali hii imetokana na
kufungwa kwa mjadala juu ya
utekelezaji wa maazimio ya
bunge juu ya mkataba kati ya
TANESCO na Richmond
Development Company kabla ya maazimio kukamilika
hivyo, na msukumo kuhusu
utekelezaji wa maazimio
husika ikiwemo la kufanya
marekebisho ya sheria tajwa
ungeongezeka iwapo hoja binafsi niliyoiwasilisha kutaka
uamuzi ubadilishwe
ingejadiliwa. Ikumbukwe kwamba miaka
miwili imepita bila ya
utekelezaji kamili wa
maazimio 10 kati ya 13
yaliyobaki hususan Maazimio
Nambari: Nambari 3,5,7,8,9,10,11,13,14 na 18;
toka mjadala kuhusu
Richmond ufungwe bungeni
mwezi Februari 2010; na ni
miaka minne toka bunge
lipitishe maazimio mwezi Februari 2008. Kama kwa
miaka minne, taifa
limeshindwa kukamilisha
utekelezaji wa maazimio ya
bunge kwenye suala moja,
haiwezekani umma ukaamini kwamba utekelezaji wa
maazimio mengine ya bunge
mathalani ya Novemba 2011
uchunguzi wa sekta ndogo ya
gesi asili au utekelezaji wa
maamuzi ya serikali kuhusu uchunguzi ulioanzishwa hivi
sasa juu ya watendaji
waandamizi katika Wizara ya
Afya kufuatia mgomo wa
madaktari. Hivyo bunge na serikali lazima
kwa pamoja vyombo vyote
vionyeshe kwa vitendo
kumaliza masuala haya ili
kuweka misingi ya
uwajibikaji katika masuala mengine; Sekretariati ya
Maadili ya Viongozi wa Umma
nayo ni mamlaka ya kuweza
kuwachukulia hatua
waliokiuka sheria ya maadili
ya viongozi wa umma katika masuala hayo na mengine. Hivyo, narudia kusisitiza
kwamba uwepo wa sheria na
kanuni za maadili pekee
hauwezi kusaidia iwapo
kanuni hazisimamiwi, na pia
hauwezi kusaidia iwapo kanuni ni mbovu. Mwaka 2010
nilieleza kwamba Sheria na
kanuni husika hazina meno ya
kutosha lakini hata yale meno
kidogo yaliyopo hayang’ati;
kwa kuwa hakuna hatua stahili zinazochokuliwa. Wakati huo nilieleza bayana
kuwa Sekretariati haijawahi
kutoa taarifa ya yoyote
kuhusu aliyewahi
kuchukuliwa hatua za kisheria
kwa kutokutangaza mali zake ama kutoa taarifa za
zisizokuwa za kweli katika
fomu husika; hivyo kutolewa
kwa taarifa ya sasa kuwa
uhakiki umeanza iwe ni hatua
ya mwanzo tu kwa ajili ya mamlaka husika kuchukua
hatua zaidi. Pamoja na udhaifu
wa sheria, changamoto
kubwa zaidi ni
kutokusimamiwa kwa
utawala wa sheria ambao katika suala hili la maadili
wahusika wakuu katika
kusimamia sheria husika ni
ofisi ya Rais na sekretariati ya
maadili ya viongozi wa umma.

John Mnyika (Mb) 15/02/2012
 
Napenda sana jinsi ambavyo unavyota REACTIONS mapema pale ambapo kuna jambo linalokuhusu wewe kama kiongozi au jambo linalohusu CHADEMA.

KEEP IT UP BRO
 
Mara zote huwa huko makini na unachoandika na hata kusimamia kile unachoongea! Palipo na ukweli lazima ukweli usimame....... Bravoooo!!!!
 
hivi huyu alisoma shule gani, maana naona anaongea points tupu;

Serikali badala ya kusimamia mambo ya Taifa na kanuni / sheria walizoweka; Sheria wanatunga wenyewe kisha wanavunja wenyewe.

Kutwa wanafikiria kuwajadili watu na wanafikiria kuifunga JF.

HAYA JITETEEENI NA HILI NALO KUHUSU KANUNI ZENU NA KATIBA YENU YA JMT.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hata mimi hii tume ya maadili ya viongozi wa umma imeniacha kinywa wazi?
It is wastage of our meager resources. Kama wangekuwa makini wangeaza kwanza
na wale wote waliogoma kujaza hizo forms za kutaja mali zao mfano Mch. Rwakatare.
Next wangefuata wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kwa kuanzia na ile LIST OF
SHAME aliyoitaja Dr. Slaa.

Then wakishamaliza kuzihakiki what next?

Hili li-tume nalo limekosa maana limekuwa kama kichaka cha kuwaficha viongozi.
Hivi inaingia akilini eti kuhakiki mali za Mnyika na wala sio mtu kama Chenge?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom