J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'

Mnasema Lowassa ni Tajiri ana uwezo wa kununua wajumbe na ameshaweka mtandao wa kumpitisha 2015! Kumbuka pia J.K.Nyerere aliwahi kusema yafuatayo baada ya kucheki afya yake ''Hivi sasa nina afya njema na nina uhakika nitamwona Rais ajaye wa awamu ya nne yaani 2005'' Je alimwona?

Kumbukeni yafuatayo: Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie Roho;
Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa;
Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile;
Wala Uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea. ( Ecclesiastes. 8:8).


Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za Mauti! ( Mithali.14:12)
 
Mimi siamini kwamba EL hajui anachofanya ndani ya ccm kwa sasa! Anajua fika kuna vikao vya cc, nec na mkutano mkuu. Anajua kuwa ili apitishwe na chama lazima apite kote huko. Siamini kama anao uwezo wa kupanga safu katika nec na mkutano mkuu ambako kote kuna wajumbe wengi zaidi ashindwe kupanga safu katika cc? EL anajua anachofanya na anajua kuwa with money in tz nothing impossible. My take: wapenda mabadiliko wote tufurahie kwa lowasa kupitishwa na ccm maana hawezi kuhonga wa tz 10m wamchague hivyo kazi itakuwa rahisi kuimaliza ccm.

sasa nakale ka-tume ketu ka uchaguzi chini ya katiba hii, hakata-hongeka kweli? au katiba mpya itatengemaa kabla ya siku?
 
Mnasema Lowassa ni Tajiri ana uwezo wa kununua wajumbe na ameshaweka mtandao wa kumpitisha 2015! Kumbuka pia J.K.Nyerere aliwahi kusema yafuatayo baada ya kucheki afya yake ''Hivi sasa nina afya njema na nina weza kumwona Rais ajaye wa awamu ya nne yaani 2005, biblia inasema binadamu ataishi miaka makumi mawili matatu na kumi moja(yaani miaka 70) na akijaliwa zaidi ataishi miaka makumi mawili manne(yaani miaka 80) lakini akiishi zaidi ya hapo ni matatizo kwa hiyo naombeni msiniombee matatizo''

Kumbukeni yafuatayo: Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie Roho;
Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa;
Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile;
Wala Uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea. ( Ecclesiastes. 8:8).


Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za Mauti! ( Mithali.14:12)

alisema hayo kwenye red na sio vinginevyo.
 
900million per month. Na vitega uchumi kibao. Huyu ni billionaire, anataka nini kingine? Usultani? Seriously kuna watu hatari
 
Imetulia, na mwandishi wa makala hii ni mtu mkubwa mwenye kujua mengi zaidi ya aliyoandika, na kilichosemwa kimeakisi ukweli na historia ya ukweli kuhusu Lowasa. Mtu asiyeonyesha wazi vyanzo vya mapato yake akishakalia ikulu ni balaaa. Ukoma huu tuukimbie kwa jitihada zote.

Kama walifikiri Nyerere akifa kila kitu kimekamilika
kujisafishia njia kumbe nchi hii ina wenyewe.
 
Sasa kama afya yake sio nzuri kelele za nini?

Pigieni debe wagombea wenu.

Nani humu anaweza kuthibitisha ENL amesema anagombea 2015? Wapi alisema hayo?
 
CANDID SCOPE

MKUU NIMEKUSOMA VIZURI. Wengi walifikiri Kikwazo ni Nyerere hivyo baada ya yeye kufa basi mambo yao yatakua SHEGA. MPUUZI wa kwanza kufikiria hivyo ni Malecela kwani baada ya Nyerere KUWAFUKUZILIA MBALI LOWASA NA MALECELA NA KUTISHIA KURUDISHA KADI . 2005, Malecela alijaribu but hakuvuka CC. 2015 itakua zamu ya Lowasa nae hatavuka CC. HABARI NDIO HIYO
 
Uchaguzi wa wazazi umejaa lowasa. Yaani magazeti ya leo yamejaa habari za watu kupokea lowasa kuanzia elfu 40 na wengine boksi moja.

Yaani mtu hawezi kushinda uchaguzi bila kutoa lowasa!!

Mwananchi limeweka wazi kila kitu. Yaani watu walikua baa ya chako ni chako wakipewa lowasa baada ya kuona gari linapaki wakadhani ni pccb wakatimua mbio!

Mkutanoni watu watajaa kwenye vyoo kunako makimba wakigawiwa lowasa, kwa mama ntilie kwenye vibanda vya simu kote huko ni lowasa tu zinagawiwa!!!
 
Huyo marehemu/ hayati J. K. Nyerere alikuwa anafaa kuwa Rais? Kama alifaa mbona mpaka leo tuko kwenye lindi la poverty? na kwa nini alijifanya kung'atuka?!
 
AMINIUSIAMINI

UMENIFURAHISHA MKUU. Unajua kuna vijana wachache wao njaa zinawasumbua ila nafurahi kua wengine tumeanza kuwaelewesha na wanaonekana somo wanaanza kuliellewa eg WISEMAN na MZEE WA POINTI hatimae maoni yao sasa ni mazuri kuas mtu anaetoa LOWASA POPOTE na sio tu kugombea URAIS HAFAI KABISA. Tusijikite tu kewenye urais twende mbali zaidi na kuhakikisha RUSHWA AKA LOWASA TUNAITOKOMEZA. YES WE CAN
 
"Lowasa ni mmoja kati ya mafisadi wakubwa nchi hii niliowataja mwembe yanga. Licha ya yeye kunitishia kunipeleka mahakamani hadi leo hajafanya hivyo. Anaogopa nini? Lowasa anahonga sana aende Ikulu. Lakini mimi namwambia wale wote waliosema Chadema haiko mikoa ya kusini sasa wameumbuka. Umati huu umewaumbua pamoja na matawi yote haya.Lowasa anapaswa kwenda Keko sio Ikulu"- DR W. SLAA, Tandahimba, Mtwara.
 
ANDATE

Kati ya watu woote waliotoa comment wewe umenifurahisha sana. Mimi huwa napenda sana watu tunapojadiliana kwa kutoa mawazo huku tukitoa hoja nzito na NUKUU za kusupport hoja zetu. Mkuu hiyo nukuu ya Nyerere kuhusu afya yake nimeikubali! Big up
 
Kama rushwa ingekua inatungisha mimba wanazi wa lowasa wengekua wajawazito. Naamini baadhi ya great thinkers wengekua sasa wanahudhuria clinic...lol. Sitakaa kimya hata kidogo kuona rushwa ndio inampa mtu uwezo wa kutuongoza. Never. Mtoto wa mkulima hata kama ana uwezo mzuri au amesoma chuo kikuu asipewe uongozi simply because hatoi lowasa!!!! Tuichukie lowasa maana lowasa ni adui wa haki hiyo ni ahadi no 5 ya mwana tanu, 1965
 
Ni vibaya kuizungumzia maiti. lakin siku zote historia inabaki kuhukumu. Na pasi na shaka sote itatuhukumu kama inavyohukumu wenzetu waliotangalia mbele ya haki.

Nyerere alipiga sana kelele suala la Rushwa. Ukitazama kiundani zaidi na kuangalia Historia ya Rushwa kwa Tanganyika utagundua yeye Nyerere ndio aliasisi rushwa wakti wa uongozi wake kwani wakti wa mkoloni hakukuwa n rushwa. Tujiulize kwaninirushwa ilianza wakti wa uongozi wa Nyerere?

Nyerere huyu huyu ndie alietesa wananchi wake kwa kuondoa bidhaa madukani na kusababisha ulanguzi tanganyika. Nyerere huyu huyu alipiganisha vita vya Uganda kwa nia tu a kutaka kumrudisha madarakani swahiba wake Obote na kuuwa wananchi wake wengi na.

Nyerere huyu huyu aliwaambia wananchi wake wafunge mikanda ya kiuchumi kwa miezi 18 na alisahau kuwaambia wafungue kitu ambacho kinawasibu mpaka leo.
Nyerere huyu huyu aliwaondoa confidence raia wake kitu ambacho mpaka leo wananchi wake hawajiamini kwa lolote.
Nyerere huyu huyu alijawa porojo za kisiasa na kusahau uchumi.

lakin kubwa zaidi matatizo yoooote ya Tanganyika yanatokana na msingi mbovu ulioasisiwa na Nyerere kwa nchi yake tanganyika.
 
Lowassa hatokubali kuanguka kirahisi kwa namna yoyote. Hadi sasa Lowassa hajajibu tuhuma juu yake zaidi ya kutoa angalizo kuwa hakuna alichofanya bila baraka za Rais.......sasa badala ya kutazama tu kuwa watatumia kigezo cha minutes za Mkapa na tapes za Mwalimu jiulize Lowassa ana kadi gani mkononi mwake na vipi atazicheza
 
wapendwa wana JF.

najua baada ya kusoma title ya thread hii, wengi wenu mtamaka "here we go again!".

i have to declare my interest first. mimi ni mfuasi mkubwa wa falsafa na mitizamo ya marehemu mwalimu JKN. so, it goes without saying that i strongly supported mwalimu when he disapproved EL for presidency back those years. i still believe kwamba mwalimu was very right - i must quickly add "at least under circumstances at that point in time".

topic ya thread hii si kitu kigeni sana kwenu i know...ninachofanya ni kujaribu tu ku-inject a slightly different tone!

ninatambua kuwa EL amejadiliwa sana humu jamvini - both negatively and postively. while integrity yake imekuwa questioned na wapinzani wake kwa upande mmoja, kwa upande mwingine wale wanaomuunga mkono wana-cite "uchapaji kazi wake uliotukuka".

richmond scandal imekuwa ikitumika sana kumkandamiza EL. lakini sote tunajua kuwa EL alikuwa anasimamia maamuzi yaliyopata baraka zote kutoka kwa boss wake JK. hapa juzi juzi prof muhongo amefanya heroics pale TANESCO ambazo zina viashiria vyote, japo si kwa scale, vya yale maamuzi ya EL kwenye richmod. lakini mwisho wa siku mmoja anaitwa shetani while mwingine anaitwa malaika!

EL ni tajiri, yes. but tell me who isn't. mathalani kamanda wangu mbowe ni tajiri, does that rule him out as a potential presidential material? i dont think so!

lengo la thread hii ni kupendekeza tuwe na objective approach ya kuwapima watu ambao tunawatarajia wawe au wanaoonekana wana nia ya kuwa viongozi wetu.
kutoa sweeping statements kama "so and so ni tajiri kupindukia, mhuni, etc" is not only unscientific but also very mediocre. honestly, hatuwezi kumpata kiongozi aliye na sifa za malaika - atakuwa na hili zuri na pia atakuwa na jingine baya. cha msingi ni kuwepo kwa a measurable criteria.

why, then, dont we design a formula that will lead us to quantify all the important components and attributes of a leader that we are all dying to get for that highest position? for instance, JK alichaguliwa kutokana na bashasha zake (a big mistake) bila ya kuangalia maeneo mengine yanayo-matter zaidi. kwa nini tuendelee kufanya makosa yale yale?

mind you am not here to champion for EL course, far from it, si chaguo langu. ninachokiongelea hapa ni kutoa hukumu ya haki kwa wote.
vile vile kwa vile EL ni miongoni mwa starring aspirants for 2015 presidency nimeonelea nimtumie tu kama mfano katika kutafakari juu ya kiongozi atakayetufaa.

this is not fantasy thinking, it is real!
 
WAGOMBEA 17 WA CCM 1995

Mwaka 1995, walijitokeza wagombea wanaccm 17 kuomba kuteuliwa kuipeperusha bendera ya ccm. Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na vikao 3 ie CC, NEC na Mkutano Mkuu. Kikao cha kwanza kilikua ni CC. Mwenyekiti wa kikao alikua Mwenyekiti wa ccm A.H. Mwinyi. Baba wa Taifa Mwl Nyerere alialikwa ili asaidie shughuli hii pevu.

Nyerere bila kumungunya maneno wala kupepesa macho, kama ilivyo kawaida yake kwenye masuala ya kitaifa alisema wazi kuwa MALECELA NA LOWASA HAWAFAI KABISA KUONGOZA NCHI HII. Nyerere alisema Malecela ana madhambi mengi na ameyaweka wazi katika kitabu ambacho pia alielezea udhaifu wa Kolimba. Kuhusu Lowasa, Nyerere alisema baada ya kua amepewa file confidential na watu wa usalama-"Huyu kijana wa miaka 42 tu amepata wapi utajiri wote huu?? S. Sita ambaye alikua Compaign Manager wa J. Kikwete na E. Lowasa kwa pamoja aliinuka na kumtetea sana Lowasa hadi kufikia kusema hizo ni tuhuma tu hazijathibitishwa na pia kua Lowasa ana mvuto mkubwa kwa wananchi na anakubalika sana.

Baada ya kusikia "upuuzi" huu Nyerere hakusubiri Sita amalize hadithi zake alimkatisha na kumwambia "Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa, na kama ni mzuri kanywe nae chai". Wana-CC wengine wajitahidi kuwatetea Lowasa na Malecela kwa nguvu kubwa maana tayari walikua na makundi. Kutokana na hilo Nyerere alisema "Niko tayari kurudisha kadi yangu ya chama, CCM sio baba yangu wala mama yangu. Kuna wagombea wana uchu sana wa kwenda Ikulu. Mimi nimekaa pale ikulu kwa miaka 25. Ikulu si mahali pa kupakimbilia, ni mzigo. Ukiona mtu anakimbilia ikulu ujue huyo ni wa kuogopwa kama ukoma hasa anapotumia pesa. Je amepata wapi hizo pesa na atazirudishaje??". Kutokana na tishio hilo pamoja na nguvu kubwa aliyokua nayo A. Mrema wa Nccr ilibidi wana-CC hao kunywea hivyo Malecela na Lowasa wakachinjiwa baharini. Majina 5 yakapelekwa NEC na hatimaye majina ma3 yakapelekwa Mkutano Mkuu (Mkapa, Kikwete na Msuya) na mwishowe Mkapa akachaguliwa kuwa mgombea wa CCM

UCHAGUZI WA 2005

Kama ilivyokawaida kikao cha kwanza cha kuchuja wagombea kilikua ni CC. Malecela, kwa mshangao wa wengi, naye pia aligombea na wakati huo alikua M/Mwenyekiti wa CCM. Kwa kutumia wadhifa huo, toka 1995 Malecela alizunguka nchi nzima na kufajhamiana na wajumbe wote wa vikao vyote muhimu hivyo wkt wa kuchukua na kujaza na kurudisha fomu yeye alikua wa kwanza kumaliza mchakato wote huo na takriban asilimia 85 ya wajumbe wa vikao vyote 3 walikua wanamkubali na Malecela mwenyewe na wapambe wake waliamini baada ya kifo cha Nyerere kusingekua na kikwazo tena. Mkapa,Mwenyekiti wa CCM alifungua kikao na kuwaonyesha alichosema Nyerere kuhusu Malecela. Wana-CC wengi walikumjegea hoja Malecela lakini hoja za msingi zilizojengwa na Mkapa na wengine kua chama kitashindwa kuonekana kinamuenzi Nyerere na pia itakua vigumu kumnadi MALECELA ambaye tayari alikua amechafuka. Hatimaye, kwa mara nyingine, Malecela akachinjiwa baharini. J. Kikwete ndiye akapererusha bendera ya ccm.

HARAKATI ZA E. LOWASA UCHAGUZI 2015

Licha ya Nyerere kusema Lowasa hafai na kwamba ni kijana mdogo mwenye utajiri mkubwa na mwenye uchu mkubwa wa kwenda Ikulu, Lowasa baada ya kujiuzuru uPM alianza jitihada kubwa mno za kutaka kuwa Rais wa TZ 2015. Katika jitihada hizo amefanya mambo mengi miongoni mwake ikiwa ni pamoja na 1. Kuweka mtandao mkubwa wa wapambe wake wakiwamo mawaziri lukuki waliomo kwenye Barza la mawaziri la sasa 2. Kuhakikisha kundi lake linaingiza watu wengi kwenye NEC 3. Kuhakikisha waCC na Wajumbe wengi wa mkutano mkuu nao wanakua upande wake 4. kugawa vyakula, kuku, ngombe mbuzi kama hana akili nzuri kwa watu na taasiis mbali mbali 5. kugawa na kuchangisha fedha kwa dini zote mbili ili asionekane mbaguzi 6. kutumia vyombo vya habari kumsafisha 6. kutumia wabunge mbalimbali kumsafisha na ikiwezekana mjadala wa Richmonduli urudishwe upya na pia amekua akiwalipa wetu wengi na vijana wake ili kumsafisha katika mitansao mingi ya jamii.

Lowasa amedaiwa kuwa ni fisadi mkubwa na kumekua na tuhumu kibao dhidi yake kama ifuatavyo
1. Amedaiwa kua ni mla rushwa mkubwa na kamwe hana moral authority kukemea rushwa
2. Amedaiwa alipokua AICC alitumia vibaya madaraka yake
3. Amedaiwa kua ni mgonjwa hivyo hawezi mikikimikiki ya uchaguzi na ya kuongoza nchi
4. Amedaiwa kutumia hela nyingi sana kuwaweka watu wake NEC hadi hela zilikua zikigawiwa vyooni, kwenye vibanda vya simu na kwa mama ntilie na vocha za simu
5. Anadaiwa akiwa Waziri wa Ardhi alitumia vibaya madaraka na kuuza viwanja hovyo hasa open spaces kwa wahindi
6. Ingawa alikua mtumishi wa serikali ana mahoteli mengi, majumba pamoja na jumba la ubalozi wa Africa Kusini.
7. Richmonduli
8. Ana utitiri wa vitega uchumi eg Alpha
9. Ni shareholder wa Vodacom analipwa 900M KWA MWEZI
10. Amekorofishana na swahiba wake JK

Hizi ni tuhuma ambazo ameshindwa kabisa kuzikanusha


MKUTANO WA KAMATI KUU 2015
Kwa maoni yangu, huu ndio mkutano utakaomchinjia baharini Lowasa na rundo lake la wapambe nuksi. Lowasa na Malecela wanafanana sana (1. wote wana uchu SANA wa kwenda ikulu, wote wana rundo la wapambe, wote watakua wamegombea mara 2)Mwenyekiti JK atakua na kazi ndogo tu. Kwanza atawaonyesha mkanda wa Nyerere 1995 aliposema
1. Lowasa ni kijana mdogo mwenye utajiri wa kutisha
2. Mtu anaekimbilia Ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma
3. Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
4. JK ataonyesha video na minutes za kikao cha CC cha 2005 ambapo Mkapa alitumia hoja za Nyerere za 1995 kumchinjia baharini Malecela.

Hivyo wote mnaotumia JIKI kumsafisha Lowasa na njaa zenu mjue fika mgombea wenu hauziki. Hivi CCM ikimteua Lowasa kuwa mgombea je itakua imetoa picha gani kwa wanachama wake? Je wanachama wataweza tena kusema mbele ya watu kua CCM ni chama CHA WAFANYAKZANI NA WANYONGE??

Mtu pekee ambae angeweza kumsafisha Lowasa ni Nyerere tu vinginevyo sioni mwingine. Tukumbuke kua nchi imegundua uwepo wa Uranium, gas na oil hivyo kumpa mtu mwenye hurka na uroho wa mali kama Lowasa ni kuipeleka nchi pabaya.

Ni imani yangu watu wengi watachangia na kutoa maoni yao ili nchi ipate Rais anayefaa na sio mtu anayetumia hela kwa namna ambayo haijapata kutokea hapa nchini.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!

Mkuu hongera kwa uchambuzi murua!
 
Back
Top Bottom