J.K. na uhuru wa mahakama.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Katika hotuba yake huko Shinyanga wakati wa kuzima mwenge, J.K pamoja na mambo mengine aliwawosia Watanzania kuwa na subira katika kuchukua maamuzi. Alisema ya kuwa siyo jambo la busara kuchua uamuzi wa jambo lolote lile huku ukiwa na jasba. Akitoa mfano, alisema kufuatia wimbi la kuuwawa kwa maalbino, tayari alikwishaweka kipengera katika mojawapo ya hotuba zake za mwisho wa mwezi, kilichotoa mwito wa kuwanyonga wahusika wa vitendo hivyo. Akifafanua zaidi alielezea ya kwamba alilazimika kukiondoa kipengere hicho baada ya kushauriwa kwamba hakuwa busara kuanza kuzungumzia kunyongwa kwa wahusika hata kabla ya kesi zenyewe kupelekwa mahakamani. Mbali na hayo alionekana kuiagiza mahakama kuchelewesha mchakato wa kukamilisha usikilizwaji wa kesi hizo mpaka hapo atakapokuwa amemaliza kipindi chake cha urais.
Kutokana na kauli hizo kunajitokeza mambo mawili yanayohusu uhuru wa mahakama kama mhimili: Jambo la kwanza ni kuhusu mpaka wa rais katika kuingilia mchakato wa uchunguzi wa matukio yanayo ashiria kuwepo kwa mazingira ya makosa ya jinai. Kama itakavyokumbukwa, wakati wa uchunguzi wa sakata la EPA rais alitoa amri kwamba wahusika wa sakata hilo, ambao kwa hiari watarejesha fedha walizokuwa wameiba (tena bila ya riba) hawatachukuliwa hatua zaidi. Hivi sasa kwa kauli yake hii anakili yeye mwenyewe ya kuwa hakuwa na madaraka ya kisheria kutoa msamaha huo. Lakini baya zaidi, wakati akionekana angalau kujisahihisha kwa makosa hayo anazidi kutenda mengine ambayo ni mabaya zaidi; nayo ni kuelekeza huo mhimili wa mahakama kulalia haki ya waathirika wa vitendo hivyo vya mauaji ya albino. Ikumbukwe tendo la kuagiza kuwa kesi hizo ziwekwe zuriani mpaka atakapong'atuka ni kuchelewesha haki; na hilo ni sawa na kumyima mtu haki
 
ulikaribia kuwa na hoja lakini naona hukusikiliza Hotuba vizuri. kwakuwa anania hiyo bac kwamaksudi watachelewesha kesi.
 
Back
Top Bottom