J.K, Mapinduzi siku zote duniani huanzishwa na "WAHUNI" Tusiwapuuze!

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kwa sasa ukisema tuuvunje muungano haimaanishi unauchukia ila ni busara tu hutumika.

Hata kama ni wachache hawautaki muungano tuuvunje kama UJERUMAN Na ikiwapo aja Na wananchi wakitaka tutaungana tena. Kama tumeoleana, tunaingiliana busara itumike. Utabaki undungu na urafiki. Sheria zitambue hilo.

Unajua tutaung'ang'ania na kuunda hoja za kuwatukana wasioutaka hatimaye zitajengwa chuki kali za watanganyika na wazanzibari na tutatengana kwa shari kama KOREA, ETHIOPHIA NA ERITRIA, SUDAN AU URUSI.

Kawaida waanzisha mapinduzi ni "wahuni" tu.
Wanaotumia ustaarabu sikuzote hawasikilizwi.
Wasomi wakianzisha huongwa vyeo kama Maalim Seif na Bilali.

Wahuni ndio wahanga wa ukosefu wa ajira, elimu bora na huduma bora za Afya ndio wanaoongoza mapinduzi.
Ila huja kusapotiwa na werevu baada ya mbinu za kihuni zaidi kutumika kuwadhiti.

Hoja za kutoutaka muungano Zilianza toka Mwalimu Jk akiwa madarakani. Wanasiasa mkazibadili mkaziita KERO ZA MUUNGANO.

Swali wazanzibari walioko selikalini watumishi wa uma walioko bara itakuwaje? HAO TUTAWACHUKULIA kama ilivyo kwa wachina kwenye ujenzi wa barabara au baadhi ya waasia wageni.

Waliooleana. Ata mzee Obama alioa Marekani.

Mjadala wa katiba uwe wazi kujadili uwepo wa muungano. Kuwapa nusu ya wajumbe haikuwa suluhu.

Nakushauri rafiki yangu jk wahuni ndio waletamapinduzi.
Huu ni ushauri wangu kwa jk.
 
Bwana William kama hao waliochoma kanisa huko Zanzibar wako kwenye kundi la wahuni basi hakutakuwa na haja ya kuwasikiliza hawa wauwaji
 
Ni ukweli usiopingika wanaoitwa wahuni ndio waleta mabadiliko sehemu yoyote husika duniani hata Marehemu Gadaffi kama asingefariki angelijua hivi kwani wale aliowaita (Mende) ndio walimtimua madarakani baada ya kutowasikiliza hatimaye ukamkuta umauti kwenye mtaro wa Mende,lakini ndugu zetu wa kisiwa cha Zanzibar katika tukio lao la kudai kuvunjwa kwa muungano wamekosea sana kuchoma moto nyumba za Ibada za waumini wengine wasio na hatia na muungano na sidhani kama makanisa yanazuia kutatua kero za muungano. ishara hii inaashiria kitu kingine kabisa ambacho kinaweza kuleta mtafaruku mkubwa katika jamii na inashagaza sana serikali imekubali vipi kikundi hiki cha wahuni ambao wamevalia vizuri akina mama wakiwa na Hijab zao akina baba wakiwa na Baraghashia zao na makanzu yao kama mtu angeliwagusa akavuta moja ya vazi lao shida ingelianzia hapo, je kikundi hiki nani kakipa hata uwezo wa kuandika mabango na kufanya maandamano makubwa yakiwashirikisha wanawake wengi tu wakipita mitaani hatimaye wengine kupata nafasi ya kuchoma moto nyumba za ibada ya madhehebu mengine inasikitisha sana tunakoelekea ebu tusubiri tuone IGP mwema na Itelegensia yenu ilikuwa wapi, Usalama wa Taifa ulikuwa wapi? Mujwahuzia
 
Wazanzibar walioko serekalini wako chini ya mwamvuli wa jamhuri ya muungano wa tanzania hivyo zanzibar ikiondoka inaondoka na chao na bara tunarudisha tanganyika chini ya serekali tutakayo ichaguwa bila kushirikisha wazenji na sisi tutachukuwa chetu. Kwa vile ccm ni muungano wa vyama 2 tanu ya tanganyika asp ya zanzibar na serekali ya muungano ilio chaguliwa na wazenji na wabara itabaki haina chake hivyo itajuwa pakwenda.
 
NI kweli... uhuni ni perception, na kwa context ya siasa, kila anayehoji rights zake huonekana mhuni hadi anapofika chumbani ndio viongozi hustuka

Madagascar is another example mhuni alichukua nchi na hadi leo jamaa bado anamuona rais yule (dogo janja mhuni), lakini ndio hivyo tena
 
Kwenye karne ya 19 wahuni walipewa jina maalumu na Karl Marx mwenye kumbukumbu atukumbushe jamani
 
Kwa vile ccm ni muungano wa vyama 2 tanu ya tanganyika asp ya zanzibar na serekali ya muungano ilio chaguliwa na wazenji na wabara itabaki haina chake hivyo itajuwa pakwenda.

kwa hiyo muungano ukivunjika hakuna ccm hamna tena maana ccm ina represent muungano.
 
HATA KAMA CHAMA KINAKUFA SIO VIZURI KUVUA NGUO ZENU ZA NDANI AMBAZO NI CHAFU NAMNA HII MBELE ZA WATU TENA WATU WAZIMA JAMANI HIKI NI KINYAAAA SISI SOTE TUNAUJUA UKWELI

ACHENI KUHARISHA HADHARANI CCM IMEKWISHA NA INAKWENDA ZAKE SASA MSIENDE NAYO NDIO MAANA MNAAMBIWA VUENI GAMBA VAENI GWANDA

m4c kwa ukombozi wetu PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZZZZ ZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ
 
M4C
HATA KAMA CHAMA KINAKUFA SIO VIZURI KUVUA NGUO ZENU ZA NDANI AMBAZO NI CHAFU NAMNA HII MBELE ZA WATU TENA WATU WAZIMA JAMANI HIKI NI KINYAAAA SISI SOTE TUNAUJUA UKWELI

ACHENI KUHARISHA HADHARANI CCM IMEKWISHA NA INAKWENDA ZAKE SASA MSIENDE NAYO NDIO MAANA MNAAMBIWA VUENI GAMBA VAENI GWANDA

m4c kwa ukombozi wetu PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZZZZ ZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ
 
Muhuni ni mtu yoyote anayedai haki kwa lugha ya watawala.

Wanaitwa hivyo sababu wengi hawana ajira hawana fedha na ni wahanga wa umasikini na huwa hawategemewi kuchukua nchi
 
Back
Top Bottom