ITV/Radio One vs CHADEMA kunani?

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Wakuu Salama?

Kuna suala leo limenitatiza sana ingawa limekuwa likijotekeza mara kwa mara katika mazingira fulani fulani

Habari kubwa kwenye magazeti almost yote ya leo ni Juu ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kugoma kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa kile alichoeleza kuwa hana imani na Jeshi hilo kwani limekalia taarifa nyingi za uchunguzi ikiwemo ile ya kutegewa kinasa sauti chumbani kwake kule Dodoma.

Aidha, habari hiyo ambayo inauza magazeti yote ya leo imeambatana na maamuzi mbalimbali ya kamati kuu ya CHADEMA iliyoketi kwa siku mbili.

Nimejaribu kufuatilia vipindi vya udondozi wa magazet kwenye TV na Radio kuanzia Star TV, RFA, Magic FM na Channel 10 kote wamesoma habari hiyo kubwa nchini. Maajabu ITV na Radio One kwenye vipindi vyao vya udondozi wa magazeti hawajasoma kabisa habari hiyo na mara zote watangazaji wamekuwa wakiudanganya umma kuwa, habari iliyopamba magazeti yote ni ile ya Rais wa Jumuiya ya madaktari kufikishwa mahakamani.

Kinachokera zaidi, Mwandishi anasoma; nanukuu "Katika Gazeti la Tanzania Daima habari kubwa iliyopamba ukurasa wa mbele ni ile isemayo MADIWANI 22 WA CCM MISUNGWI WAJIORODHESHA KUHAMIA CHADEMA" wakati habari kubwa ni ya Dkt. Slaa.

Aidha, taarifa za habari za jana kwenye TV stations zote hakukuwa na habari hiyo ya CDM isipokuwa Channel ten pekee. Niliikodolea macho ITV bila mafanikio.

My Take
-Hivi ITV/Radio One kuna nini hadi kwa makusudi wanaudanganya umma juu ya habari kubwa kwenye magazeti ya leo?
-Kuna tatizo kati ya ITV/Radio One na CHADEMA?
-Inakuwaje mhariri/mwandishi anaruhusu upotoshaji na upindishaji wa ukweli makusudi?

Nawasilisha...
 
Ni ukweli kabisa.Inawezekana wana agenda ya siri au wamepigwa mkwara na serikali ya magamba tangu warushe jangwani hewani.Ila tunamuomba mwenyekiti wa IPP aingilie kati kwa hili tutakuwa hatuchune hii ITV.
 
hata mengi hana imani na vyombo vya usalama sasa nitashangaa mbaba huyu kama hata waunga mkono chadema kwa hili..vinginevyo anaendeleza ukada wake kwenye chama cha mabwepande..hivi kesi ya mtoto wake kutaka kushikishwa madawa ya kulevya..
 
Wakuu Salama?

Kuna suala leo limenitatiza sana ingawa limekuwa likijotekeza mara kwa mara katika mazingira fulani fulani

Habari kubwa kwenye magazeti almost yote ya leo ni Juu ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kugoma kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa kile alichoeleza kuwa hana imani na Jeshi hilo kwani limekalia taarifa nyingi za uchunguzi ikiwemo ile ya kutegewa kinasa sauti chumbani kwake kule Dodoma.

Aidha, habari hiyo ambayo inauza magazeti yote ya leo imeambatana na maamuzi mbalimbali ya kamati kuu ya CHADEMA iliyoketi kwa siku mbili.

Nimejaribu kufuatilia vipindi vya udondozi wa magazet kwenye TV na Radio kuanzia Star TV, RFA, Magic FM na Channel 10 kote wamesoma habari hiyo kubwa nchini. Maajabu ITV na Radio One kwenye vipindi vyao vya udondozi wa magazeti hawajasoma kabisa habari hiyo na mara zote watangazaji wamekuwa wakiudanganya umma kuwa, habari iliyopamba magazeti yote ni ile ya Rais wa Jumuiya ya madaktari kufikishwa mahakamani.

Kinachokera zaidi, Mwandishi anasoma; nanukuu "Katika Gazeti la Tanzania Daima habari kubwa iliyopamba ukurasa wa mbele ni ile isemayo MADIWANI 22 WA CCM MISUNGWI WAJIORODHESHA KUHAMIA CHADEMA" wakati habari kubwa ni ya Dkt. Slaa.

Aidha, taarifa za habari za jana kwenye TV stations zote hakukuwa na habari hiyo ya CDM isipokuwa Channel ten pekee. Niliikodolea macho ITV bila mafanikio.

My Take
-Hivi ITV/Radio One kuna nini hadi kwa makusudi wanaudanganya umma juu ya habari kubwa kwenye magazeti ya leo?
-Kuna tatizo kati ya ITV/Radio One na CHADEMA?
-Inakuwaje mhariri/mwandishi anaruhusu upotoshaji na upindishaji wa ukweli makusudi?
Nawasilisha...
Mi naona hiyo habari iliyosomwa ni nzuri sana tu kwa cdm!...wala usihofu!
Ukiikwepa CDM kwenye tea-break utakutana nayo Lunch- break!....Nowhere to hide!
 
Mi naona hiyo habari iliyosomwa ni nzuri sana tu kwa cdm!...wala usihofu!
Ukiikwepa CDM kwenye tea-break utakutana nayo Lunch- break!....Nowhere to hide!

Asante kaka,kwa kukazia Chadema ni Kama maji vile usipoyanywa utayakogea sema wachache sana hawaukubali ukweli huu.
 
Mi naona hiyo habari iliyosomwa ni nzuri sana tu kwa cdm!...wala usihofu!
Ukiikwepa CDM kwenye tea-break utakutana nayo Lunch- break!....Nowhere to hide!

Mkuu lengo langu halikuwa kueleza habari ni nzuri kwa CDM au laa bali kuonesha jinsi mwandishi anavyoweza kuudanganya umma kuwa, habari kubwa ni hiyo ya MADIWANI 22 WA CCM KUTAKA KUHAMIA CDM wakati ni tofauti.Nimekupata lakini.
 
Mengi atakuwa ana bifu na cdm,mengi akitofautiana na tasisi fulani ni haramu kusoma habari ya iyo tasisi..rejea bifu la yanga na Mengi same to Simba too..mara nyingi inakuwa ni order.MENGI NI MUNGU MTU
 
wamempa sifa nyingi sana juzi wakati akipokea tuzo kutoka kwa viongozi wa dini na mzee mwinyi alitumia muda mwingi kumpamba ndugu MENGI. Kwa hiyo kinchoendelea hapa ni mgema amesifiwa sasa anaweka tembo maji
 
Uhuru wa kuchagua cha kuandika,kuònyesha uko mikoni mwao so its okay kufanya wanachoona sawa kwao
 
Ulichokisena ni ukweli mtupu. ITV/Redio One huwa hawasomi taarifa ambazo zimo ktk magazeti hasa zile za CHADEMA. Mimi nilifuatilia Jumatatu juu ya habari zilizotolewa na CHADEMA jpili ambapo magazeti yote yaliandika habari hizo. Lakini Redio One hawakuzisoma habari hizo. Nikawauliza hata wenzangu.."Hivi kwanini Redio One wanasoma habari ambazo hazipo magazetini?" Wakanijibu Redio One ndio kawaida yao. Kama wanafuatilia uzi huu, basi wabadilike.
 
mengi nae si kigeugeu yule.. kwanza hajulikani ata ni chama gani
 
Kwani habari kubwa ni ile iliyoandikwa kwa maandishi makubwa au yenye impact kubwa?nifahamisheni wanahabari
 
Uhuru wa kuchagua cha kuandika,kuònyesha uko mikoni mwao so its okay kufanya wanachoona sawa kwao
Issue siyo kuandia issue ni kusoma magazeti yalichoandika kwanini hukwepa kusoma habari zinazoihusu chadema aau tuwasusie kama TBC...........
 
mengi nae si kigeugeu yule.. kwanza hajulikani ata ni chama gani

Sidhani kama ni Mzee Mengi anaelekeza haya wanayofanya. Ni woga tu wa waandishi hawa na kutafuta kujipendekeza. Ni jambo la ajabu kupindisha mambo yaliyo wazi. Yaani nyeusi unaiita nyeupe wakati kila mtu anaona ni nyeusi. Inabidi uwe na akili ya matege kidogo.
 
ITV/Radio one ni vyombo vya habari vilivyozeeka na vimepitwa na wakati wakuu imani yangu ilishaamia chanel ten wakati nikisubiri mwananchi TV wailaunch...tokea jumatatu niliwaona kuwa ni wapotoshaji tena wana upotoshaji wa kitoto bcoz jumatatu hawakusoma vichwa vya habari za mbele za mwananchi,nipashe na tanzania daima badala yake waliyasoma mwishoni habari za michezo wakati wakisoma magazeti kwa nyuma.nilimcheck yule dada na simbeye nikawaona kama wanafiki nikabadidi chanel kwakweli hawa wanapotosha umma na wanaonyesha hawako consistence na habari zao sijui wanamdanganya nani wa leo
 
Back
Top Bottom