ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu..

Mkuu mimi sijamlaumu Mengi hata mahali pamoja na ndio maana nimesema ITV nikijua kuna uongozi na kuna wanaofanya maamuzi ys moja kwa moja ingekuwa Mengi ningetaja moja kwa moja Mengi,ila watu wameng'ang'ania
mara sijui wivu kwa Mengi mara nimetumwa na Manji vitu vya ajabu kabisa.

Watu wengi tunadhani kukosoa ni kuchukia,binafsi kwangu Itv ndio Tv yangu ya kwanza na bila kuangalia habari Itv naona bado sija angalia habari,lakini haya ndio maoni yangu juu ya swala hili hivyo kusema ni haki pia.
Prog. ya udhalilishaji ni ile ya EATV na siyo ile ya ITV!. EATV inaendeshwa na binti, sasa kitendo cha wao kualikwa kwa mara ya kwanza, tena kufanya kazi ya baba!, wakajituma vilivyo ili kuonyesha uwepo wao na kumuipress bosi mtoto na big boss wakaishia ku overdo!. Wasemehe maana walifanya in goodfaith!

Kwa vile wenye ulemavu wenyewe hawajalalamika, nashauri kubali yaishe usije piga kelele mwishowe wenyewe wakalalamika kweli kuwa wamedhalilishwa!.
 
Iwapo thread kama hii imeshakuwepo mtaniwia radhi.

Hivi kumwalika mtu nyumbani kwako ndio lazima umuonyeshe mbele ya kadamnasi ya watu jinsi anavyokula,anavyokunywa na anavyocheza?
Mtu unapoamua kutoa tunaambiwa hata mkono wa pili usijue.

Nimeona jinsi EATV walivyowaonyesha wenzetu wenye ulemavu wakila na kucheza kama vile ni maajabu mtu mwenye ulemavu kucheza na kufurahi leo nimeona tena ITV wakitangazia kipindi maalum kuonesha jinsi
walivyo waalika wenzetu wenye ulemavu kwa kweli nimeshangaa hivi kumualika mtu kwako mpaka umuwekee kipindi maalum?

Vyama vya kutetea haki za wenye ulemavu mko wapi?

Hayo ni maoni na mtazamo wako hakuna shida. Lakini kwa upande mwingine jamii ya walemavu wanahitaji msaada kwa hali na mali. Kufanya hivyo kuna faida yake kwani kutafanya watu wengine wenye uwezo nao kufuata mkumbo. Huo ni ujumbe tu kwa jamii ya watanzania.
 
Hili limekuwa tatizo kubwa ktk jamii yetu, mtu anapotoa msaada atataka watu wote wajue na kama hakuna watu wa habari anaweza akaahirisha kutoa msaada huo!Iwe kupeleka watu India au kuona watoto yatima, Mungu ametuelewesha namna ya kufanya pale tunapotoa sadaka kumbuka Kaini na Habili wote walitoa sadaka mmoja ikakubaliwa mwingine ikakataliwa ni kwa sababu hakufuata utaratibu. Kuna wakati mi na wenzangu tulijipanga tukafanya ka-shopping kadogo tukaenda Ocean- road kuwaona wagonjwa, tuligawa vizawadi wodi kadhaa, Wauguzi walituuliza sana inakuwaje hamna watu wa habari!Tuache kujikweza, AJIKWEZAE ATASHUSHWA, huenda mzee wetu ameanza kushushwa maana popularity inatokomea taratibu.
 
Prog. ya udhalilishaji ni ile ya EATV na siyo ile ya ITV!. EATV inaendeshwa na binti, sasa kitendo cha wao kualikwa kwa mara ya kwanza, tena kufanya kazi ya baba!, wakajituma vilivyo ili kuonyesha uwepo wao na kumuipress bosi mtoto na big boss wakaishia ku overdo!. Wasemehe maana walifanya in goodfaith!

Kwa vile wenye ulemavu wenyewe hawajalalamika, nashauri kubali yaishe usije piga kelele mwishowe wenyewe wakalalamika kweli kuwa wamedhalilishwa!.

Au wenyewe wakasema namna ile ndiyo burudani kwao. Utakuwa umeumbuka, bora kupiga kimya tu.
 
Back
Top Bottom