ITV na udhalilishaji wa wenzetu wenye ulemavu..

...sio kuwasaidia tu ninaishi nao ndio maana nashindwa kuwaelewa hawa ITV.

Na wewe mbona unajifagilia hapa kuwa unawasaidia na pia unaishi nao? Kwanini usingekaa kimya tu ili upate hiyo "thawabu"? Unawasaidia na kuishi nao ili uje ujitangaze JF?
 
Nyie limewadhalilisha,

wenyewe walemavu wanalifagilia. Unafikiri walikuwa hawajui kamam wanachukuliwa picha? Si ndo kwanza walikuwa wanazikimbilia kamera? Kila mwaka si inaonyeshwa, wangekuwa wanaona wanadhalilishwa si wangegoma kwenda.....Kuna mmoja jirani yetu alivyotoka kwenye mnuso aliwaambia washkaji zake "leo mtaniona ITV" Bahati mbaya hakuonekana, alisikitikaje?

Kuuza sura kwa wengine ni deal jamani...... msimseme mzee wa watu.
 
Ndugu kumjali mtu mwenye ulemavu ni jambo
ambalo kila mwanadamu anapaswa na sina shida na hilo,lakini kuna maana gani kumjali halafu kumdhalilisha.

Muheshimiwa uliyemtaja hapo juu hatujui huenda hausiki moja kwa moja na maamuzi kama hayo ndio maana nikasema Itv nikijua kuna uongozi na watu wanaofanya maamuzi ya moja kwa moja.

Mfano mtu anapokuwa anakula ule ni wakati wake wa privacy,kwa nini umuonyeshe kwenye Tv tena unamvuta kwenye screen,wakati chakula umemuandalia wewe mwenyewe sasa unataka nani aone?wakati wale walikuwa ni wageni wako wewe?

Hapo kuna tofauti gani na kampuni ya simu inapotoa msaada kwa watoto yatima na kuita waandishi wa habari??

Na dhifa za taifa zenye makulaji zioneshwazo na TV, mfano alipokuja prince Charles na kuhostiwa na JK, nazo ni udhalilishaji? Si walionesha watu wanakula?
 
Na wewe mbona unajifagilia hapa kuwa unawasaidia na pia unaishi nao? Kwanini usingekaa kimya tu ili upate hiyo "thawabu"? Unawasaidia na kuishi nao ili uje ujitangaze JF?

Mimi nilikuwa najibu swali la mchangiaji aliyeniuliza.
Pili kuishi na mlemavu ambaye ni familia yako ni kujifagilia??
Na hizi nilizoandika ni hisia zao pia,wao kama watu wenye ulemavu hata kama ni wachache lakini ni walemavu na wamesikia kudhalilika kwa kile kinacho oneshwa Itv.
 
Na dhifa za taifa zenye makulaji zioneshwazo na TV, mfano alipokuja prince Charles na kuhostiwa na JK, nazo ni udhalilishaji? Si walionesha watu wanakula?

unawezaje kulinganisha hili na tukio la kuwaalika watu kwa kisingizio cha kuwajali na kuwaonesha kwenye TV,nini maana ya kutoa??
 
Nyie limewadhalilisha,

wenyewe walemavu wanalifagilia. Unafikiri walikuwa hawajui kamam wanachukuliwa picha? Si ndo kwanza walikuwa wanazikimbilia
kamera? Kila mwaka si inaonyeshwa,
wangekuwa wanaona wanadhalilishwa si
wangegoma kwenda.....Kuna mmoja jirani
yetu alivyotoka kwenye mnuso aliwaambia
washkaji zake "leo mtaniona ITV" Bahati mbaya hakuonekana, alisikitikaje?

Kuuza sura kwa wengine ni deal jamani...... msimseme mzee wa watu.

Lakini pia wapo ambao hawafurahishwi na kitendo hicho nao ni walemavu na wanasikia kudhalilika je hisia zao ni za kupuuzwa?

Kwa nini umualike mtu halafu uonyeshe mbele ya kadamnasi ulichomtendea,kwanza hata kwa tamaduni zetu kama waafrika ile si sawa hata kidogo.
 
Mimi nilikuwa najibu swali la mchangiaji aliyeniuliza.
Pili kuishi na mlemavu ambaye ni familia yako ni kujifagilia??
Na hizi nilizoandika ni hisia zao pia,wao kama watu wenye ulemavu hata kama ni wachache lakini ni walemavu na wamesikia kudhalilika kwa kile kinacho oneshwa Itv.

Kwani katika kujibu hilo swali kulikuwa na ulazima wa wewe kusema kuwa "ninawasaidia na kuishi nao"?

Hata ITV ukiwauliza kwanini walionesha hafla hiyo ya walemavu watakua na jibu la kuridhisha kama wewe ulivyoweza kujustify hapa kuwa ni kwa sababu uliulizwa na mwanaJF hapa!
 
unawezaje kulinganisha hili na tukio la kuwaalika watu kwa kisingizio cha kuwajali na kuwaonesha kwenye TV,nini maana ya kutoa??

Tofauti ni ipi ya hafla ya mengi kwa walemavu na dhifa ya taifa kwa wageni wa nchi? Yaani unaona ni sawa kwa nchi kupata mgeni na kuutangazia ulimwengu kuwa "leo nina mgeni ntamlisha na kumnywesha"?
 
Iwapo thread kama hii imeshakuwepo mtaniwia radhi.

Hivi kumwalika mtu nyumbani kwako ndio lazima umuonyeshe mbele ya kadamnasi ya watu jinsi anavyokula,anavyokunywa na anavyocheza?
Mtu unapoamua kutoa tunaambiwa hata mkono wa pili usijue.

Nimeona jinsi EATV walivyowaonyesha wenzetu wenye ulemavu wakila na kucheza kama vile ni maajabu mtu mwenye ulemavu kucheza na kufurahi leo nimeona tena ITV wakitangazia kipindi maalum kuonesha jinsi
walivyo waalika wenzetu wenye ulemavu kwa kweli nimeshangaa hivi kumualika mtu kwako mpaka umuwekee kipindi maalum?

Vyama vya kutetea haki za wenye ulemavu mko wapi?
wanaotakiwa kulalamika ni wao au ni wewe?
unataka Mengi asiwasaidie tena?
INAONYESHA KIASI GANI AKILI YAKO HAIWEZI KUFAFANUA MAMBO,UNGETAFUTA MAANA YA UDHALILISHAJI KABLA YA KULETA MADA YAKO HAPA
 
Tofauti ni ipi ya hafla ya mengi kwa walemavu na dhifa ya taifa kwa wageni wa nchi? Yaani unaona ni sawa kwa nchi kupata mgeni na kuutangazia ulimwengu kuwa "leo nina mgeni ntamlisha na kumnywesha"?

Hivi Prince Charles anasikia kunyanyapaliwa au kutengwa na jamii??

Nini maana ya kumualika mtu kwa kusema unamuonyesha ukarimu ili asijisikie ametengwa halafu unamuonesha kwa kadamnasi jinsi ulivyomuhudumia?
Kwani wangesema tu walikula na kunywa na walemavu isingetosha?
Wanamuonyesha nani wakati wale walikuwa wageni wao?
Kumkarimu mtu mpaka uonyeshe kwenye tv??
 
wanaotakiwa kulalamika ni wao au ni wewe?
unataka Mengi asiwasaidie tena?
INAONYESHA KIASI GANI AKILI YAKO HAIWEZI KUFAFANUA MAMBO,UNGETAFUTA MAANA YA UDHALILISHAJI KABLA YA KULETA MADA YAKO
HAPA

Ninao watu wenye ulemavu ambao ni member wa familia yangu,na wamejisikia kudhalilika kwa wanachokifanya ITV,na nafikiri mawazo yao yanahitaji kuheshimika pia.

Pili kumsaidia mtu au kumualika nyumbani kwako kwa kusema unamuonyesha ukarimu kuna haja gani tena utangazie dunia nzima??
 
hatukatai kuwajali sasa maonyesho yote yale ya nini? Hv unazijua haki za walemavu linapokuja suala la kuwaripoti? Sheria zipo ila sema nchi yetu ukiwa na pesa basi hata akikusaidia kisha akakudhalilisha bado utalazimika
kumlamba miguu!!! Penye ukweli muwe
mnatafakari angalau sio kutukuza tu just b'coz
ni mengi kawasaidia!!

Tatizo watu wanawabeba watu mioyoni mwao mpaka wanaona hawastahili kukosolewa.
 
Comment yangu

Mimi nadhani hisia zako ndio zinakufanya uone kama unadhalilishwa, kwani
hakuwaalika ili kuwasaidia bali nijuavyo mimi
huwa anafanya kama "Walemavi Day" kwa
hiyo ni sawa kuwaonesha na kuweka kipindi
maalum kwa sababu siyo kipindi rasim ITV
ndio maana kinaitwa hivyo. Na lengo ni

kuionesha jamii namna walemavu
wanavyoweza kufanya mambo mbalimbali ya
kiubunifu katika jamii, tungejuaje vikundi vya
ngoma, muziki na vingine kama
wasingeoneshwa?

Pia sherehe kama sherehe ikifanywa na jumuia yoyote ya watu si mbaya kuoneshwa kwa vyombo vya habari, mfano makampuni ya Company's Day kwa kila mwaka mbona huonesha kwenye vyombo vya habari jinsi walivyosherekea?
Mtoa maada inavyooneshwa umeathiriwa na MILA YA KUWAFICHA WALEMAVU ambayo waafrica wengi imetupotosha hata kushindwa kutembea nao na kuwaficha majumbani wasiende shule.

Kipindi maalumu kinatuwezesha tuwaone wanavyoweza kuonesha vipaji vyao, ubunifu wao, na kutoa nafasi kwa wengine kuona kumbe ulemavu mwingine si lazima uwe ombaomba, unaweza kucheza kwenye mkusanyiko wa watu na watu wakakutuza na hiyo ikawa ajira yako kama baadhi ya walemavu wa macho pale Dodoma wafanyavyo stand na kwenye train badala ya kuombaomba

Ushauri,
Nadhani ni vyema mtoa mada ujikomboa kutoka kwenye Dhana ya kuwaficha walemavu kwa kuona kuwa wakionesha uwezo wao kutokana na ulemavu wao wataonekana wanajidhalilisha. Pili uwe mstari wa mbele kuwafanya walemavu waoneshe kwa umma / watu ni nini wanaweza kufanya ili watumie vipaji vyao kujipatia kipato kama wale
wacheza mziki wa TOT

Mkuu mimi naamini ktk haki za walemavu na watu wote kwenye jamii.
Ila wanachofanya ITV ni udhalilishaji wa hali
ya juu.

Pili haikuwa na haja ya kuonyesha kwa watu wakati uliyemualika tayari umesha mkarimu,halafu hivi ili mlemavu aoneshe kipaji chake lazima umualike kwa kisingizio
cha kumuonesha kumkarimu basi si bora uandae talent show kama unataka kutafuta hivyo vipaji.
 
Ninao watu wenye ulemavu ambao ni member wa familia yangu,na wamejisikia kudhalilika kwa wanachokifanya ITV,na nafikiri mawazo yao yanahitaji kuheshimika pia.

Pili kumsaidia mtu au kumualika nyumbani kwako kwa kusema unamuonyesha ukarimu kuna haja gani tena utangazie dunia nzima??
Mkuu Kiziza, tulio kuelewa tumekuelewa!.

Mimi nakuunga mkono kiasi fulani na kiasi fulani nakubaliana na ITV isipokuwa baadhi ya maeneo.
1. Kwanza kitendo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Mzee Reginald Mengi kuwafanyia tafrija jamii ya watu wenye ulemavu ni jambo jema, la kupongezwa na kuungwa mkono na kina mwenye mapenzi mema kwa sababu lengo ni kuwaonyesha hao wenye ulemavu jinsi unavyo wathamini. Big up Mengi for that!.
2. Kitendo cha kuionyesha hafla hiyo kwenye news kama tukio jingine lolote pia its right.
3. Kitendo cha kuandaa kipindi maalum kuhusu hafla hiyo kwa lengo la kuhamasisha wengine pia wawajali wenye ulemavu its a good move as well sambamba na kuonyesha vipaji mbalimbali walivyonavyo walemavu.
4. Kitendo cha kusaidia wenye ulemavu na kuwafanyia tafrija ili kuonyesha watu waone jinsi unavyosaidia, hiyo ni show off na ni wrong!. Kuna watu kibao wanaosaidia bila kufanya show off!.
5. Kitendo cha kuwaalika wenye ulemavu halafu kuwarekodi tena with close-up ili kuonyesha wenye ulemavu wanakula vipi au ili kuonyesha umma wenzetu wenye ulemavu wa viungo wanacheza vipi muziki licha ya mapungufu yao, huu kwa kweli ni kuingilia right to privacy ya wenye ulemavu na kuonye prolonged shots na close-ups za maumbile yao wakila au wakicheza, huku ni kuwadhalilisha!.
6. Kwa vile the deviding line betwen publicity ya kusaidia ili uonekane unasaidia (show off) na kuonyesha ili kuhamasisha wengine wasaidie is very thin, na kwa sababu Mzee Mengi kusaidia wenye ulemavu haajaanza leo nawaombeni tuendelee kumuaminia anasaidia in good faith na sio for show off, ila hao wanaofanya hiyo huo udhalilishaji sio yeye as Mengi bali watendaji wa vyombo vyake vya habari!.
7. Hafla hiyo bado ingeweza kurekodiwa kipindi maalum bila ya udhalilishaji wa watu wenye ulemavu kwa production team kuwa a bit considarate warekodi nini na kuonyesha nini na kwa muda gani. Kitendo cha kiyaonyesha maungo ya wenye ulemavu for too long sio kuwapublicise bali kuwadhalilisha!.
 
Ninao watu wenye ulemavu ambao ni member wa familia yangu,na wamejisikia kudhalilika kwa wanachokifanya ITV,na nafikiri mawazo yao yanahitaji kuheshimika pia.

Pili kumsaidia mtu au kumualika nyumbani kwako kwa kusema unamuonyesha ukarimu kuna haja gani tena utangazie dunia nzima??

Hao watu wa kwenu walionekana kwenye TV?KAMA HAWAKUONEKANA basi ujue hawakutaka kuuza sura na kama wanahic ni uzalilishaji wasiwe wanafiki wasiende tena wawaachie wale wanaoburudisha nafsi zao na kupenda kuonekana kwenye TV.wakihisi kudhalilishwa wasiende kabisa.

Tumezoea sherehe zote hunyehwa watu wanavyosherehekea, kama mizinga na askari ck za sikukuu za kiserikali,harusi na mengine leo kuonyeshwa walemavu tu umekuwa udhalilishaji?au kwakuwa walisaidiwa? acha hisia zako mbovu na kuchafua TV za watu kama huna la kuongea kaa kimya tu
 
vipi wale jamaa wa mabaga fresh wanajidhalilisha bila kujua?? na wale wanaochukuliwa kucheza shoo .acheni dharau .mengi kaweza na wewe jaribu acha wivu na fikra hasi.
 
Hao watu wa kwenu walionekana kwenye TV?KAMA HAWAKUONEKANA basi ujue hawakutaka kuuza sura na kama wanahic ni uzalilishaji wasiwe wanafiki wasiende tena wawaachie wale wanaoburudisha nafsi zao na kupenda
kuonekana kwenye TV.wakihisi kudhalilishwa
wasiende kabisa.

Tumezoea sherehe zote hunyehwa watu wanavyosherehekea, kama mizinga na askari ck za sikukuu za kiserikali,harusi na mengine leo kuonyeshwa walemavu tu umekuwa udhalilishaji?au kwakuwa walisaidiwa? acha hisia zako mbovu na kuchafua TV za watu kama huna la kuongea kaa kimya tu

Eti kudhalilisha tv za watu,
ndio tatizo tulilokuwa nalo kwenye jamii yetu,
kukosoa inaonekana ni kudhalilisha unatakiwa usifie tu,kwa sababu kwa tamaduni zetu kukosoa inamaanisha kumchukia muhusika.
 
Sioni kama kuna udhalilishaji wa aina yoyote muacheni mengi mtu wa watu bana.je na kwa wale wagonjwa wa moyo anao wapeleka india kwa jili ya matibabu ana kua anawadhalilisha wa gonjwa wa moyo? Endelea mengi malipo yako yapo mbinguni.
 
Back
Top Bottom