Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,580
- Thread starter
- #21
Mkuu Sly, kwanza samahani kwa kuchanganya lugha, kiukweli kuna baadhi ya maneno ukitumia lugha halisi ya maneno yenyewe ambayo ni professional vocabulary yake yanaeleweka kwa urahisi zaidi kwa lugha ya kutoholewa kuliko tafsiri rasmi ya Kiswahili. Kuna kutumia Kiswahili Sanifu na Kiswahili Fasaha. Kiswahili Sanifu ni ile lugha rasmi kwa mujibu wa kamusi, na Kiswahili Fasaha ni ile lugha ya kueleweka sio lazima iwe sanifu. Kuna maneno mengi tuu ni rahisi kuyatumia kwenye Kiswahili Fasaha kuliko Kiswahili Sanifu!Napenda kumshukuru aliyeandika mada hii na kuwezesha kuchambuliwa kwa ufasaha na ufanisi mkubwa kutoka kwa wachangiaji. Tatizo langu kubwa ni lugha iliyotumika, hivi ni kweli wote waliotumia maneno ya Kiingereza walikosa tafsiri yake kwa Kiswahili? Au ndiyo ufisadi mwingine ndani ya Taifa katika matumizi ya lugha? Angalia sana unapokuwa mkosoaji kwani huenda nawe unahitaji kukosolewa ila hujijui. Tuache mawazo potofu ya kwamba ili ujulikane kuwa umesoma na kuelimika lazima utumie maneno ya Kiingereza katika maongezi yako. Wafaransa, Wajerumani, Wajapani, Warusi, Wachina n.k nao watasemaje? Tuelimike na tubadilike.
Mfano
KIswahili Fasaha Kiswahili Sanifu
1. Friji - Jokofu
2. Mail - Barua Pepe
3. Dekoda - Kingamuzi
4. Dokta - Tabibu
5. John - Yohana
6. James - Yakobo
7. DC - Mkuu wa Wilaya
8. Vocha - Kadi Ongezeko la salio
9. TV - Luninga
10. SMS - Ujumbe Mfupi wa ...
Hiyo ni mifano michache ya maneno ya Kiingereza ambayo ni rahisi zaidi kutumika kwenye lugha fasaha lakini sio sanifu.
Ila pia kuna maneno ya kitaaluma ambayo bado hayana Kiswahili rasmi mfano " Morbid Curiosity" mengine mengi tuu yapo na yameshatoholewa hivyo hivyo kugeuka Kiswahili sanifu.
1. Secretariat
2. Oganaizesheni
3. Operesheni
4. Faulo
5. Shuti
6. Blog, FB na tweeter
7. Goli
8. Ligi
9. Jaji
10. Muziki
Na mwisho kuna maneno makali ukiyatumia kwa Kiingereza yanapungiua ukali kuliko ukiyatumia kwa Kiswahili mfano neno "very unprofessional', ukilitimia kwa kiswahili lina sound kama unamtukana!.
1. Shit ni M..vi
2. Fool ni Mpu...vu
3. Mad ni Kichaa
4. Insane ni Mwenda wazimu
5. Thick ni punguani
6. Homo ni Hani....
7. Gay ni Wase....
8. Sex ni Kut....
7. Sleep together ni Kula..na
8. Gold Digger ni wachunaji
9. Back ni Nyu...
10. Game ni mambo fulani
Kwa vile jf ni social media kama fb na tweeter hivyo matumizi yoyote ya kuchanganya lugha kwa madhumuni ya kufupisha, kueleweka kwa urahisi na kupunguza makali ni ruksa!.