ITV mmevuka mpaka

Kwanini inawauma sana wana cdm hajui hamshindi, nyie endeleeni na sera yenu ya nchi haitawaliki ila hata mkipewa nyie haita tawalika vilevile kwa sababu mmekwisha wajenga wananchi kuwa nchi haitawaliki.
 
Nafikiri tatizo la itv ni kubwa kuliko kuchanganya picha. Hawa jamaa hata wakikosea au mitambo yao ikipata hitilafu wakiwa hewani hata siku moja hawaombi radhi. Nafikiri mengi ana kazi kubwa ya kuwaelewesha kuheshimu wateja
 
Hii hata haisumbui wana wa Arumeru hawatafanya uchaguzi kwa kutumia propaganda za TV!

Unajua inasaidiaje?

Pale matokeo yatakapopindishwa,na CCM kushinda(maana ndiyo mpango uliopo)... Wengine tusishangae...
 
me nashangaa watun kazi kulalama lalama tu utadhani umati unaoonekana kwenye Tv ndo kura zenyewe,we ukioneshwa umati mkubwa inakusaidia nn wakati uko tanga,mbeya,mara na uchaguzi uko arumeru? waarumeru hawaitaji kuangalia tv kupiga kura coz wao ndo wanaohudhuria mikutani hyo,taarifa ya habari unaoneshwa wewe uliye mbali na arumeru ambayo huna effect yoyote katika uchaguzi huo

umati unasaidia sana kwa wale wafuata upepo
 
ITV wanajitahidi kutupa coverage ambayo haiko biased kihivyo.. Mie toka kampeni zimeanza ninaangalia kampeni kupitia ITV na wanajitahidi kutoa coverage nzuri kwa CDM.. Maneno yenye utata toka kwa mawaziri (kama jana toka kwa Waziri Nagu) tunaona ITV.. So please wana JF tukumbuke huwezi kupata kila unachotaka ww..
Sosoliso, asante kwa kuliona hili. Watu hatuna shukrani kabisa!.

Mwandishi wa ITV kwenye kampeni ya Arumeru kwa upande CCM ni Novatus Makunga, huyu ni kada wa CCM na uchaguzi wa mwaka 2000 aliomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Arusha kupitia CCM. Anayeandaa ripoti ndiye anayechakachua na sio ITV newsroom. q
Mwandishi wa ITV kwa upande wa Chadema ni Ufoo Saro, yeye ndie aliyeripoti kampeni ya Dr. Slaa yuko very fair kwa Chadema. Hakuna TV yoyote nyingine inayo wa cover Chadema vizuri ya ITV!.

Niliwahi kutoa ushauri wana jf tuwe watu wa shukrani japo kwa madogo tuu. Tupunguze kulalamika kila wakati. Coverage nzuri zote za Chadema kwenye ITV huzioni wala kuzitolea pongezi, bali +ve covarage ya CCM ndicho pekee watu wanalalamikia!.

ITV inastahili pongezi kwa +ve coverage Arumeru Mashariki
 
Tatizo kubwa la ITV ni kuwapa CCM coverage kubwa na kuitanguliza habari ya Sioyi kabla ya ile ya Nassari kila taarifa yao ya habari
 
Inaruhusiwa katika tasnia ya habari kutoa picha zilizohifadhiwa na wala hakuna tatizo.
nafikili ni uelewa wako mdogo ndo umekufanya ukurupuke kuja kuandika post hii!

yes inarusiwa,lakini kama ni file photos pia wanahabarisha kwa maandishi.sio kimya kimya mkuu.
 
Acha wachakachue mkuu usipate shida.Ila nawasifu kwamba wanaonyesha uhalisia wa CDM ambayo itatusaidia sana kujua mwenendo wa chama.
 
me nashangaa watun kazi kulalama lalama tu utadhani umati unaoonekana kwenye Tv ndo kura zenyewe,we ukioneshwa umati mkubwa inakusaidia nn wakati uko tanga,mbeya,mara na uchaguzi uko arumeru? waarumeru hawaitaji kuangalia tv kupiga kura coz wao ndo wanaohudhuria mikutani hyo,taarifa ya habari unaoneshwa wewe uliye mbali na arumeru ambayo huna effect yoyote katika uchaguzi huo

naona akiliyako ime stak
 
chadema.jpg
ccm oyiiiiii
 
Ujinga mwingine wana record wakati kamera imeshushwa usawa watumbo hivyo huwezi kujua kama kulikuwa na umati then za CCM wanapanda juu yamiti!pumbaffa kabisa hawa!!
 
Itv kama mnaona hamwezi kutuletea habari ya ukwela na bora hiyo habari muiache.

picha za kampeni ya ccm mlizo tuonyesha leo si halisi kabisa mmetuchanganyia na piçha za zinduzi.

uongo wa kwanza:leo arusha ilikuwa na baridi,mawingu kiasi na umande kwa mbali,lakini nyie mmetuonesha kukavu na vumbi.picha iliyokuwa tofauti kabisa na ya chadema iliyo onyesha kijani kibichi.

uongo wapili: mmetonyesha sioi akihutubia umati mkubwa wa watu kwenye uwanja wa mpira na bila aibu mkatuchanganyia na picha halisi iliyo onyesha hali halisi ya arusha ilivyo leo,ukweli ni kuwa leo sioi alikua na watu wachache sana mithili ya mtu anayehutubia mkutano wa ukoo,mtu alie angalia TBC habari atakubaliana na mimi.

au kuna arumeru nyingine mliyo endaaa
nawapa ushauri wa bure.
MKIWA WAONGO MUWE NA KUMBUKUMBU.
kinachomata mwisho wa siku ni kura utakazo pata na sio idadi ya watu wanaokuja mikutanoni, IGUNGA,BUSANDA kote huko umati ulikuwa mwingi lakini mwisho wa siku watu wanaipa KURA CCM! so endeleeni kuesabu wingi watu mikutanoni, siasa is more than what u think my friend.....SHINE UR EYES!!!
 
hapa labda ndugu yangu ufuatili kila siku zinaonyeshwa itv wanarusha story balance kwa chadema na ccm,kitu mnacholalamikia itv mbona hakipo kwani jamaa wanafanya mikutano zaidi ya kumi kwa siku kwa timu tofauti kabisa na chadema ambao wanfanya mkutano mmoja ama miwili hivyo kama mwandishi wa habari mzuri hautategemea mkutano mmoja pekee na hicho ndicho wanajf kinachotusumbua mfano ukiwa makiba na mbuguni jana kulikuwa kukavu,arusha mjini mvua

wacha porojo wewe inamaana na sioi wanakua wawili kwa wakati mmja?
 
unajua ninyi msoelewa demokrasia mnamatatizo sana! kujaza watu sio tatizo. wengine ni wacheda, CFU na vyama vingine wanaokuja kutafta weekness za ccm. na wengine ni wa ccm ambao katika mikutano hii mnayotukana watu badala ya kuwaambia mtawapatia maendeleo gani wenyewe wanagundua kua hamfai na kuhama ccm.
ninyi subirini trehe 1 tumpeleke nassari bungeni mlie.
 
Sosoliso, asante kwa kuliona hili. Watu hatuna shukrani kabisa!.

Mwandishi wa ITV kwenye kampeni ya Arumeru kwa upande CCM ni Novatus Makunga, huyu ni kada wa CCM na uchaguzi wa mwaka 2000 aliomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Arusha kupitia CCM. Anayeandaa ripoti ndiye anayechakachua na sio ITV newsroom. q
Mwandishi wa ITV kwa upande wa Chadema ni Ufoo Saro, yeye ndie aliyeripoti kampeni ya Dr. Slaa yuko very fair kwa Chadema. Hakuna TV yoyote nyingine inayo wa cover Chadema vizuri ya ITV!.

Niliwahi kutoa ushauri wana jf tuwe watu wa shukrani japo kwa madogo tuu. Tupunguze kulalamika kila wakati. Coverage nzuri zote za Chadema kwenye ITV huzioni wala kuzitolea pongezi, bali +ve covarage ya CCM ndicho pekee watu wanalalamikia!.

ITV inastahili pongezi kwa +ve coverage Arumeru Mashariki

kuweka rekodi vizuri ni kwamba novatus makunga hajawahi kugombea ubunge ccm arusha mwaka 2000
 
nimeiangalia na kusikiliza vizuri amesema makada wa sisi wameendelea na mikutano ya kampeni katika kata mbalimbali hakuna neno leo lililotakwa ndugu yangu hiyo ya kuchanganya picha mimi siyo mtaalamu na wala siingilia na wala siyo interest yangu mimi naangalia hoja zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya wana arumeru mashariki hata zikiwekwa picha za uzinduzi igunga ama manzese siyo kitu cha msingi

mbona unakuwa mgumu kuelewa nimeeleza ccm inafanya kampeni na timu zaidi ya kumi kwa maana timu moja yupo sioi na mwigulu,timu nyingine lusinde,timu inayofuata ni wassira,timu nyingine esther bulaya,timu nyingine martini shigela,timu nyingine mary nagu hivyo si ajabu mwandishi mzuri akatafuta mikutanoi mikubwa tofauti mitatu hata kwa kuwa na wapiga picha tofauti na jioni akachanganya mikutano yote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom