Elections 2010 ITV mmeanza lini kuwa CCM?

Nimekuwa nikishangaa sana baadhi ya watu kumuona Mengi ni mzalendo na mpiganiaji wa maslahi ya nchi. Big bloody mistake!
Mengi ni opportunist tu, anaangalia upepo unaelekea wapi naye anafuata.
Halafu anapenda umaarufu na kupendwa. This time nimefurahi kuwa watu wameona Mengi's true colours.
So make your own judgment (a.k.a changanya na za kwako!!).
 
Tanzania ya leo haimati ni TV gani inaonyesha balanced news. watanzania wameshaona ukweli. Serikali inawajali hasa kipindi cha uchaguzi. Mara utaona Rais anakaa kwenye vumbi eti anaongea na Handcapped. Lakini tunasahau kuwa handcapped mmoja alitiwa ndani alipokwenda ikulu aonane na Rais ili amweleze shida yake. Hawakuweza hata kumpa msaidizi wa Rais ili aongee naye, alisweka ndani hadi wanaharakati walipomtoa na baadaye kituo kimoja cha TV kilitoa offer ya kumpa nauli arudi kwao Arusha.
Kwenye kampeni tunamuona JK kaa kwenye vumbi for photo opt, lakini aliyemfuata Ikulu hakuweza kuonana hata na secretary, akaishia lupango.
Mwaka huu ngoma mdundo, watatumia TV, magazeti ya serikali na binafsi but ukweli utabaki palepale. Watanzania wamechoka na wanataka MABADILIKO....Period.
 
walishanunuliwa kitambo saana yaani mpaka watoto wanaosoma mashaili wanaonyeswa na siyo sela za mgombea, na channel kichefuchefu zaidi ni CHANEL 10 au imenunuliwa na Rostam nini!??

Mkuu kwa miaka mitano ya awamu ya nne rais alikuwa Rostam Aziz, JK ni boya tuuuuuuuuuuuuuuuuu.RA ndiye anaamua nani awe nani, nini kifanyike
 
Ndugu zangu, Great thinkers,
Juma lililopita nimekuwa nafuatilia kwa karibu taarifa za habari. Kwa miaka sasa huwa naangalia ITV kwa sababu wamekuwa wanabalance habari zao bila kupendelea chama chochote. Ingawaje huwa Mzee mengi anapewa muda zaidi katika habari lakini hilo kwangu si hoja kwa sababu yeye anasaidia jamii na si mwanasiasa wa chama chochote.

Katika juma lililopita habari za ITV zimeanza kusifia CCM karibu kila siku. jana Jumapili nimeona habari zote ni kuhusu CCM na kidogo CUF. Je Mmenunuliwa ka bei gani?

Si muda mrefu tutaacha hata kufuatilia taarifa za habari maana zitakuwa ni zile zile tulizozizoea za TBC. Sasa hivi kinachopendeza TBC ni Mdahalo tu. Halafu pamoja na mdahalo mzuri mliotangaza wiki iliyopita, mengi mazuri yalisemwa kuhusu maendeleo ya nchi hii, Mbona hamjachukua sehemu ya ule mdaharo kutengeneza habari? Au kwa upande wenu hakukuwa na habari pale? Tujuzeni mapema tusielekee kusiko.

Mengi ana kadi ya CCM aliyopewa pale CCM Kisutu miaka ya 1970s/ 1980s na aliionesha wakati Sophia Simba aliposema yeye si CCM.
 
Back
Top Bottom