Elections 2010 ITV mmeanza lini kuwa CCM?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Ndugu zangu, Great thinkers,
Juma lililopita nimekuwa nafuatilia kwa karibu taarifa za habari. Kwa miaka sasa huwa naangalia ITV kwa sababu wamekuwa wanabalance habari zao bila kupendelea chama chochote. Ingawaje huwa Mzee mengi anapewa muda zaidi katika habari lakini hilo kwangu si hoja kwa sababu yeye anasaidia jamii na si mwanasiasa wa chama chochote.

Katika juma lililopita habari za ITV zimeanza kusifia CCM karibu kila siku. jana Jumapili nimeona habari zote ni kuhusu CCM na kidogo CUF. Je Mmenunuliwa ka bei gani?

Si muda mrefu tutaacha hata kufuatilia taarifa za habari maana zitakuwa ni zile zile tulizozizoea za TBC. Sasa hivi kinachopendeza TBC ni Mdahalo tu. Halafu pamoja na mdahalo mzuri mliotangaza wiki iliyopita, mengi mazuri yalisemwa kuhusu maendeleo ya nchi hii, Mbona hamjachukua sehemu ya ule mdaharo kutengeneza habari? Au kwa upande wenu hakukuwa na habari pale? Tujuzeni mapema tusielekee kusiko.
 
Ebanaeee!!!!!!!! Hii nchi imejaa majoga sijapata kuona ni kwamba hawa watu siyo kwamba wamenunuliwa yawezekana wanaogopa kuzushiwa la kuzushiwa, nani anapenda aitwe mkwepa kodi? Au nani anapenda kushtakiwa kwa kuiba mke wa mtu? Hata ningekuwa mimi ningefanya hivyo ili niwe safe lakini kakura kangu maana ntakapigia gizani kataelekea kwa chadema
 
Tusiwaonee ITV jamani, kwa mazingira yaliyopo wamejitahidi sana, yapo mapungufu ya kibinadamu, nao lazima watetee kitumbua chao, mtumikie kafiri upate mradi wako, nawapongeza sana, nadhani tupeleke tuhuma zaidi kwa chombo chetu wenyewe TBC kabla hatujaangalia cha jirani maana huo si wajibu wake, tuendelee kuisusia TBC hadi inyooke japo kuna wakati nikiibia wananifurahisha kidogo...
 
Ndugu zangu, Great thinkers,
Juma lililopita nimekuwa nafuatilia kwa karibu taarifa za habari. Kwa miaka sasa huwa naangalia ITV kwa sababu wamekuwa wanabalance habari zao bila kupendelea chama chochote. Ingawaje huwa Mzee mengi anapewa muda zaidi katika habari lakini hilo kwangu si hoja kwa sababu yeye anasaidia jamii na si mwanasiasa wa chama chochote.

Katika juma lililopita habari za ITV zimeanza kusifia CCM karibu kila siku. jana Jumapili nimeona habari zote ni kuhusu CCM na kidogo CUF. Je Mmenunuliwa ka bei gani?

Si muda mrefu tutaacha hata kufuatilia taarifa za habari maana zitakuwa ni zile zile tulizozizoea za TBC. Sasa hivi kinachopendeza TBC ni Mdahalo tu. Halafu pamoja na mdahalo mzuri mliotangaza wiki iliyopita, mengi mazuri yalisemwa kuhusu maendeleo ya nchi hii, Mbona hamjachukua sehemu ya ule mdaharo kutengeneza habari? Au kwa upande wenu hakukuwa na habari pale? Tujuzeni mapema tusielekee kusiko.

Kwakweli hata mimi nimewashitukia tayari, yaani wamebadilika kweli kweli.
 
Kwa siku za nyuma, Taarifa za ITV zilikuwa zinaweka wagombea wengi angalau JK, Dr. Slaa, CUF na wengine. Lakini sasa ni CCM tu. wako radhi kutangaza hata wagombea wa ubunge lakini siyo Dr. Slaa. Mwaka huu CCM watakiona cha moto hata TV zisipotangaza. Kura tutapiga.
 
Haya mambo sometimes yananichanganya!!! Mimi jamani taarifa za habari nisipowahi ya Mlimani TV basi tena maana nikiangalia hizi channels nyingine napata kichefuchefu... Kampeni ni za kijani tu... Mengine usipotafuta magazeti ndo basi tena, labda na sisi wachache kwenye mitandao.

I hate this!
 
Hao ITV ni walewale tu. wanamlinda mteja wao wa matangazo wakimpoteza nani atamudu gharama zao?
 
Ni kweli yaelekea ITV imebadilika na imeanza kuipendelea CCM na mgombea wake. Wameacha ku-balance kabisa.
Inawezekana mmiliki wake ametishiwa na kuambiwa amfagilie Bw Kikwete mgombea wa CCM.

Sasa TV stations zote zitakuwa zinaboa kwa habari za kisiasa, kwani TBC ya serikali ndiyo kabisa, Star TV nayo hovyo, sasa ITV nayo imekuwa hovyo. Vituo vyote hivyo vimekuwa kama maafisa habari wa Kikwete au watu wa propaganda wa CCM.
Si wavae tu mavazi ya 'Kikwete Press 2010' ili mambo yawe official?

Inatakiwa wamiliki wa gazeti la Mwananchi waanzishe TV station yao, warushe mambo hewani. Hapo ndio mafisadi watakoma.

Hata wafanyeje, waTz wameelewa sasa.
Hawamtaki msanii. Wanamtaka MPIGANAJI DR. SLAA.

Tumpigie kura Dr. Slaa.
SLAA NI RAIS 2010!
 
Style hii inasaidia wengi sana akiwemo mzee mengi.......kwani inasemekana halipi kodi
ebanaeee!!!!!!!! Hii nchi imejaa majoga sijapata kuona ni kwamba hawa watu siyo kwamba wamenunuliwa yawezekana wanaogopa kuzushiwa la kuzushiwa, nani anapenda aitwe mkwepa kodi? Au nani anapenda kushtakiwa kwa kuiba mke wa mtu? Hata ningekuwa mimi ningefanya hivyo ili niwe safe lakini kakura kangu maana ntakapigia gizani kataelekea kwa chadema
 
Haya mambo sometimes yananichanganya!!! Mimi jamani taarifa za habari nisipowahi ya Mlimani TV basi tena maana nikiangalia hizi channels nyingine napata kichefuchefu... Kampeni ni za kijani tu... Mengine usipotafuta magazeti ndo basi tena, labda na sisi wachache kwenye mitandao.

I hate this!
thanks SUWI; na mimi nitahamia Mlimani TV maana huko kwingine ni upuuzi mtupu. yote wanayotuahidi ccm ni marudio maana tuliishaahidiwa bila kutekelezewa. A change is a must
 
duh,mimi nilishaacha kuangalia TV za kibongo. Angalau mitandao inakuwa na habari zote. Magazeti naangalia vichwa vya habari.
 
Kwa taarifa yako, wanaweza kutangaza kuwa kikwete alikuwa Tarime na maneno aliyokuwa akiongea, lakini wakaweka picha za jangwani. so msitishike, ccm itaanguka kama vile wana wa islaeli walivo peta huku majeshi ya kivita vya Farao yakizama Baharini.
 
Haya mambo sometimes yananichanganya!!! Mimi jamani taarifa za habari nisipowahi ya Mlimani TV basi tena maana nikiangalia hizi channels nyingine napata kichefuchefu... Kampeni ni za kijani tu... Mengine usipotafuta magazeti ndo basi tena, labda na sisi wachache kwenye mitandao.

I hate this!
thanks SUWI; na mimi nitahamia Mlimani TV maana huko kwingine ni upuuzi mtupu. yote wanayotuahidi ccm ni marudio maana tuliishaahidiwa bila kutekelezewa. A change is a must

Mie nafikiri si upuuzi, ila unaugonjwa, na ugonjwa wenyewe ni kuwa unayotaka kuyasikia mwenye binafsi hayasikiki. Na ukienda ndani zaidi unaweza gundua weye ni mbinafsi ama dikteta. Samahani mkubwa kama nimekukwaza.
 
walishanunuliwa kitambo saana yaani mpaka watoto wanaosoma mashaili wanaonyeswa na siyo sela za mgombea, na channel kichefuchefu zaidi ni CHANEL 10 au imenunuliwa na Rostam nini!??
 
ITV Miaka ya nyumba ilikuwa inatoa miafaka ya vyama vya upinzani sawa na CCM lakini naona Mengi anazidi kushindwa kimaendelea kushinda Kupata Mikataba minono nchini as a private interprenuer

Tunahitaji a Private TV Station isiyona Utamu wa Utaajiri wa Tanzania --- Wow It cannot happen...
"Leadership does not always wear the harness of compromise"
 
Back
Top Bottom