ITV acheni mara moja kusambaza uongo na kueneza sumu hii kupitia Mwalimu Nyerere

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Wakuu tangu jana nimeona ITV wameanzisha kipindi kizuri tu, ambacho nafikiri watakuwa wanaonesha vipande vya hotuba tamu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Lakini kuna kosa kubwa la kimantiki na kiufundi katika utangulizi unaosomwa na Deo Rweyunga kabla kipande hichi cha hotuba maarufu ya "Nyufa" haijaenda hewani.

Rweyunga anasema Mwalimu alisema nini juu ya UTAWALA BORA!!!!!! Hakuna kitu kama hicho katika kinywa cha Mwalimu Nyerere, nimemsikiliza na kumsoma sana mara kadhaa, hakuna mahali Baba wa Taifa alikuwa anatumia neno UTAWALA BORA. Mara zote alisisitiza UONGOZI BORA. Kuna maana kubwa sana katika utofauti wa maneno hayo. UTAWALA vs UONGOZI. Halafu the first one ni moja ya maneno yanayotokana na DONORS IMPOSITION, ambayo kwa kweli yameshatuathiri sana nasi tunayaimba kwa nguvu zetu zote. Kama tunavyoimba sawa na walivyokuwa wakiimba MAKABURU; RULE OF LAW, bila kuhoji ARE THOSE LAWS FAIR...ABLE TO MAKE JUSTICE PREVAIL AND GIVES HOPES TO WANANCHI, AS THE TWO (JUSTICE and HOPES) are the cornerstone for peace and stability in where.

Naweka nukuu ya Mwalimu Nyerere juu ya UONGOZI BORA na si utawala bora. Nukuu inatoka Azimio la Arusha juu ya mambo muhimu kwa sisi kuendelea, WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA , ingawa pia neno hilo amelirudia mara nyingi sana katika maneno yake. Ni vyema Watanzania tuimbe na kusisitiza uongozi bora si kinyume chake;

"(d) Uongozi Bora:

TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo lililopo
ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi na kwa
hiyo Ofisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze utaratibu maalum kuhusu
mafundisho ya Viongozi tangu wa Taifa zima hadi Mabalozi ili
waielewe siasa yetu na mipango ya uchumi. Viongozi ni lazima wawe
mfano mzuri kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia."

Tunaweza kujadili. Si vyema kueneza uongo huo na sumu ya watu kutambua utawala bora bora badala ya uongozi bora.
 
Kwani wewe hujui kuwa awamu ya JK wamebadilisha neno from UONGOZI BORA kwenda UTAWALA BORA?? haya yote ni kwa sababu ya ufisadi na huyu Rweyunga ndo moja wapo ya watangazaji makanjanja wasiokuwa na msimamo
 
Ni makosa tu ya kibinadamu ungetoa maoni yako yakasikika wangerekebisha.
 
Kwani wewe hujui kuwa awamu ya JK wamebadilisha neno from UONGOZI BORA kwenda UTAWALA BORA?? haya yote ni kwa sababu ya ufisadi na huyu Rweyunga ndo moja wapo ya watangazaji makanjanja wasiokuwa na msimamo

Tangu enzi ya Mkapa bwana.Hata Wilson Masilingi alikuwa waziri wa utawala bora wa mkapa.
 
Neno utawala kwa nyerere linamfaa sana kwani ndivyo alivyoTawala serikali yako. Action speak louder than words. mark my words. Tumjaji kwa matendo yake kuliko mambo ya kufikirika.
 
Naweka nukuu ya Mwalimu Nyerere juu ya UONGOZI BORA na si utawala bora. Nukuu inatoka Azimio la Arusha juu ya mambo muhimu kwa sisi kuendelea, WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA , ingawa pia neno hilo amelirudia mara nyingi sana katika maneno yake. Ni vyema Watanzania tuimbe na kusisitiza uongozi bora si kinyume chake;

"(d) Uongozi Bora:

TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo lililopo
ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi na kwa
hiyo Ofisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze utaratibu maalum kuhusu
mafundisho ya Viongozi tangu wa Taifa zima hadi Mabalozi ili
waielewe siasa yetu na mipango ya uchumi. Viongozi ni lazima wawe
mfano mzuri kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia."

Tunaweza kujadili. Si vyema kueneza uongo huo na sumu ya watu kutambua utawala bora bora badala ya uongozi bora.

Nyani hajioni kundule, umedai Rweyunga amepotosha hotuba ya Nyerere kuhusu nyufa, kwa kusema
UTAWALA badala UONGOZI bora. Badala kutuwekea hiyo inception ya hotuba ya Nyerere umeokota
nukuu nyingine kabisa kutoka Azimio la Arusha ambayo haihusiani na hotuba husika. Why compares
apples and oranges. Weka nukuu ya hiyo hotuba, sio na wewe kuzidikutupotosha zaidi dude.
 
Kwani wewe hujui kuwa awamu ya JK wamebadilisha neno from UONGOZI BORA kwenda UTAWALA BORA?? haya yote ni kwa sababu ya ufisadi na huyu Rweyunga ndo moja wapo ya watangazaji makanjanja wasiokuwa na msimamo

Correction: Si JK, ni tangu enzi za mkapa. Nadhani Mkapa ndo alianzisha matumizi ya neno hilo la UTAWALA Bora, JK kalichukua jinsi lilivyo na kulitumia kwa kasi. Sasa tuna watawala na si viongozi.
 
Wameshatuzoesha wenyewe bana! Tazama hapa ,kidumu cha cha mapinduzi na wafuasi wao huitikia kidumu chama tawala!
 
Back
Top Bottom