Kiongozi pongezi sana kwa kutimiza miaka 11 ya ndoa na my wife wako.
Wakati mwingine tukikutana na watu mlio na uzoefu wa kiwango hicho inakuwa ni chachu kwetu.
Mimi ndo nakamata miaka mitatu sasa, naomba Mungu aniwezeshe na kunijaalia ili siku moja nifikie hapo ulipo, nadhani siku hiyo nitakukumbuka Realman.
Kwa kweli niwatakie maisha marefu zaidi ya yenye furaha zaidi.
Naomba leo umwagie maji mengi zaidi kwa niaba ya JF!!
Nafikiri wengi wakifikia miaka hiyo wanaleta mazoea kwemye ndoa wanaanza kupunguza care flaniflani hivi na mwanamke anakuwa bize sana na malezi ya watoto kuliko mumewe majukumu pia nayo yanaongezeka pia, sasa hapo usipoangalia vizuri mwanaume anaanza kuwa na company ya marafiki mbalimbali ambao wana tabia tofautitofauti hapo ndipo inapoanza kasheshe.
Hongera zenu RMn na wifi..mimi ndio naingia tenth month, ndoa si rahisi bwana yataka moyo! Ulikofika tuombe mungu nasi tufike. Kiss wifi kwa hisani ya warembo wote JF.
....hongera sana Realman na mkeo miaka 11 si haba kwenye ndoa. Kama usemavyo ndoa tamu bana mkielewana.....nikija kufikia hiyo miaka 11 ya ndoa my little boy atakuwa big boy. Uwiii!! Naona mbali kweli kweli maana ndio kwanza nina 1 year na mwezi hivi.
Jamani RealMan natumaini sijakosea leo ni aniversari yako.
Hongera sana kama nimepatia!
Tujuze siku ya leo iko vipi kwako na kwa mupenzi wako, siku ya leo umesherekea vipi?
Wana JF nimeona nisikae kimya bila kuwajuza wema wa Mungu kwangu.
Najua wengine mtakuwa mmevaa kijani/njano kusherekea "chama chetu cha mapinduziiii chajenga nchi" (itikia ni wimbo) huku wengine (pengine) mmevaa nguo nyeusi kuashiria maombolezo kitaifa.
Leo ninatimiza miaka 11 toka nimekula kiapo cha kuishi (kama mume na mke) na huyu mdada.
Tulikutana 1994 na ndoa ikafungwa miaka 6 baadae
Ndani ya miaka hii 11 Mungu kanijalia kuwa baba wa boy-10 na girl-7 na ukiwaangalia ni dhahiri hakunichakachua labda awe amechakachua na mdogo wangu, hahaahahaaa!!!
Ni miaka ya kuishi na mwanamke ambaye alichukua nafasi ya mama na dada yangu katika maisha.
Miaka 11 imenifundisha nisimwamini kila mtu ninaposigana na mke wangu. Nakumbuka in our early years niliwahi kushare na mchungaji juu ya tofauti zangu na mke wangu only for the pastor to use my story in his preaching the next sunday. Siku hizi nayasovu mwenyewe tu, no outsiders!
Miaka 11 ya kutambua kwamba vitu vidogo sana (thanks, sorry, karibu, darling..) vinajenga uhusiano na vitu vidogo pia huwasha moto.
Jamani wakati mwenzenu nashereheka 11 years kuna experience zipi (nzuri/mbaya/vituko) umewahi pitia kwenye mahusiano yako.
Karibuni tuzungumze!!!!!!!!!!!!!!!!
Nipo njiani mkuu...lol..changamoto kwa senior bachelors hii... wapi The Finest!!!!