It's either you're honest,...or

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Napenda kujua historia ya mtu katika relations kabla ya ku-stick nae.
Lakini hii niliyo pewa ime nivunja moyo na sidhani kama hua namaanisha
pale ninaposema napenda ukweli,...the truth hurts,....now i believe.

Eti,...
nimekua na two boyfriends before wewe,...na what is worse katika
mda wote huo,nilitoa "viumbe" tumboni mara 3.......bla bla bla

Napenda ukweli,lakini huu siwezi kuubeba,....je najisaliti mwenyewe au niko sahihi?
 
Mhhhh huo ukweli unauma na kuuvumilia ni ngumu sana
Kuna kuwa honest ila hapo ni too much mkuu kuubeba
 
huyo ndio waukweli sasa...kakwambia ukweli akijua kuwa yeye yayari kashaweka matatani uwezo wake wakuzaa hivyo wewe umepewa hint kwamba bwana mie hapa kama unategemea mtoto ujuwe kuwa wacheza bajati na sibu. sasa huoni kuwa kafanya jema hapo?? je angeficha hilo alafu baadae baada ya kuhangaika kupata mtoto bila mafanikio ugundue kula alikuwa anatoaga mimba sii unhgemlaumu.
 
Sijaona cha ajabu hapo zaidi ya masikitiko tu!! Mpaka umefikia hatua ya kumuweka kikaangoni na kumjaji, basi ujue mapenzi kwake yameshaisha hivyo ni bora ukamuacha kwa amani tu!! Lakini fikiria na wewe umetoka na girls wangapi kabla yake? Na katika issues zako zote ingekuwa we ndo mbeba mimba, ungeshatoa ngapi? Msipende kujudge ni bora atleast ukajua mustakabari mzima ulompelekea yeye kufanya aloyafanya then unaamua!!
 
Mhhhh huo ukweli unauma na kuuvumilia ni ngumu sana
Kuna kuwa honest ila hapo ni too much mkuu kuubeba

Mpenzi na ww unaniangusha sasa,yaani mm nikikwambia ukweli kuwa nina watoto sita na nilishawahi kufumaniwa utaniacha??!!!
:focus: kijana usiwe unaulizwa maswali kama huna uwezo wa kuhimili majibu yake. Umeambiwa ukweli unaanza kujiuliza maswali mara mbili mbili je angekudanganya??? Naona ulipenda kusikia wewe ndio wa kwanza na hajawahi kupenda......wanaume mnapendaga sana kusikia uongo na ndio maana huwa mnadanganywa sana.
 
Mie nasema kila siku, Trust katika Mapenzi sio lazima iwe 100% kama kweli wampenda Mpenzi wako.... Ndo haya sasa!!
 
Mie nasema kila siku, Trust katika Mapenzi sio lazima iwe 100% kama kweli wampenda Mpenzi wako.... Ndo haya sasa!!

Sijui kwa nini hili suala mi nalitazama kwa namna tofauti. Hivi huu ukweli pekee watosha kuonyesha kuwa huyo dada hamfai msela? Ni kweli inastua na inaweza kupunguza imani, but IMO.......there is something that must be proved beyond the reasonable doubt!
 
Dunia ya leo msichana wa form 2 ana bf tayari hapo akipata mimba opt ndio hiyo mara nyingi hii inasikitisha na mara nyingi maadili ndio kichocheo,kwanza huyo tunayemuongela ana umri gani? na hizo habari za mauaji wakati anaripot usoni alikuwaje?je alionyesha masikitiko kidogo/sana anajutia hayo matendo au la na je ikitokea tena sasa hivi ana ujasiri wa kurudia? Binadamu yeyote asiye na hofu ya Mungu anaona hicho si kitu na i think yeye jamii yake inayomzunguka yeye ndio katoa chache so far i can tell that..otherwise wengi wanafanya hivi vitu na wanaficha so kuoa huyu sio garantii ya kukosa kukuzalia watoto mradi awe anajutia makosa hayo na kutubu mbele za Mungu
 
Aiseee...
Ina maana huyo dada hakujifunza baada ya mara ya kwanza wala ya pili??

Newayz kama unampenda unaweza pishia mbali hilo la kuchoropoa muendelee. Ila sasa ndo uwe tayari kulea akipata mimba yako usikute unamhukumu kumbe na wewe ndio wale wale wanaolipia kwenda kutoa.
 
Ukimchunguza sana bata hutamla! kuna mambo mengine ni magumu sana kuyasamehe unapoambiwa ukweli na mwenza wako. Sa nyingine huwa nafikiria na pia huwa napenda wawe wakweli lakini, ni muhimu kuwa na kiasi na busara kwenye mazungumzo!
 
Siku zote ukweli. Mimi huwa sipendi kujua historia ya mwanamke ninaye mpenda. Najua itaniumiza.
 
Back
Top Bottom