It is true that there is life even after THIS.................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,172
Ni kweli kubakwa ni udhalilishwaji kijinsia na tuendelee kuutupia madongo
lakini ni ukweli pia kila inapowezekana mwathirika mtarajiwa pambana kujinusuru na suluba hiyo...................................

Ukweli unaniongoza kuamini ya kuwa mwathirika mtarajiwa akiona amewekwa kwenye kibanio cha sawasaawia ni vyema akakubali yaishe kwani hakuna mapana yasiyo na ncha.....................................

Na ni ukweli uliokithiri ya kuwa kunusuru uhai wa mwathirika upewe kipaumbele kulikoni kujikita katika kunusuru kero ya kubakwa............

Kwani ni ukweli usiopingika ya kuwa maisha endelevu pia yapo na tena yenye furaha baada ya kunyanyasika.........................fikiria uhai na uutetee kadiri inavyowezekana.............

ila usinisurubu kwa kudhani ninapigia tarumbeta wabakaji....la hasha.......................ninawakemea kwa nguvu zote..............
 
Ubakaji wa sasa hivi kwetu hapa mwingi unasababishwa na waganga na vita hizi ndogondogo, maybe tuanzie huko kwa waganga kwa kuwaelimisha watu wasiamini sana hay maushirikina ili tujikwamue na hii kadhia
 
Genuinely speaking Rutashubanyuma.... nimesoma ndio najua inahusu
kubaka but naomba unidadafulie before i comment for sijakupata exactly what it is unasema...
 
Mwafrika kwa ushirikina sijui kama kuna mahali tutafanikiwa kumwondoa..........................tnaabudu nguvu za giza kupita kiasi ninamfahamu afisa mmoja wa ngazi za juu sana serikalini ambaye ilibidi akunamishwe na mganga wa kienyeji ili apate cheo.........................yaani alibakwa huku akijiona.............lol
 
Genuinely speaking Rutashubanyuma.... nimesoma ndio najua inahusu
kubaka but naomba unidadafulie before i comment for sijakupata exactly what it is unasema...

hii nimeipata kwenye makala moja ya majuu nimeona nisibandike kwa sababu wengi wetu hatupendi makala ndefu kwa hiyo nikaona nitoe ufupisho wake.................................inahusu mdada mmoja ambaye pamoja aliwekwa kwenye kibanio na mbakaji alipambana hadi mhujumu mazingira yule akamkata koo kabla ya kumbaka..........................kwa hiyo walichoshauri wataalamu wa hayo masuala ni kuwa ni bora angalinusuru maisha yake kwa kuvumilia hiyo dhambi iliyotendwa juu yake badala ya kusalimisha uhai wake na bado maiti yake ikabakwa pia.............................

sasa swali langu ni je hiyo ni sahihi kuwa kuna uhai hata baada ya kubakwa???????????
 
Mwafrika kwa ushirikina sijui kama kuna mahali tutafanikiwa kumwondoa..........................tnaabudu nguvu za giza kupita kiasi ninamfahamu afisa mmoja wa ngazi za juu sana serikalini ambaye ilibidi akunamishwe na mganga wa kienyeji ili apate cheo.........................yaani alibakwa huku akijiona.............lol
Mmemsikia Prof. Maji Marefu, Mbunge wa Korogwe, juzi bungeni? Amekiri hadharni kuwa mafanikio yake kupata ubunge yalitokana na ushirikiano wa kitaaluma na waganga wenzake. Pia akawabeza wabunge wanaowadharau waganga mchana lakini ni wateja wao wakubwa wakati wa kutafuata vyeo. Niliona wengi wao kwenye Mjengo wakitoa tabasamu za kijuha (silly smiles) kwa vile alikuwa amewaanika.
 
Mwafrika kwa ushirikina sijui kama kuna mahali tutafanikiwa kumwondoa..........................tnaabudu nguvu za giza kupita kiasi ninamfahamu afisa mmoja wa ngazi za juu sana serikalini ambaye ilibidi akunamishwe na mganga wa kienyeji ili apate cheo.........................yaani alibakwa huku akijiona.............lol

Duuh!! Huko nako ni kubakwa kweli? Yaani unakwenda kwa mganga kisha unamweleza matatizo yako ya kutaka kupanda cheo kwa gharama yoyote; anakupa treatment plan inayokutaka uingiliwenaye kingono. Unakubali kimsingi na treatment plan inayohusisha kuingiliwa kingono kisha unaingiliwa. Halafu ukishamaliza kuingiliwa unamlipa pesa kwa tiba zake kisha unadai kuwa umebakwa? SIDANGANYIKI.
 
hii nimeipata kwenye makala moja ya majuu nimeona nisibandike kwa sababu wengi wetu hatupendi makala ndefu kwa hiyo nikaona nitoe ufupisho wake.................................inahusu mdada mmoja ambaye pamoja aliwekwa kwenye kibanio na mbakaji alipambana hadi mhujumu mazingira yule akamkata koo kabla ya kumbaka..........................kwa hiyo walichoshauri wataalamu wa hayo masuala ni kuwa ni bora angalinusuru maisha yake kwa kuvumilia hiyo dhambi iliyotendwa juu yake badala ya kusalimisha uhai wake na bado maiti yake ikabakwa pia.............................

sasa swali langu ni je hiyo ni sahihi kuwa kuna uhai hata baada ya kubakwa???????????

Yes kuna uhai, I was a victim of that when l was 7 by my nephew by that time alikuwa nafikiri form one or two. I survived, and l dont hate all men, though l still hate my nephew!
 
mtu akitaka kunibaka,asidhanie atapata easy ride...i will fight,nikifa yote sawa kwanza hakuna anayejua life after death inawezekana huko maisha ni mazuri sana ukifa,
ruta huyo dada aliyechinjwa koo unajuaje kama asingefight asingechinjwa koo???wabakaji wengine simply ni wauaji mie nimeangalia CSI mara nyingine hawa wabakaji hawawezi kufunction mpaka mtu awe amekufa hii inampa sense of control mbakaji so,sio kweli kama asingefight angebaki kuwa hai...simply she was in a wrong place at the wrong time...
 
Jestina,
what a coincidence kati ya thread na avatar yako
Gabrielle Union ni mhanga wa kubakwa na bado alipiga moyo konde na ni bonge la muigizaji.she's my fav......
 
Ruta una uhakika gani kwamba nia ya mbakaji haikua kulala na maiti?!Kuna watu akili zao ni tofauti sana na zetu!!Wengine hiyo starehe yao kwahiyo binti angeweza akatulia na bado akatolewa uhai!!

Binafsi ikitokea mtu anataka kunibaka sitomfaidisha kwa kumwacha anipate kirahisi...ntahakikisha kila mmoja anatoka pale na maumivu au yeye tu ndo
anatoka na maumivu!!
 
Jestina,
what a coincidence kati ya thread na avatar yako
Gabrielle Union ni mhanga wa kubakwa na bado alipiga moyo konde na ni bonge la muigizaji.she's my fav......

thanks,kuna mtu ameniuliza hii avatar nikawa simjui jina mie niliibua tu hii avatar mtandaoni...ngoja nimgoogle.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom