Issango Kuuwawa na diwani wa CCM

Mlitika

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
457
260
Amepandishwa mahakama ya mwanzo kujibu tuhuma za kutishia kumuua aliyechuana na Mh. M. Dewji (CCM) katika kukisaka kiti cha ubumge wa Singida Mjini, kamanda Josephat Issango. Ilielezwa mahakamani hapo kuwa diwani huyo wa kata ya Unyamikumbi (CCM) mjini Singida alimtumia ujumbe wa simu ya mkononi (SMS) mlalamikaji kuwa atamkata kichwa na kummeza. Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana ya sh. 300,000

Hata hivyo chanzo cha habari hakikueleza sababu za diwa kuahidi kuchukua hatua hiyo kali dhidi ya maisha na uhai wa Isango.

Issango ameonekana siku zote akiwanyima usingizi viongozi na wafuasi wa CCM mjini Singida kwa hoja zake majukwaani na katika makala mbalimbali kwenye magazeti.

Habari hii imeandikwa pia kwe Nipashe ya tarehe 30/5/2012
 
Asiogope hawatawezq.

Kama wauaji wa Mwenyekiti wa CDM kata ya Usa-River wamedakwa, hata hao watazuilika
 
Back
Top Bottom