Israel yakosolewa vikali kwa kuwafukuza Wapalestina

Mandago

JF-Expert Member
Feb 8, 2008
238
99
Israel yakosolewa vikali kwa kuwafukuza Wapalestina

0,,2319585_1,00.jpg


Hillary Clinton
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Hillary Clinton
Marekani yaiongoza jumuiya ya kimataifa kuikosoa Israel


Marekani na Umoja wa Ulaya zimeikosoa vikali Israel kwa kuzifukuza familia za Wapalestina kutoka eneo la Jesusalem Mashariki zikionya kuwa hatua za aina hiyo zinahatarisha mchakato wa kusaka amani ya Mashariki ya Kati. Umoja wa Ulaya pia umesema ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi katika eneo hilo unakiuka sheria za kimataifa.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton ameiongoza jumuiyaya kimataifa kulaani kufukuzwa kwa familia za Wapalestina kutoka Jerusalem Mashariki akiileza hatua hiyo kuwa kitendo cha kujutia na cha ochokozi. Bi Clinton pia ameishutumu Israel kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ya kimataifa kwa mujibu wa mikataba ya amani iliyotiwa saini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Washington Marekani akiwa ameandamana na waziri wa kigeni wa Jordan, Nasser Judeh, bi Clinton ameelzea masikito yake makubwa kusuhu kufukuzwa Wapalestina kutoka Jerusalem Mashariki.

"Vitendo hivi ni vya kujutia sana. Nimeshawahi kusema kuwa kuzifukuza familia na uvunjaji wa makaazi huko Jerusalem Mashariki si njia ya Israel kutimiza majukumu yake. Nimeitaka serikali ya Israel na maafisa wa baraza la mji wa Jerusalem wajiepushe na vitendo vya uchokozi."

Polisi wa kupambana na ghasia wa Israel waliokuwa na virungu walizitimua familia mbili za Wapalestina kutoka nyumbani kwao katika eneo linalokaliwa la Jerusalem Mashariki Jumapili iliyopita, hatua iliyozusha machafuko katika kitongoji cha Sheikh Jarrah, kinachokaliwa na Waarabu. Sheikh Jarra ndicho kitongoji tete kabisa kilichoko karibu na mpaka unaolezwa kuwa wa kijani kati ya mashariki na magharibi mwa Jerusalem.

Hatua hiyo ilifuatia uamuzi wa mahakama kuu ya Israel kuamuru Wapalestina 53 wafukuzwe kutoka eneo hilo wakiwemo watoto 19.

Sweden, inayoshikilia urais wa Umoja wa Ulaya imeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu kufukuzwa kwa Wapalestina kutoka eneo la Jerusalem Mashariki kunakoendelea, ikisema hakukubaliki na ni kinyume cha sheria za kimataifa. Taarifa ya Umoja wa Ulaya iliyotolewa mjini Brussels Ubelgiji imesema kufukuzwa kwa Wapalestina kutoka Jerusalem Mashariki kunaenda kinyume na miito iliyotolewa na jumuiya ya kimataifa kuepukana na vitendo vya uchokozi katika eneo hilo. Taarifa hiyo aidha imesema kufukuzwa kwa Wapalestina kutoka Jerusalem Mashariki kunathibitisha mkondo wa kutia wasiwasi unaofuja kuundwa kwa mazingira yanayofaa kuendeleza juhudi za kutafuta suluhisho la mzozo kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa Ulaya pia binafsi zimeikosoa Israel kwa kuwafukuza Wapalestina kutoka eneo la Jerusalem Mashariki. Msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Ufaransa, Romain Nadal, amesema kwa mujibu wa sheria ya kimataifa, hatua ya Israel sio halali na kuongeza kuwa kuwafukuza Wapalestina kunahatarisha mchakato wa kusaka amani.

Naye waziri wa mambo ya kigeni wa Norway, Jonas Gahr Stoere, amesema hatua ya Israel inahatarisha mchakato mzima wa kutafuta amani ya Mashariki ya Kati. Jumuiya ya kimataifa mara kwa mara imehimiza Israel iepukane na vitendo vya uchokozi dhidi ya Wapalestina kwa kuwa hatua hiyo inavuruga uwezekano wa kufikiwa makubaliano kuhusu mji wa Jerusalem kwa msingi wa suluhisho la mataifa mawili.

Israel ililiteka eneo hilo katika vita vyake vya mwaka 1967 vilivyodumu siku sita na baadaye kuligawa katika hatua ambayo jumuiya ya kimataifa haijaitambua. Wapaletina wanataka eneo la Jerusalem Mashariki liwe mji mkuu wa taifa lao huru litakaloundwa ambalo linayajumulisha maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza. Hatma ya mji wa Jerusalem ni mojawapo ya maswala nyeti katika mzozo baina ya Israel na Wapalestina.

Mwandishi.Josephat Charo

Mhariri:Aboubakary Liongo
 
Hapa ndipo ulipo unafiki. Mauaji ya Rwanda hakuna mtu aliyeyalaani, ukiachilia mapigano mbalimbali yaliyowahi kutokea Afrika!
 
Wapalestina wana haki ya kusaidiwa, inchi zote zimepata uhuru duniani lakini inchi ya pekee iliyo baki bado imetawaliwa ni palestina tu, palestina ni nchi ya pekee bado imetawaliwa kwa mabavu mpaka hivi leo.

Israel inabidi ikosolewe
 
Last edited:
Hapa ndipo ulipo unafiki. Mauaji ya Rwanda hakuna mtu aliyeyalaani, ukiachilia mapigano mbalimbali yaliyowahi kutokea Afrika!

Wazungu wanafanya kitu kwa faida zao wenyewe tu, hawajali mtu mwingine, zote hizi ni propoganda zao tu, sidhani kama itafanyika kitu.
 
Hawa Wapalestina itabidi wajiulize kwa nini hawana uhuru, wamepoteza nafasi nyingi za kupata amani kutoka kwa Waisraeli. Wanaamini kwamba njia ya dialogue pekee haitoshi. Rejea kila kunapokuwa na mazungumzo ya amani na Israeli, Hamas huwa wanafanya nini wakati huo, hasa pale wanapofikia kukubaliana. Hamas Policy: "There is No language the Israelis will ever understand except Gunfire!" Wanapenda kuichokoza Israeli makusudi kwa kurusha makombora on a daily basis halafu Israeli waki-retaliate basi lawama zote wanamwagiwa Israeli. Kwa nini wasifuate nyayo za Misri na Jordan (nchi pekee za Kiarabu zilizotiliana mkataba wa amani na Israeli) ambao waliona kwamba vita sio njia nzuri ya kufikia makubaliano na Israeli na wakafanya amani?
 
Hawa Wapalestina itabidi wajiulize kwa nini hawana uhuru, wamepoteza nafasi nyingi za kupata amani kutoka kwa Waisraeli. Wanaamini kwamba njia ya dialogue pekee haitoshi. Rejea kila kunapokuwa na mazungumzo ya amani na Israeli, Hamas huwa wanafanya nini wakati huo, hasa pale wanapofikia kukubaliana. Hamas Policy: "There is No language the Israelis will ever understand except Gunfire!" Wanapenda kuichokoza Israeli makusudi kwa kurusha makombora on a daily basis halafu Israeli waki-retaliate basi lawama zote wanamwagiwa Israeli. Kwa nini wasifuate nyayo za Misri na Jordan (nchi pekee za Kiarabu zilizotiliana mkataba wa amani na Israeli) ambao waliona kwamba vita sio njia nzuri ya kufikia makubaliano na Israeli na wakafanya amani?

Ndugu Buchanan, Waisraeli hawataki mapatano, vipi watataka mapatano na wao wanataka kuendelea kuitawala inchi ya watu, kama kweli wanataka mapatano wangeipa uhuru Palestina zamani, ndugu Buchanan napenda kukujulisha pia, waisraeli ndio wanao vitawala viomba vya habari muhimu (in the world) kwa hiyo propoganda unazo zisikia katika vyombo vya habari kuhusu Israeli ni uongo mtupu, Wasraeli ndio walio itawala Palestina, ukitazama ramani ya dunia kabla ya 1947 Israeli haipo katika ramani hiyo.
 
Last edited:
Back
Top Bottom