Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,389
- 31,335
Nonda, nimesoma hicho kijarida. Nimekisoma na kufanya fikra kama mimi na kile nikijuacho. Hii ni tofauti na wewe uliyesoma na kumeza kila kitu.Ndugu Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni bomu.
Ni mazingaombwe yasiyo na majibu ya mkato( kiini macho)
Kauli zenu zitaungwa mkono na wasomaji wengi, pia kupandisha mizuka wengi lakini bado hatuzungumzii mazingaombwe ya Muungano. Mimi nafikiri huwa tanafanya kwa makusudi ili kutengeneza chuki au kuamsha jazba kwa wanaofata mkumbo tu.
Hiki kijarida ,gonga link http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27 kinajaribu kuelezea utata na ugumu wa Muungano wa baadhi ya mambo kama ulivyo Muungano wa TZ na mahusiano ya kimataifa. Ni vyema kukisoma chote lakini kwa muktadha wa mliyoyaandika anzia uk 94 kwenda mbele.
Na baada ya kukisoma bado tutakuwa na ujasiri wa kuamsha mizuka ya wanajf?
Ukisoma kwa umakini utadhani ni watu wameandika, nenda uk 94 utaona ni maoni binafsi ya mtu yanayoweza kuegemea upande anaoutaka.
Utashangaa kusikia Wzbar wanalalmikia adha za muungano, ni mwiko kwao kuongelea faida za muungano ambazo ni nyingi sana na hivyo ndivyo mwandishi wa Kijarida alivyozivia akili za Wenzetu. Majuzi wakati wa kauli ya kibaguzi ya mwarabu Jusa, tulianza kampeni dhidi ya Wzbar waishio bara na inaendelea kuhusu ajira, ardhi n.k. Kelele zimekwisha zikionyesha umuhimu wa muungano kwao.
Kilichokuwa kinawatia kiburi ni tetesi za mafuta, sasa yapo Uganda na Kenya. Kiburi kwisha
Zbar ifanye ifanyavyo bado bara ni sehemu muhimu sana ya uchumi wake. Siyo Israel wala Oman. Ukweli huu unauma na hakuna mzbar anayeweza kuuongelea. Bara wakiweka kauzibe Zbar itaumia sana.
Hili linakuja ni suala la muda tu.
Maswali ni haya:
Nyerere amepeleka ukristo Zbar, sasa Waisrael ambao ni wajomba wa damu wa Yesu wataleta nini?
Katika mambo 11 Zbar inayodai ni ya muungano, mambo ya nje ni mojawapo. Seif Idd amefanya hivyo?