Israel Kusaidia Zanzibar Jinsi ya Kupambana na Maafa na Majanga.

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Israel Kusaidia Zanzibar Jinsi ya Kupambana na Maafa na Majanga.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti, Uchunguzi na Usimamizi wa Majanga Nchini Israel Bwana Gideon Kader kwenye Hoteli ya David Ciladel Mjini Jerusalem. Kushoo mwa Balozi Seif ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifahamishwa hatua za mfumo unaochukuliwa wa kukabiliana na Maafa katika Miji ya Israel unaotumia Mtandao wa Kisasa. Nyuma ya Balozi ni

Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd wakipokea maelezo kuhusu utaratibu wa kakabiliana na majanga.

Akionyeshwa na akifahamishwa hatua za mfumo unaochukuliwa wa kukabiliana na Maafa na majanga katika Miji ya Israel unaotumia Mtandao na mitambo ya Kisasa.



Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd ukipeana afya na kupongezana na wenyeji wao wa Israel walioongozwa na Waziri Mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Raia Nchini Israel Luteni Kanal Tai Peleg.


Taasisi hio ya Utafiti, Uchunguzi na Usimamizi wa Majanga Nchini Israel inaangalia uwezekano wa namna ya kuisaidia Zanzibar katika harakati zake za kupambana na Maafa wakati yanapotokezea Maafa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bwana Gedion Kandel wakati wa mazungumao yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yupo Nchini humo kwa ziara ya Kiserikali mazungumzo yaliyofanyika hapo katika Hoteli ya David Citadel Mjini Jerusalem.

Bwana Gedio alisema Taasisi yake tayari imeyapokea maombi ya Zanzibar na kukubali kushirikiana pamoja wakati yanapotokezea matatizo ya Majanga na hatimaye kupelekea Maafa , Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya Utafiti wa Majanga aliishauri Zanzibar kuandaa Mpango Maalum wa maeneo ambayo Taasisi yake inaweza kusaidia.

Alisisitiza kwamba vitengo vya Maafa hufanikiwa vyema katika utekelezaji wa majuku yake endapo Bajeti ya Vitengo hivyo inakuwa ya kuridhisha.

Balozi Seif alisema Majanga yanayopelekea kutokea kwa Maafa yanaweza kupungua kutokana na uwajibikaji mkubwa wa watendaji hao unaoambatana na Taaluma ya kina. Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake alitembelea Taasisi ya Usalama wa Raia inayojishughulisha na Maajanga Home Front Command { HFC } Mjini Telaviv.

Mkuu wa Taasisi hiyo Luteni Kanal Tai Peleg aliueleza Ujumbe wa Zanzinbar kwamba Taasisi hiyo imeundwa kufuatia Janga la Maafa yaliyokuwa ayakiikumba Nchi hiyo likiwemo lile la Mashambulizi ya Kivita.

Alisema Taasisi hiyo tayari imejijengea umaarufu mkubwa kutokana na watendaji wake kushiriki katika kutoa msaada wa Kiufundi kwenye Matukio ya Maafa mbali mbali Duniani.

Ameishauri Tanzania na Zanzibar kwa Ujumla kutumia fursa ya mafunzo yatakayotolewa na Taasisi hiyo katika Semina itakayofanyika mnamo mwezi wa Septemba mwaka huu wa 2012.

BONYEZA VIDIO UONE MACHAFUKO YA ZANZIBAR MKONO WA KISIASA /AU UAMSHO http://www.youtube.com/watch?v=MnT8bTMN4oU
 
Back
Top Bottom