Mkuu.Nitajibu ya Shossi na mdondoaji kwa pamoja.
Mimi sina sababu ya kutetea Christians, ninachotaka ni kusaidia watu kuelewa kuwa kila jambo lazima liwe na evidence, tusiende kwa hisia tu. Okello alijitanganza Field Marshal, swali ni kuwa alipewa na nani huo u-field marshal. Sasa kwasababu kaandika katika kitabu chake basi ndio tumeze bila kufikiri hata kidogo!
Okello alikuwa mkereketwa wa dini ya Kikristo tangu anatoka uganda hadi anarudi. Maneno anyosema kuwa ametumwa kuwaokoa wala siyakatai, na kuwa aliua Waarabu wala sikatati kwasababu baada ya mapinduzi hakukuwa na dini ilikuwa ni panga kichwani, na ilifanywa na wanamapinduzi wote si Okello peke yake. Sasa kama aliua waarabu hiyo siyo evidence kuwa ametumwa na kanisa. Kama ni hivyo provide substantial evidence. Kumbuka Waarabu hao ndio walipeleka waafrika utumwani, sasa tuseme walitumwa na waislamu au uislam.
Kuhusu share BoT please provide evidence zilikuwa na thamani gani ili tuweze kupata mahali pa kuanzia mjadala. Lakini kumbuka kuwa tulikuwa na EA common currency hadi mwaka 1966, na baada ya hapo tukawa na monetary collaboration kwasababu ya EAC, lakini kila nchi ilikuwa na Central bank yake (Angalia lini BoT ilianzishwa).
Zanzibar haijawahi kuwa independent member wa EA FYI.
Hata kama share zipo bado kuna mambo mengi sana BOT imeyfanya makubwa kuliko hizo share. Znz wakati wa komandoo ilifikia mahali ina collapse, mishahara yote BoT, na hivi tunavojadiliana Znz wanapata umeme buree miaka nenda rudi, wanalipiwa na kodi za wabara, huu ni ukweli si masimango. Mwaka jana kifaa kilipoharibika ilichukua miezi 3 na 5 miliion US$ kutoka BoT baada ya SMZ Kukwama, Muulize Shamsi vua Naohadha. Sasa sijui hizo share ni kiasi gani na zenye thamani gani. anyway tujadiliane
Mimi nimekutana na habari hii:- sijui kama itawasaidia ?
2. Suala la Bodi ya Sarafu na Namna Zanzibar Ilivyochomwa Kisu Mgongoni na Tanganyika
Turudi kwenye historia kidogo kuona namna ambavyo Tanganyika imeutumia Muungano kuinafiki Zanzibar kwa hadaa na ghilba. Wazungu huita hali hii knife on the back. Nyaraka zilizopatikana kutoka Crown Agency London, Uingereza, zinaibua siri nzito ambayo inafunua namna Tanganyika ilivyotumiliwa na kujikubalisha kutumikia matakwa ya mkoloni, Muingereza, ili kuinyima Zanzibar nguvu za kiuchumi kwa makusudi. Ni suala la Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (EACB).
Kwa mujibu wa nyaraka hizo, wakati wa ukoloni zile nchi zilizojulikana kama East African Territories Kenya, Uganda, Tanganyika, Zanzibar, Somalia na Aden zilikusanywa pamoja katika Bodi ya EACB. Baada ya kupatikana kwa uhuru, Aden na Somalia ziliamua kujiondoa kwenye Bodi hiyo, lakini nyingine ziliendelea. Zanzibar haikuwa inajuwa kuwa kumbe wakati huo, tayari Tanganyika ilishatakiwa na mkoloni wake, Uingereza, kuhakikisha kwamba uwezo wa Zanzibar kifedha na kiuchumi unaporomoshwa kwa kadiri ilivyowezekana ikianza na kuuondoa uwakilishi wake kwenye Bodi hiyo.
Mwaka 1964, kulikuwa kuwe na mkutano wa Bodi hiyo. J.B. Loynes, ambaye alikuwa na dhamana katika Wizara ya Makoloni ya Uingereza alimuandikia H. R. Hirst, ambaye alikuwa katibu wa Bodi kwamba: isipokuwa kama kuna kauli madhubuti kutoka Dar es Salaam inayothibitisha kuhudhuria kwa Zanzibar (na tusiwe sisi tunaozua suala hilo), haitokuwa sawa kwa Bodi kumualika mwakilishi kutoka Zanzibar kwa sasa. Kusema kweli, italeta fadhaa kuona wale wenye nia ya kujitenga huko Visiwani wanapewa kichwa.
Hata hivyo, Hirst alikuwa amefahamishwa na Jacob Namfua, aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha wa Tanganyika, kuwa suala la kuiondoa Zanzibar kwenye Bodi hiyo lilikuwa ni kinyume na Mkataba wa Muungano, maana mpaka wakati huo suala la sarafu halikuwa la Muungano. Barua ya Namfua kwa Hirst ya Juni 9, 1964, inaeleza: Nimeagizwa kutamka kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Muda inayoongoza Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, katika vikao vya siku za mbele vya Bodi, utaendelea kwa utaratibu ule ule kama ilivyokuwa kabla ya Muungano. Makubaliano ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar hayahamishi moja kwa moja mambo ya sarafu kuingia katika Serikali ya Muungano na mpaka yatakapofanywa mabadiliko kama itakavyokubaliwa, uanachama wa Bodi ya Sarafu unabaki kama ulivyo.
Lakini inaonekana kuwa Uingereza ilikwishaamua kwamba iwe iwevyo, Zanzibar haikutakiwa kabisa kuwemo kwenye Bodi hiyo. Kwa hivyo, Loynes akamuandikia tena Hirst Septemba 8, 1964 akimwambia: Tunaweka wazi kwamba hatuitaki Zanzibar katika kikao chetu kinachofuata na natumai lazima kutakuwa na njia zinazoweza kuwaweka nje. Lile ambalo ningependa kufanya kwa sasa ni kukumbusha juu ya suala hili, ili kuhakikisha kwamba hakuna makabrasha yanayovuka bahari hadi tutapokuwa na uhakika wa msimamo wetu.
Kufika hapo, Tanganyika kwa kuwa ilikuwa yenyewe tangu mwanzo haina dhamira njema na khatima ya Zanzibar kiuchumi na, kwa kuwa, ilikuwa tayari kutumikia hata maslaha ya wale ambao Mwalimu Julius Nyerere alikuwa huku nje akiwaita mabeberu, ikapiga magoti kutimiza matashi yake na matakwa ya Muingereza.
Mgao wa ziada wa fedha za Bodi ulifanywa Oktoba 1964 na fungu la Zanzibar hapo, na kuanzia hapo, lilikwenda katika kasha la Tanganyika katika Crown Agency (rejea barua ya W.H. Tweed ya Oktoba 1, 1964).
Ghilba hii ilihalalishwa kwa Toleo la Sheria, Mswada Na. 43, la Juni 18, 1965, ambapo ilielezwa: Mambo yafuatayo sasa yanatengwa kwa Bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na yanatangazwa kuwa Mambo ya Muungano: mambo yanayohusiana na sarafu na mzunguko wake na shughuli za benki, fedha za kigeni na udhibiti wa viwango vya kubadilishana fedha, na kifungu kidogo (1) cha kifungu 68 cha Katiba ya Muda hivi sasa kinarekebishwa kwa kuongeza mambo yaliyotajwa kama jambo jipya (xii) katika tafsiri ya Mambo ya Muungano.
Kwa hakika huu, kama alivyokuwa akiuita Marehemu Ali Nabwa, ulikuwa ni ujambazi wa hali ya juu dhidi ya Zanzibar! Ulikuwa uonevu wa dhahiri uliofanywa na Nyerere, Amir Jamal (aliyekuwa Waziri wa Fedha) na Edwin Mtei (aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo) kwa kuchochewa, kuongozwa na kudhibitiwa na watawala, wakoloni Waingereza.
Ni wazi kuwa, kwa Tanganyika kutimiza matakwa ya Uingereza, kulikuwa ni kujidhalilisha yenyewe mbele ya mkoloni huyo, na ndiyo maana hata katika nyaraka hizo nilizozitaja unaiona dharau ambayo Waingereza waliionesha kwa viongozi hao wa Tanganyika. Kwa mfano, Loynes alimtaja mara moja Mtei kama kitakataka tu (Nabwa, 2003).
Lakini japokuwa hii ilikuwa ni aibu kwa upande wa Tanganyika, ilikuwa ni aibu iliyowasaidia kuzivunja nguvu za Zanzibar kiuchumi na imekuwa ndiyo hasara kwa upande wa Zanzibar, kwani baada ya hapo zilifuatia rasimu kwa rasimu za barua iliyokuwa inatakikana kuhalalisha kutolewa kwa Zanzibar nje ya Bodi, huku Loynes akisisitiza kwamba lugha iwe makini kiasi kwamba wao (wapanga njama hizi) wasiweze kutambulika, maana wote walijuwa kuwa wanayoyafanya yalikuwa kinyume na sheria.
Yaliofuata hapo ni historia ya mzozo mmoja mkubwa katika Muungano unaohusisha nafasi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na nani anamdai mwenzake baina ya Zanzibar na Tanganyika katika Muungano huu.
3. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kabari za Tanganyika kwa Zanzibar
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilianzishwa kutokana na Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 1965 ili kuchukua jukumu la kifedha lililokuwa likisimamiwa na EACB iliyokuwa na Makao yake Makuu Nairobi, Kenya.
Lakini kuanzishwa kwa BoT hakukuja hivi hivi tu, bali kwenyewe kulikuwa ni matokeo ya dhuluma iliyofanyiwa Zanzibar kwenye EACB kama ilivyooneshwa hapo juu. Ili kufanikiwa kuitupa Zanzibar nje ya Bodi hiyo, Tanganyika iliingiza haraka haraka shughuli za matumizi ya sarafu na utawala wa mabenki katika Muungano.
Kwa kutumia Katiba ya Muda ya Muungano (1965), Sheria Na 43 ya 1965 (1965 Act. No. 43 of 1965), Serikali ya Tanganyika ilipeleka Bungeni marekebisho ya kifungu Na. 85 cha Katiba hiyo na kuongeza kifungu kidogo Na. XII cha Orodha ya Makubaliano ya Muungano kinachohusu masuala ya fedha, mabenki, sarafu, fedha za kigeni na udhibiti wa fedha za kigeni kuwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano kama inavyosemeka.
Gazeti la Serikali ya Muungano la tarehe 18 Juni 1965 ndilo lililotangaza kufanyika marekebisho hayo ambayo ni kinyume kabisa na Makubaliano ya Muungano ya 1964. Baada ya kufanyika marekebisho hayo, Edwin Mtei aliandika barua rasmi kwa Katibu wa EACB na kumueleza kwamba kuanzia Disemba 29, 1965 kwamba kuanzia hapo ni yeye Mtei ndiye angeliiwakilisha Tanzania katika Bodi hiyo. Kwa hakika, hili lilikuwa ndilo jambo lililokuwa likitakiwa na Waingereza.
Baada ya kukamilika kufanyika marekebisho haya ya Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano, Waziri wa Fedha wa wakati ule wa Tanganyika, Amir Jamal, alimuandikia barua Mwenyekiti wa EACB na kumuagiza rasmi kwamba haki zote na amana zote za Zanzibar zilizokuwemo katika Bodi hiyo, zipelekwe katika Benki Kuu chini ya Serikali ya Muungano na kwamba kuanzia pale ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania pekee ndiye tu atakayeiwakilisha Tanzania katika Bodi hiyo. Haya yalifanyika baada ya kulazimisha kuingizwa kifungu Na. XII katika Orodha ya Mambo ya Muungano ambacho hakikuwemo kabisa katika Makuabaliano ya Muungano ya 1964 (Duni, 2008).
Uchambuzi huu unaiita hii kuwa ni kabari ya kijambazi ya Tanganyika kwa uchumi za Zanzibar. Kuyatia masuala ya fedha katika Orodha ya Mambo ya Muungano ulikuwa ubabe wa makusudi maana ni jambo ambalo, kisheria, lisingeweza kufanyika bila ya idhini ya Zanzibar na pia wizara ya fedha ya Muungano haikuwa na haijawahi kuwa ya Muungano hadi leo. Kama kulikuwa na kitu cha Muungano hadi wakati huo kwenye masuala ya fedha, ilikuwa ni usimamizi wa taratibu na utoaji wa sarafu na udhibiti wa mwenendo wa kubadilisha thamani ya shilingi tu.
Serikali ya Muungano haikuwa imepewa idhini ya kusimamia fedha za Zanzibar na kile ilichokifanya kwa kuzitwaa fedha za Zanzibar hakiwezi kupewa jina jengine la kiungwana zaidi ya wizi uliofanywa kwa jina la Dola. Maana kilichofuatia baada ya hapo ni kuwa, fedha hizo ziliingizwa kuanzisha mtaji wa BoT, ambayo leo hii Zanzibar inaambiwa haina chake.
Ukweli ni kuwa BoT ina mchango wa Serikali ya Zanzibar ambao ulitokana na mgawo wake ilioupata baada ya kuvunjika kwa EACB. Kumbukumbu zinaonesha kwamba wakati wa kuanzisha kwa BoT, Bodi ya EACB ilikuwa imeshapeleka paundi za Kiingereza 82, 840 kama ni mchango wa Zanzibar katika uanzishwaji wa Benki hiyo.
Duni (2008) anaeleza vyema hisabu halisi ya mtaji wa BoT na mchango wa Zanzibar katika mtaji huo, kwamba benki hiyo ilianzishwa kwa mtaji wa paundi milioni moja (1,000,000) za Kiingereza ambayo ilikuwa ni sawa na milioni 20 za Afrika Mashariki kwa wakati huo, ambapo Serikali ya Tanganyika ilitoa paundi 668,884, ya Zanzibar ikatoa hizo 82,840 na kasoro ya kujalizia ili kufikia pauni 1,000,000 yaani paundi 248,276 ikajazwa na Serikali ya Muungano, ambayo Zanzibar ni sehemu yake.
Hisabu ya mtaji wa BoT inaelezeka hivi:
Mchangiaji Kiwango cha Mchango (kwa Paundi)
Tanganyika 668,884
Zanzibar 82,840
Jumla Ndogo (Tanganyika na Zanzibar) 751,724
Serikali ya Muungano 248,276
Jumla Kuu 1,000,000
Katika hili la BoT, hoja ya Zanzibar sio tu kwamba Zanzibar ina amana yake katika uanzishwaji wa benki hiyo ambayo, hata hivyo, kwa miaka yote hii Serikali ya Muungano hawataki kuitambua, lakini zaidi ni kuwa sheria iliyoianzisha benki hiyo ilikuwa na misingi ya kibeberu, ambapo iliipa Serikali ya Muungano nguvu zote za kumiliki na kusimamia fedha huku ukiipopotoa kabisa Zanzibar. Kwamba pamoja na mchango wake wa asilimia 11.02 katika mtaji ulioanzisha BoT, Serikali ya Zanzibar haikutajwa kabisa kwenye sheria hiyo.
Badala yake sheria hiyo, kwa makusudi, inaiteremsha hadhi Serikali ya Zanzibar kwa kuilinganisha kuwa sawa na Serikali ya Mkoa. Hii maana yake ni kuwa, kama ambavyo serikali za mikoa haziwezi kukopeshwa, ndivyo ilivyo pia kwa serikali ya Zanzibar. Leo hii, ikiwa Serikali ya Zanzibar inataka kukopa BoT, inalazimika kufanya hivyo kwa kupitia Serikali ya Muungano tu, na si vyenginevyo. Lakini kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano na Katiba zote mbili ambazo zilipaswa kuutafsiri Mkataba huo, Serikali ya Zanzibar ndiyo yenye jukumu la kusimamia uchumi wa Zanzibar. Ni vipi Serikali inaweza kusimamia uchumi ikiwa haina mamlaka kwenye fedha na njia za kuzipata fedha hizo?
Kuinyima Serikali ambayo ina jukumu la kusimamia uchumi wa watu wake nguvu za kukopa na kufanya mikataba inayohusiana na fedha na taasisi nyengine ni unyongaji wa makusudi, na kwa bahati mbaya Zanzibar imejikuta katika kitanzi hicho.
Nimeiopoa hapa,
Siasa za Muungano na hatima ya uchumi wa Zanzibar « Zanzibar Daima