Isingekuwa ni muungano, hali ya kiuchumi na kisiasa zanzibar ingekuwaje?

Mie nilimsikia waziri mmoja akisema wanatenga eneo la bandari huru ila nahisi ni siasa tu!!!

Kama wenyewe watajiamulia kama walivyo jiamulia kumaliza matatizo yao ya kisiasa basi wataweza ila wakisubiri waamuliwe Dodoma hiyo wasahau........
 
Mdonoaji mimi si mzanzibari ila nafuatilia sana historia sio tu ya Zanzibar hata ya nchi inazoizunguka Tanzania hayo yote ni ya kweli unayosema kikubwa nikuwa Karume "baba" alikuwa seamen alitembea nchi nyingi na kujionea walivyopiga hatua wewe fikiria pale michenzani nyumba ziliyengwa miaka ya sitini yule mzee alijenga barabara nne mbili kila sehemu wakati ule sidhani kama kulikuwa na haja ya kufanya vile ila hakuangalia wakati ule alijua wazanzibar wataongezeka na mji utapanuka. Leo hii hapa mjini mfano barabara ya uhuru kutokea clocktowe mpaka pale inapoanza buguruni ni barabara ya njia moja kila upande! sisi nadhali tuliangalia mahitaji ya wakati ule tu hatukujua kama Dsm itakuwa.

Viongozi wetu MashaAllah kila siku wanasafiri wanaona mambo mengi ya kuweza kuja kuya introduce huku kwetu ila wakishapanda ndege huwa wanayaacha airport za wenzetu.! Hatuna mipango hatujui hata mahitaji yetu! Betri yangu ya laptop ipo low as umeme hakuna tangu asubuhi hehehehe.....:wink2:

Mkuu,

Mie sio mzanzibari kaka mie mtanganyika tena nimechanganya vibaya sana maana hata sijui kabila langu maana nimezaliwa na baba mtanganyika, mama mtanganyika, ila babu zao ni kasheshe inaanza kuna mjerumani, myemen, muethiopia, mmasai, mcommoro, mhindi sasa mwishoe nimekaa nikajiuliza mie kabila langu nani nikaishia kujiita mtanganyika maana asili ngumu sana labda ndio tuite mswahili kama Professa George wa Nairobi alivyosema asiyekuwa kuwa kabila maalum wanaitwa waswahili.

Ila wazanzibar nawasupport kwani kuna kipindi nilikaa huko muda mrefu nikifanya kazi na kwakweli kilichonivutia ni ile great misconception tuliyokuwa tukifundishwa darasani kwamba zanzibar kilikuwa kituo kikuu cha biashara ya utumwa. Nikiwauliza wazawa wa kule wakawa wananibishia ndipo nikaamua kuisoma historia yao na kwakweli nimekubaliana nao kuwa haikuwa hivyo. Zanzibar ilikuwa ni kitivo cha biashara, mahusiano, na utumwa. Utumwa haikuwa kwamba wazanzibar wanawatumia hapana walikuwa wanatumika kama ilivyo Dar sasa kuwa jiji la biashara (Kama unakumbuka Transatlantic slave trade zanzibar ilikuwa kituo muhimu sana) sasa walikuwa wakija kufunga mikataba, biashara nk. Vilevile zanzibar walikuwa na biashara zengine mfano walijenga bandari mombasa, Kilwa na Dar-es-Salaam (hata jina walilianzisha wao) . In short nimekuja kugundua do not believe what you have been taught darasani kwani vyengine ni uongo mtupu na mind games kusahaulisha watu wasijue walikotokea.
 
Kama wenyewe watajiamulia kama walivyo jiamulia kumaliza matatizo yao ya kisiasa basi wataweza ila wakisubiri waamuliwe Dodoma hiyo wasahau........

Ni kweli unayoyasema ndio nikabakia kuyachukulia maneno kama ya kisiasa tu... Anyway time will tell
 
tusubiri EAC na sie tunyongwe kiuchumi maana Kenya wameshaingiza benki yao KCB na ina matawi saba kwa hapa Dar pekee arusha na mwanza nadhani pia wana branchi zao. Hawa jamaa wameingia mpaka jinja uganda na mwaka juzi wamefungua branch southen sudan. Sisi tena juzi juzi benki ambayo haina muda mrefu kwenye biashara za kibenki EXIM ndio iliweza kufungua branch comoro tukiingia kwenye hiyo EAC tutashuhudia Equity Bank na nyinginezo zikifungua matawi mpaka mpanda!..................
 
Mdondoaji,

..Karume aliwahi kunukuliwa akisema "azimio la arusha mwisho chumbe". Zanzibar haikuwahi kuwa nchi ya kijamaa kama tunavyoujua huku Tanganyika.

..wakati mnasubiri kurudishiwa pwani ya Afrika mashariki, na kuanza kuchimba mafuta, kuna mambo ambayo mnapaswa kuyarekebisha ndani ya Zanzibar ya sasa ili msonge mbele.

..kuwa na eneo kubwa na rasilimali nyingi haimaanishi kwamba moja kwa moja mtapata maendeleo. we have all those things in Tanganyika lakini hatuna maendeleo kwasababu ya uongozi na mipango mibovu.

..narejea hoja yangu kwamba Zanzibar ilianza kudhoofika kidogo kidogo toka enzi za Sultani. kile kitendo cha kunyanganywa maeneo iliyokuwa "ikimiliki" ni ushahidi tosha kwamba Zanzibar ilikuwa dola dhaifu/inayodhoofika kulinganisha na dola zilizokuwepo wakati huo.

..we can discuss jinsi gani zao la karafuu limedorora hapo Zanzibar. inawezekana kabisa price controls ikawa moja ya sababu. hilo huwezi kusingizia muungano. karume alitaifisha ardhi kabla hata hatujaungana. inawezekana pia utaifishaji ardhi uliliweka zao hilo ktk mikono ya watu wasio na ujuzi na mitaji ya kilimo chake. we saw what happened in Tanganyika when sisal production was nationalised. hii inaweza kuwa thread inayojitegemea na si vizuri kutumbukiza siasa humo.

Mohamed Shossi,

..ni kweli Karume alikuwa na nia ya kuibadilisha Zanzibar ifanane na nchi zilizoendelea.

..tatizo lake ni kwamba alianza kuwekeza ktk miradi ambayo haikuwa sustainable.

..Karume alipaswa kuwekeza ktk sekta kama za viwanda, utalii, kuimarisha kilimo etc etc. badala yake akajikita kwenye sekta zinazotumia fedha kama kujenga nyumba za wazee, kuanzisha TV kama huduma na siyo biashara, etc etc.

..sasa utaona kwamba Karume alikuwa mtumiaji mzuri wa fedha badala ya kuwa mzalishaji mzuri.

..Zanzibar ni nchi ya kwanza kuwa na TV ya rangi, hilo halina ubishi. but what happened after that, ni muhimu zaidi. ungetegemea Zanzibar ndiyo wawe wanaongoza basi kwa utaalamu wa sekta ya habari ya TV ktk eneo hili la Afrika lakini sivyo.

..mwingine anajisifia Zanzibar ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na matawi ya mabenki ya Ulaya. this is another wrong notion. hizo benki zilikuwepo hapo kuinyonya Zanzibar na siyo kitu kingine. vijana wa leo tunapaswa kujiuliza what happened to Benki ya Watu wa Zanzibar. nini kimefanyika kuhakikisha benki hiyo inajitanua maeneo mbalimbali ya Zanzibar,Tanganyika,and beyond?
 
Tatizo la Tanzania mkuu,

Siasa nyingi na ubinafsi wa viongozi wetu. Tunaingia katika EAC wakati sheria za ardhi bado hazijatekelezeka vema, uchumi haujasimama vema, umeme tatizo na tuna unemployment that is sky rocketing. Wakija wakenya wanachukua ardhi kwani wanaa strong currency hivyo kwao inakuwa rahisi kununua ardhi, kazi ndio kama ulivyosema makampuni yao kibao yapo hapa hivyo ukikuyu na ukalenjin kibao watu wetu watabakia wakitangatanga tu barabarani, uchumi wetu unachechemea tunakuwa kiuchumi kwasababu tu ya ukuaji wa service sectors kama simu, financial institutions and tourism, sekta nyengine kama viwanda na madini plays a small part of our economy, agriculture ambayo ndio backbone yetu inakufa siku zinavyokwenda sasa jumuiya ya afrika mashariki itatusaidia kwa lipi?

Nilikuwa siku mmoja najadiliana na waganda na wakenya wakisifia jumuiya ya afrika mashariki nikawaambia hembu niambieni Tanzania itafaidika nini na jumuiya hiyo?? Jibu walikuwa hawana. Hebu nisaidie Shossi tutafaidika nini na jumuiya ya afrika mashariki??
 
Mohamed Shossi said:
Ila wazanzibar nawasupport kwani kuna kipindi nilikaa huko muda mrefu nikifanya kazi na kwakweli kilichonivutia ni ile great misconception tuliyokuwa tukifundishwa darasani kwamba zanzibar kilikuwa kituo kikuu cha biashara ya utumwa. Nikiwauliza wazawa wa kule wakawa wananibishia ndipo nikaamua kuisoma historia yao na kwakweli nimekubaliana nao kuwa haikuwa hivyo. Zanzibar ilikuwa ni kitivo cha biashara, mahusiano, na utumwa.

Mohammed,

..utawala wa Sultani wa Zanzibar hauwezi kukwepa shutuma kwa ushiriki wake ktk biashara ya utumwa.

..kile kitendo cha kushiriki, kuiwezesha,na kuifadhili, misafara ya kukamata na kuuza watumwa ni ushahidi tosha wa unyama wa utawala huo.

..Zanzibar pia ilifaidika kiuchumi kutokana na mapato yaliyotokana na kuwauza utumwani mababu zetu.
 
Mdondoaji said:
Siasa nyingi na ubinafsi wa viongozi wetu. Tunaingia katika EAC wakati sheria za ardhi bado hazijatekelezeka vema, uchumi haujasimama vema, umeme tatizo na tuna unemployment that is sky rocketing. Wakija wakenya wanachukua ardhi kwani wanaa strong currency hivyo kwao inakuwa rahisi kununua ardhi, kazi ndio kama ulivyosema makampuni yao kibao yapo hapa hivyo ukikuyu na ukalenjin kibao watu wetu watabakia wakitangatanga tu barabarani, uchumi wetu unachechemea tunakuwa kiuchumi kwasababu tu ya ukuaji wa service sectors kama simu, financial institutions and tourism, sekta nyengine kama viwanda na madini plays a small part of our economy, agriculture ambayo ndio backbone yetu inakufa siku zinavyokwenda sasa jumuiya ya afrika mashariki itatusaidia kwa lipi?

Nilikuwa siku mmoja najadiliana na waganda na wakenya wakisifia jumuiya ya afrika mashariki nikawaambia hembu niambieni Tanzania itafaidika nini na jumuiya hiyo?? Jibu walikuwa hawana. Hebu nisaidie Shossi tutafaidika nini na jumuiya ya afrika mashariki??

Mdondoaji,

..hapo tuko pamoja 100%.

..lakini labda suala hili aulizwe Kikwete manake EAC ilikuwa chini ya wizara ya mambo ya nje wakati wote wa utawala wa Nkapa.

..walipokuwa wana-sign mikataba walikuwa wanaisoma vizuri na kuielewa?
 
Faida kubwa tutakayoipata ni somo la kuwa DOMO-krasia la Tanzania, kuanzia mimi, wewe, JokaKuu. na wote hapa JF haisaidii kujenga jamii. Sisi tunapenda domo wajamaa wanapanga ujanja wa kuchukua kila kitakachowapa faida.

Pili sisi Tunaibana sana Zanzibar...kuna kadhia ya ugawaji wa faida ya benki kuu kwa mfano ambayo Zanzibar wanasema waliwekeza mtaji wa kama 12% lakini ni karibuni tu tokea ilipoanzishwa ndio wameanza kupata mgao wa hiyo faida tena ni 4.5%
sasa wakitokea wakenya wakiwa wababe kwetu ndio tutatia akili kuwa tulipaswa kuwatendea haki hawa Wazanzibari. wakati huo sisi kama watanganyika na wazanzibari tutakuwa tunataka kuuzuia ubabe wa Kenya.

In the end ,itatufanya tuamke na tufanye kazi na kuwa na mikakati mizuri kwa ajili ya nchi yetu. In fact sielewi mantiki ya sisi kuhofia wakenya, wakati sisi wenyewe tunafanya madudu hata pale kati yetu wanaposema wakuu, nchi haingozwi namna hii munavyoingoza. Na kama hatutaridhika na jumuiya na mambo yake, yale ya 1977 yatatokea tena. mambo mambo ifike wakati wa kuanzisha shirikisho la kisiasa.

faida nyengine ni kuwa tutakuwa na wakenya kama common threat, kwa hiyo, hizi longa longa za kidini zinazoibuka zitapungua kidogo, itatusaidia kuungana tena against the so called Kenyans threat.
 
Mdondoaji,

..Karume aliwahi kunukuliwa akisema "azimio la arusha mwisho chumbe". Zanzibar haikuwahi kuwa nchi ya kijamaa kama tunavyoujua huku Tanganyika.

..wakati mnasubiri kurudishiwa pwani ya Afrika mashariki, na kuanza kuchimba mafuta, kuna mambo ambayo mnapaswa kuyarekebisha ndani ya Zanzibar ya sasa ili msonge mbele.

..kuwa na eneo kubwa na rasilimali nyingi haimaanishi kwamba moja kwa moja mtapata maendeleo. we have all those things in Tanganyika lakini hatuna maendeleo kwasababu ya uongozi na mipango mibovu.

..narejea hoja yangu kwamba Zanzibar ilianza kudhoofika kidogo kidogo toka enzi za Sultani. kile kitendo cha kunyanganywa maeneo iliyokuwa "ikimiliki" ni ushahidi tosha kwamba Zanzibar ilikuwa dola dhaifu/inayodhoofika kulinganisha na dola zilizokuwepo wakati huo.

..we can discuss jinsi gani zao la karafuu limedorora hapo Zanzibar. inawezekana kabisa price controls ikawa moja ya sababu. hilo huwezi kusingizia muungano. karume alitaifisha ardhi kabla hata hatujaungana. inawezekana pia utaifishaji ardhi uliliweka zao hilo ktk mikono ya watu wasio na ujuzi na mitaji ya kilimo chake. we saw what happened in Tanganyika when sisal production was nationalised. hii inaweza kuwa thread inayojitegemea na si vizuri kutumbukiza siasa humo.

Mohamed Shossi,

..ni kweli Karume alikuwa na nia ya kuibadilisha Zanzibar ifanane na nchi zilizoendelea.

..tatizo lake ni kwamba alianza kuwekeza ktk miradi ambayo haikuwa sustainable.

..Karume alipaswa kuwekeza ktk sekta kama za viwanda, utalii, kuimarisha kilimo etc etc. badala yake akajikita kwenye sekta zinazotumia fedha kama kujenga nyumba za wazee, kuanzisha TV kama huduma na siyo biashara, etc etc.

..sasa utaona kwamba Karume alikuwa mtumiaji mzuri wa fedha badala ya kuwa mzalishaji mzuri.

..Zanzibar ni nchi ya kwanza kuwa na TV ya rangi, hilo halina ubishi. but what happened after that, ni muhimu zaidi. ungetegemea Zanzibar ndiyo wawe wanaongoza basi kwa utaalamu wa sekta ya habari ya TV ktk eneo hili la Afrika lakini sivyo.

..mwingine anajisifia Zanzibar ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na matawi ya mabenki ya Ulaya. this is another wrong notion. hizo benki zilikuwepo hapo kuinyonya Zanzibar na siyo kitu kingine. vijana wa leo tunapaswa kujiuliza what happened to Benki ya Watu wa Zanzibar. nini kimefanyika kuhakikisha benki hiyo inajitanua maeneo mbalimbali ya Zanzibar,Tanganyika,and beyond?

Joka kuu,

Vile vile Karume alipofatwa na Nyerere mara ya kwanza alimwambia hakuna muungano baina ya zanzibar na Tanganyika ila baada ya kuona anaweza kuja kupinduliwa na Babu ndio akasema zanzibar na Tanganyika ziungane, wewe jiulize kwanini terms and condition za muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanazifahamu Nyerere tu na Karume???

Vile sawa naweza kubaliana na wewe kuwa wazanzibari nao walichangia kwa namna fulani usocialism but the mastermind behind zanzibar revolution alikuwa Nyerere maana yeye ndio aliyekuwa akiratibu na kusimamia maandalizi yalipokuwa yakifanyika Dar. Vilevile walikuwa wakitrain vijana pindi watakaposhika madaraka waende kuongoza nchi au hilo unalibisha. Ndio maana walipoingia madarakani walikuwa na ideology kama ya Nyerere ya usocialism. Kama mwandishi huyu anavyosema:-

It has taken a full thirty years for Zanzibar to throw off the Marxist legacy of 1964 and some things will never recover: thanks to a disastrous experiment with state-owned collective farms, for example, the clove industry is virtually dead and cannot now be privatised again. But the V.I Lenin Hospital has survived (now rejuvenated and known by the politically neutral name of the Coconut Palm Infirmary), and a major restoration project is underway in Stone Town to preserve the finest of the old palaces before they crumble into the dust. Visitors to Zanzibar are now welcomed rather than restrained (as happened in the aftermath of the Revolution), and it is no longer assumed that anyone inspecting the buildings of Stone Town is necessarily doing so at the behest of the CIA. Hotels for backpackers have proliferated- parts of Stone Town are beginning to look like an African Goa- and one or two really good restaurants and hotels have also come up, notably Emerson's, the labour of love of a New York psychiatrist who came to Zanzibar four years ago, had a mid-life crisis, and decided to stay on.

(William Darlympe)

Vilevile unanyang'anyi wa eneo la pwani waliufanya wakati ambapo dola kuu duniani ilikuwa uingereza karne ya 19 na 18. Sasa nikuulize Sultani wa Zanzibar alikuwa na ubavu gani wa kupambana na Uingereza wakati ule. Ndio maana yule mwanasheria alinambia kama wakijenga kesi hawa jamaa zetu santuri itakuwa tamu Joka Kuu kwani waingereza na wajerumani walitumia ubabe kumnyang'anya Sultani wa zanzibar eneo alilokuwa akimiliki kihalali na kisheria. So hapa sio kwamba eti dola ilikuwa weak hapana ila walitumia ubabe na ubeberu kwasababu walijua bandari ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi zao. Ni kama sasa hivi ilivyo Hong Kong na China unataka kuniambia Hong Kong ni dola weak? Chechnya na Russia , Hawaii na US, na kwengineko kwingi tu. So hoja yako sio sahihi na ni weak.

Kuhusu uongozi mbovu sikatai na in fact nakuunga mkono kuwa lack of accountability na ufisadi unachangia kurudisha nyuma maendeleo but tukitazama impact yake na impact ya kumezwa na muungano nadhani hasara ni kubwa zaidi. Mfano Per capital income ya mzanzibar before muungano na miaka michache baada ya muungano ilikuwa £7,000 au $20,580 sasa hivi per capital income ya mtanzania including mzanzibari ni $720 tu! sasa nikuulize ni akina nani wameumia? Unakuta muungano una hasara zaidi kuliko hayo unayoyasema ambayo very trivial.

Vile nimekupa mfano wa banking sectors kuwapo africa mashariki zanzibar kwa maana kuwa it is a signal ya jinsi Zanzibar uchumi wake ulikuwa imara. Wewe, nikuulize swali kwanini hawakufungua branch za benki zao Tanganyika??? Vilevile, nikuulize benki za nje zinafata nini katika nchi zaidi ya kutengeneza faida?

Baadhi ya maneno mengine naweza kukubaliana na wewe mfano Karume alikuwa mtumiaji zaidi ya uzalishaji but hilo linachangiwa na kuwa jamaa alikuwa hajasoma hata darasa mmoja. alichukuliwa toka Malawi na Nyerere ili aje kuongoza nchi for the interest ya Nyerere. Hata hivyo Karume alikuwa na uzalendo na ndio maana aliweza kujenga barabara na nyumba ila alikuwa hataki ushauri wa wasomi maana alikuwa akiwahofia watampindua. Sasa hata wewe ukimweka mtu asiyejua nini unafanya unadhani who will take the blame? Nyerere na Tanganyika mkuu we have our big share of blame usikatae hilo.
 
Mdondoaji,

..hapo tuko pamoja 100%.

..lakini labda suala hili aulizwe Kikwete manake EAC ilikuwa chini ya wizara ya mambo ya nje wakati wote wa utawala wa Nkapa.

..walipokuwa wana-sign mikataba walikuwa wanaisoma vizuri na kuielewa?

Ndio maana nikasema,

Siasa nyingi na ubinafsi ndio kiini cha kukwama kiuchumi nchi yetu. Kuna nchi kama South Korea waziri mkuu wa nchi alidhamiria kuwa nchi yake inakuwa nchi ya viwanda akasimamia uanzishwaji wa kiwanda cha meli (sasa wanaongoza duniani katika uundaji wa meli), kuzalisha magari mpaka makampuni ya marekani na ulaya kama BMW magari yao wanatengenezea huko. Wao wana nini na sie tuna nini jibu unapata siasa nyingi na ubinafsi tu!!!
 
Mdondoaji,

..kuna mambo ambayo Karume aliyafanya yapo ktk sera za kijamaa. mojawapo ni utaifishaji wa ardhi. lakini sidhani kama alikuwa anafanya hivyo kwasababu alikuwa akiamini ktk siasa za Ki-Maxist. naamini Karume alichukua hatua hizo akiamini anatenda haki kwa jamii ya Waafrika wa Zanzibar.

..naona kuna hali ya wewe kujenga hoja moja halafu kuja kuikanusha ktk posting inayofuatia. nilieleza kwamba Zanzibar ilikuwa ikidhoofika kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele. pia nilieleza kwamba Zanzibar ilikuwa dola dhaifu kulinganisha na dola nyingine za wakati ule. ukweli huo ndiyo uliosababisha kupoteza maeneo yake kadhaa, na mpaka kufikia kuwa Protectorate["koloni"] ya Muingereza.

..kama Zanzibar haikuwa dola weak basi wao ndiyo wangekuwa vinara wa ile scramble for Africa. Dola ya Zanzibar/Oman ndiyo ingekuwa inatwaa maeneo ya dola nyingine kama Uingereza, Ujerumani, etc etc.

..kuhusu suala la Zanzibar kuwa na haki ya kumiliki maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki hilo nawaachia wajuzi wa historia. lakini suala moja la kujiuliza ni kwamba nafasi ya waafrika ktk hiyo legal argument ya Wazanzibar/Sultani wa Oman/Sultani wa Zanzibar itakuwa ni nini? Je, ni kuna mkataba wowote ule halali uliommilikisha Sultani wa Oman/Zanzibar Pwani nzima ya Afrika Mashariki?

NB:

..Mwalimu alibadilika na kuwa Mjamaa in 1967[Azimio la Arusha] that was 4yrs after Zanzibar revolution.

..kuna nyaraka zinazoelekeza kwamba Muungano ulilazimishwa na nchi za magharibi, in particular USA, kwa kuhofia Zanzibar kuwa ngome ya Ukomunisti Afrika Mashariki.

..vijana wasomi wa Kizanzibar waliokuwa na imani za kijamaa kama Abdulrahman Babu walihamishiwa Tanganyika ili kuiepusha Zanzibar na sera za Kikomunisti.

..sina uhakika kama Nyerere alilazimisha sera zake za kijamaa huko Zanzibar.
 
Hivi zaidi ya karafuu, utalii na bandari kuna fursa gani zingine za maana za kiuchumi Zanzibar? Au ndiyo hayo mafuta tunayoambiwa yapo na yameanza kuleta chokochoko?

Mafuta gani?? Mbona mafuta yenyewe waliyonayo yanatosha kupaka mwilini tu!! Basi tu roho ya kwanini inawasumbua...
 
Ndio maana nikasema,

Siasa nyingi na ubinafsi ndio kiini cha kukwama kiuchumi nchi yetu. Kuna nchi kama South Korea waziri mkuu wa nchi alidhamiria kuwa nchi yake inakuwa nchi ya viwanda akasimamia uanzishwaji wa kiwanda cha meli (sasa wanaongoza duniani katika uundaji wa meli), kuzalisha magari mpaka makampuni ya marekani na ulaya kama BMW magari yao wanatengenezea huko. Wao wana nini na sie tuna nini jibu unapata siasa nyingi na ubinafsi tu!!!

Hasa Zanzibari maana hata kwenye baraza la wawakilishi ikitikea jambo lolote linaloweza kuleta maslahi kwa uwiano wa muungano utasikia "HILI HALIPO KWENYE MUUNGANO" waaaaaaaapi... Mtakuja kuchapana bakora wenyewe... subirini
 
Mdondoaji,

..kuna mambo ambayo Karume aliyafanya yapo ktk sera za kijamaa. mojawapo ni utaifishaji wa ardhi. lakini sidhani kama alikuwa anafanya hivyo kwasababu alikuwa akiamini ktk siasa za Ki-Maxist. naamini Karume alichukua hatua hizo akiamini anatenda haki kwa jamii ya Waafrika wa Zanzibar.

..naona kuna hali ya wewe kujenga hoja moja halafu kuja kuikanusha ktk posting inayofuatia. nilieleza kwamba Zanzibar ilikuwa ikidhoofika kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele. pia nilieleza kwamba Zanzibar ilikuwa dola dhaifu kulinganisha na dola nyingine za wakati ule. ukweli huo ndiyo uliosababisha kupoteza maeneo yake kadhaa, na mpaka kufikia kuwa Protectorate["koloni"] ya Muingereza.

..kama Zanzibar haikuwa dola weak basi wao ndiyo wangekuwa vinara wa ile scramble for Africa. Dola ya Zanzibar/Oman ndiyo ingekuwa inatwaa maeneo ya dola nyingine kama Uingereza, Ujerumani, etc etc.

..kuhusu suala la Zanzibar kuwa na haki ya kumiliki maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki hilo nawaachia wajuzi wa historia. lakini suala moja la kujiuliza ni kwamba nafasi ya waafrika ktk hiyo legal argument ya Wazanzibar/Sultani wa Oman/Sultani wa Zanzibar itakuwa ni nini? Je, ni kuna mkataba wowote ule halali uliommilikisha Sultani wa Oman/Zanzibar Pwani nzima ya Afrika Mashariki?

NB:

..Mwalimu alibadilika na kuwa Mjamaa in 1967[Azimio la Arusha] that was 4yrs after Zanzibar revolution.

..kuna nyaraka zinazoelekeza kwamba Muungano ulilazimishwa na nchi za magharibi, in particular USA, kwa kuhofia Zanzibar kuwa ngome ya Ukomunisti Afrika Mashariki.

..vijana wasomi wa Kizanzibar waliokuwa na imani za kijamaa kama Abdulrahman Babu walihamishiwa Tanganyika ili kuiepusha Zanzibar na sera za Kikomunisti.

..sina uhakika kama Nyerere alilazimisha sera zake za kijamaa huko Zanzibar.

Kuna kipindi nilikuwa katika mkutano wa kihistoria kuhusu mipaka ya kale waliuliza swali kama hilo Je Sultani Baragrash aliipataje ile ardhi ya pwani inasemekana aliinua kwa wazawa wa pwani kwa riyale za kioman sikumbuki ngapi? Swali likaulizwa na wahudhuriaji je ikija kutuokea zanzibar wakidai fidia itakuwaje? ni maswali hayajibiki kiurahisi na yanahitaji mjadala wa kina ila wazanzibari wakidai ardhi yao tujiandae kuhama Dar na kina ndugu zangu Shossi Tanga itawapasa wahame maana wenye nchi yao wanaidai.....
 
Mafuta gani?? Mbona mafuta yenyewe waliyonayo yanatosha kupaka mwilini tu!! Basi tu roho ya kwanini inawasumbua...
Kiherehere una vithibitisho kuwa mafuta ni ya kujipaka? Kama ni hivyo kazi itakuwa nzito!!! Mie kuna mtaalamu alinambia kuwa mafuta yako mengi?
 
Mdondoaji said:
Kuna kipindi nilikuwa katika mkutano wa kihistoria kuhusu mipaka ya kale waliuliza swali kama lako Je Sultani Baragrash aliipataje ile ardhi ya pwani inasemekana aliinua kwa wazawa wa pwani kwa riyale za kioman sikumbuki ngapi? Swali likaulizwa na wahudhuriaji je ikija kutuokea zanzibar wakidai fidia itakuwaje? ni maswali hayajibiki kiurahisi na yanahitaji mjadala wa kina ila wazanzibari wakidai ardhi yao tujiandae kuhama Dar na kina ndugu zangu Shossi Tanga itawapasa wahame maana wenye nchi yao wanaidai.....

Mdondoaji,

..kuna mahali nilisikia kwamba Sultani alilipwa ili kuachia hilo eneo la pwani ya afrika mashariki.

..labda hao wenyeji wa Pwani, kama bado wapo, waanzishe harakati za kutaka kurudi kwa mmiliki wao wa zamani Sultani wa Zanzibar/Oman.

..Zanzibar napo Sultani hakuwa mwenyeji. sasa huko nako alilipataje eneo hilo?
 
Huenda wangekuwa kama Yemen. Kabla bei ya Karafuu kuanguka, ni kweli Uchumi wa zanzibar ulikuwa imara sana, lakini baada ya mazao hayo kufa, Uchumi wa zanzibar haukuwa na lternative nyingine. Kwa sasa hivi mambo ya Zenj yanakwenda vizuri kwa sababu ya utalii, ila iwapo wangekuwa alkaida wa kutaka wanawake wafunge nyuso zao kwa mbaibui, basi wangekuwa kama Yemeni ya leo.

Labda kungekuwa na tofauati kidogo kama Zanzibar ingebaki chini ya Sultani wa Oman, lakini basi kwa utaratibu huo, Zanziba ingekuwa ni nchi ya kiarabau na hawa wamatumbi wenzetu wasingekuwa na lao. Kwanza hata wasingeruhiswa kuchanganya damu na waarabu kama ambavyo Karume alilazimisha baada ya mapinduzi

Mkuu maelezo yako hayana ukweli hata kidogo kwa kukupa elimu ya ziada tu ni kuwa nchi ya Oman nusu ya bajeti yake ilikuwa inategemea pesa kutoka Zanzibar.

Nadhani pia unapotoka unaposema wanaofunika nyuso zao ni maalkaida sidhani kama una uelewa au ndio chuki tu za wanaojisitiri miili yao unataka watu watembee nusu uchi? kumbuka kuwa Zanzibar majority ni waislam na waislamu wana tamaduni zao na wameanza kujifunika nyuso zao hata alkaida ilikuwa haijulikani! Naomba nikuulize swali.....Nina lolly pop mbili moja nimeifungua na nyingine nimeifunga halafu zote mbili nazitupa chini halafu nakuambia uokote moja na uile utaiokota iliyofungwa au iliyofunguliwa?
 
Back
Top Bottom