ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
isak ndodi ninamfahamu sana, sijawi kupata tiba kotoka kwake. huyu bana ni muumini wa kanisa la sabato. mimi si msabato bali kama kuna walio wasabato ndani ya JF wanaweza wakaeleza yeye ( ndodi) ni nani. nilimfahamu ndodi huko songea, anachokifanya ndodi si jambo geni kwani hakusomea popote na siyo daktari kwa kuwa na degree ya medicine au daktari kama wale wanaoagua bagamoyo. nijuavyo mimi ndani ya kanisa la sabato wanautaratibu wa kuta elimu juu ya tiba asilia kwa kutumia mimea kutibu au kujenga afya ya mwili. kanisa la sabato lina vitabu vinavyoeleza aina ya mmea , magonjwa yanayoweza kuponywa kwa mmea huo, na hata namna ya kuandaa dawa na dozi yake kwa ugonjwa husika. hivyo vitabu vipo. isak alikuwa akifudisha vipindi vya dini (sabato) pale songea ktk shule za sekondari.wakati huo alikuwa anafundisha bible na si haya ya tiba mubadala. nadhani hapo ndiyo alijifunza kuongea mbele ya watu. lakini anachokifanya sasa ni kutangaza vile vitabu vya tiba vya kisabato, ukienda kwake atakupatia hicho kitabu utasoma na wewe utaamua wapi kwa kwenda kupata hiyo aina ya mmea / tunda/mbegu a u hata majani kwaajili ya tiba. kama aina ya ugonjwa huijui isak hawezi kukusaidia na atakwambia hana cha kufanya nawe. yeye hafanyi diagnosis( hafanyi kutambua unaumwa nini) , ukijua unaumwa nini , anaweza kukuongoza kwenye tiba. ninauhakika kama kanisa la sabato litamgundua akifanya diagnosis watamfungia mara moja. faida yake ipo kwenye kutoa huo ushauri wa tiba, na pia anauza hivyo vitabu ambavyo vinatoa mwongozo wa tiba. hata ukienda baadhi ya maduka ya vitabu, utakuta hivyo vitabu vya tiba, na mtunzi siyo isak, ni watu wengine kabisa, yeye amefahamu kupitia kusoma hivyo vitabu. kwa lugha nyingine unaweza kwenda kwa isak na ukanunua kitabu chako ukajisomea namna ya kulinda afya yako.
umaarufu wa isak hautokani na uelewa mdogo wa watanzania bali unatokana na watu kujali afya zao. mtu akisema isak anazungumza juu ya machungwa na akadai mbona sote tunajua juu ya machungwa, tukumbuke hata tunapokwenda hosptali tunakuwa hatujui tunaumwa nini, hapo tunaambiwa chanzo cha ugonjwa na tiba , ambavyo utakuta ni vya kawaida kabisa. tuwaache wanaoumwa wahoji uwezo wa isak, lakini sisi wenye afya hatumhitaji isak mpaka tutakapo umwa
Sasa we mzee wa "kindimba juu" ulijifunza nini kwenye hilo darasa la sabato huko songea? unge wahi haka kaujanja mema kabla ya Ndodi!!