Isaac Ndodi: Umaarufu Gani Huu?

Heeeee

Hivi hukupata kusikia jinsi yule mganga wa jadi aliyekuwa akiitwa...sijui LIMBE naninani huko, alivyomchukua mtoto bomba NORA ,yule mwIGIZAJI wa runinga?

Mbona pia kuna rafiki yangu humu jamvini anajiita NG'WANA MADASO. ana mchumba bomba mbaya!...lol!

hahaha yaani leo klorokwini kanichekesha kila post nayopita inaniacha hoi PJ
 
Ana matatizo huyu rafiki yangu sana...!

Mi sikuwa na mpango wa kwenda kumwona huyu ndodi, lakini kwa jinsi ninavyosikia wasimulizi wanavyomgwaya, itabidi nifike Sheikh Abeid Amani nikashuhudie, na huenda nikabadilisha mtizamo wangu wa kitiba!

Ama kweli nabii hathaminiki kwao, na matabibu wa kigeni (WACHINA)ndo wanaobebwa na kuonekana wataalamu zaidi.!
 
Huku Dar mbona mtu wa kawaida tu na ofisi zake zipo Magomeni watu tunamchukulia kama mganga njaa tu.

Hivi kumbe ukiwa na OFISI MAGOMENI huthaminiki ee?..au ni mpaka uwe nazo mtaa wa Azikiwe eeh!...sikujua!

Lakini pia mnatakiwa MSIMCHUKULIE MTU tu, try a single step, onja huduma zake, then utakuwa katika position ya kusema kama ni MGANGA NJAA au vp.

Sidhani kama anaweza kuwa'fool watu wote hao kwa tiba zisizokuwa effective...lololo!...Hii Bongo bana!
 
iveni mi amu wochingi yu mai dia.

pj tuwasiliane bwana tuko hapa watoto wa mujini wanaita A Tau wote tuanzishe kaclabu cheti na sisi kama kile chawote na zero p

Hayo ndo maneno sasa..
Ebu niPM ili tujue tutafanyafanyaje, maana tukitumia jukwaa hili wambeya watatuharass!...We huoni watu wa Dar wanajichimbia hadi wanakuwa ma- Invisible woote!..utawasikia ..oooh mara tuonane KITUNDA,..mara tukutane Bonyokwa, sisi hazarani bana, haogopwi mtu hapa!
 
Naona wengi wamemshambulia sana huyu Dr. Isac Ndodi. Binafsi sijapata huduma za tiba zake ila naamini kuna watu ambao wao binafsi au ndugu na marafiki/majirani wamehudumiwa na huyu binadamu. Ningependa wajitokeze hadharani watoe shuhuda ili tuone matokeo makubwa ya hizi dawa.

Ninamsikiliza sana katika kipindi chake Star TV, ninamkubali kwa vipindi vyake hasa kuhusu vyakula tunavyokula na madhara ya baadhi yake na nini tufanye tuachane na magonjwa ya kujitakia. Yote yale anayosema ni sawa kabisa theoretically, practically ni kwa kutumia dawa zake, ambazo tunataka shuhuda hapa.

Tusipende kushambulia kwa lugha kali bila kufanya uchambuzi wa kina. Hebu imagine dawa za kichina zilivyotapakaa na hujui wala mtengenezaji na wala kama kampuni hizo ziko duniani lakini bado tunanunua wakati kule kwao hawazitumii. Ni lini basi tutakubali kuwa huwa pia Tanzania kuna vipaji na wavumbuzi na hao basi wanatakiwa wasaidiwe au kuenziwa ili tuwe na patent rights zetu???

Kuna rafiki yangu mjukuu wake alikuwa anasumbuliwa na malaria sana na alipata dawa kwa Dr. Ndodi magomeni(dose ni a bit expensive) na alipona kabisa na walishasahau kama mtoto alikuwa ni msumbufu. Walikiuwa hawakosi hospital kwa dawa na drips za malaria. Let us praise our traditions, traditional medicine kama zitakuwa administered inavyotakiwa ni the best.

Afya yako utailinda kwa aina ya chakula unachokula na wala hutahitaji kumtembelea Dr. Ndodi. Imagine wala nyama za kuchoma sinia na bia, ndizi rost on top, chips, kuku broilers na mifupa unatafuna wakati dawa zote za makuzi yake huwa kwenye mifupa, you name all food related toxic in our bodies!!!

Bottom line afadhali Ndodi amepokelewa kwa vifijo A town kuliko mapokezi ya kifisadi Monduli na Shinyanga jimbo la cheupe ambaye mikataba yake mibovu ime-undermine huduma za serikali hasa kwa huduma za jamii(imagine shule hazina huduma na hospital hazina madawa na vitendea kazi na mishahara mibovu). Hayo madola yange top up mishahara na huduma. All the best comrade Ndodi.
 
I think its high time we went for the altenative medication, maana madawa haya ya madukani yana side effects nyingi mno ambazo, kwa bahati mbaya hatuzijui.

Isaac ndodi, japo mi si wakala wake anakuelekeza jinsi ya kutumia hivi vitu vya asilia, na more interesting hakupi yeye, anakwambia ukavinunue popote...so unajitibu kwa kitu ulicho na uhakika nacho...
I see it as a revolutional treatment!

PJ,

sisi mzee tumepoteza asili zetu. Kuna mti, sijui tunda au jani...anyway kwa kibongo sijui lakini kinombo ni "Aloe Vera" kwa historia ya Botany inaonekana kuwa hii kitu ina asili ya Afrika na sina shaka Tz moja wapo. Hii Aloe vera ni tiba ya asili ya ajabu sana kwa sababu inachance kwenye magonjwa mengi sumbufu nakumbuka zamani ukikanyaga kinyesi utatoka fangasi miguuni, unapakwa just a day kidonga kinasalimu amri!, ukiumwa tumbo linachemshwa ganda, piga maji yako glasi no dozi na tumbo kwisha habari yake. Aloe vera ilikuwa ikistawi hovyo porini, leo inasemekana inalimwa shambani na hii ni baada ya wazungu kujua habari zake na kuifanyia kazi. Ni sisi black ndio tuliowapa everthing kama walivyojua wapi kuna madini wakatengeneza shanga na dhahabu na kutuuzia kwa hela nyingi. Leo hii products nyingi za Aloe Vera zinatoka China kama sio Ulaya na Marekani.

Kuna mtaalamu alikuwa anatibu magonjwa hatarishi kama kansa na UPUNGUFU WA KINGA MWILINI na inasadikika kwa kutumia mitishamba watu walikuwa wanapona (not joke!). Lakini taarifa nilizonazo ni kuwa huyo mzee badae alipigwa marufuku kuingia kwenye chimbo (msitu)ambao alikuwa ana source hizo dawa na hii ni baada ya baadhi ya watafiti wa madawa ya asili kwenda na wazungu kwa huyo mzee na kupewa details zote za miti inayotumia. Mzee amezuiwa eti anaingilia misitu ya hifadhi bila kibali!....

Tofauti na nchi nyingine, TZ haina sheria ya kulinda Nasaba za Mimea (Plant Genetic Resource) ambazo ndicho chanzo kikuu cha ugunduzi unaoendelea kwenye dunia ya mbele!. Wazungu wakija tunawakarimu kwa kuwaelekeza katika miti muhimu (it happened in Lushoto).

Kuna ma profo pale Sokoine Uni wamehusika katika study iliyofadhiliwa na wazungu ku document miti yote ya asili na umuhimu wake kwa tiba au chakula nk. Ni kitabu kikubwa kinachoelekeza wapi miti hiyo inapatikana TZ, na majina yake kwa lugha za kienyeji na kitaalamu (botanical and family names) na pia michoro kuonyesha ilivyo .

Funny, ....Sijui jamaa walilipwa how much lakini wakati ili linafanyika TZ haina sheria ya kumzuia mzungu au mtu mwingine yeyote kuihamisha by way of piracy nasaba za miti hiyo na badae kusikia kama haya ya Alove Vera sasa inasemekana inalimwa Marekani wakati ambapo wale waliohusika kuilinda huko porini kwa milongo na milongo ya miaka (Wa Afrika) sijui kama wamenufaika kwa kiasi gani zaidi ya kulanguliwa na artificial products"
 
Naona wengi wamemshambulia sana huyu Dr. Isac Ndodi. Binafsi sijapata huduma za tiba zake ila naamini kuna watu ambao wao binafsi au ndugu na marafiki/majirani wamehudumiwa na huyu binadamu. Ningependa wajitokeze hadharani watoe shuhuda ili tuone matokeo makubwa ya hizi dawa.

Ninamsikiliza sana katika kipindi chake Star TV, ninamkubali kwa vipindi vyake hasa kuhusu vyakula tunavyokula na madhara ya baadhi yake na nini tufanye tuachane na magonjwa ya kujitakia. Yote yale anayosema ni sawa kabisa theoretically, practically ni kwa kutumia dawa zake, ambazo tunataka shuhuda hapa.

Tusipende kushambulia kwa lugha kali bila kufanya uchambuzi wa kina. Hebu imagine dawa za kichina zilivyotapakaa na hujui wala mtengenezaji na wala kama kampuni hizo ziko duniani lakini bado tunanunua wakati kule kwao hawazitumii. Ni lini basi tutakubali kuwa huwa pia Tanzania kuna vipaji na wavumbuzi na hao basi wanatakiwa wasaidiwe au kuenziwa ili tuwe na patent rights zetu???

Kuna rafiki yangu mjukuu wake alikuwa anasumbuliwa na malaria sana na alipata dawa kwa Dr. Ndodi magomeni(dose ni a bit expensive) na alipona kabisa na walishasahau kama mtoto alikuwa ni msumbufu. Walikiuwa hawakosi hospital kwa dawa na drips za malaria. Let us praise our traditions, traditional medicine kama zitakuwa administered inavyotakiwa ni the best.

Afya yako utailinda kwa aina ya chakula unachokula na wala hutahitaji kumtembelea Dr. Ndodi. Imagine wala nyama za kuchoma sinia na bia, ndizi rost on top, chips, kuku broilers na mifupa unatafuna wakati dawa zote za makuzi yake huwa kwenye mifupa, you name all food related toxic in our bodies!!!

Bottom line afadhali Ndodi amepokelewa kwa vifijo A town kuliko mapokezi ya kifisadi Monduli na Shinyanga jimbo la cheupe ambaye mikataba yake mibovu ime-undermine huduma za serikali hasa kwa huduma za jamii(imagine shule hazina huduma na hospital hazina madawa na vitendea kazi na mishahara mibovu). Hayo madola yange top up mishahara na huduma. All the best comrade Ndodi.

Maane,
This content of yours is from the HORSES MOUTH, and i take it without any caution.!

We humans are born with 4getting genes, and we there4 need to be constantly reminded of the good upkeep of our bodies, which includes the use of natural /herbal medication!
Bravo.
 
Kila nikigusa glasi ya maji baada ya tonge moja namkumbuka ndodi. Jamaa anatoa ushauri si mbaya ila tatizo lake anaongea kama chiriku. Namshauri ajifunze kutumia kompyuta ili hayo anayoongea ayasave kwenye pc kwa ajili ya kizazi chake kijacho.

Poleni wamasai wa aarusha kwa kupaliwa na jam ya magari. ila ndo hivyo sisi huku dar hatumkubali sana kwani imenenwa kuwa nabii hakubaliki kwao.

Wabongo wakiambiwa ukweli wanaonesha mishipa ya shingo ila akipigwa changa la macho wanapiga vigelegele. Kama unabisha subiri 2010 uone wabongo wanavyopenda fake things
 
isak ndodi ninamfahamu sana, sijawi kupata tiba kotoka kwake. huyu bana ni muumini wa kanisa la sabato. mimi si msabato bali kama kuna walio wasabato ndani ya JF wanaweza wakaeleza yeye ( ndodi) ni nani. nilimfahamu ndodi huko songea, anachokifanya ndodi si jambo geni kwani hakusomea popote na siyo daktari kwa kuwa na degree ya medicine au daktari kama wale wanaoagua bagamoyo. nijuavyo mimi ndani ya kanisa la sabato wanautaratibu wa kuta elimu juu ya tiba asilia kwa kutumia mimea kutibu au kujenga afya ya mwili. kanisa la sabato lina vitabu vinavyoeleza aina ya mmea , magonjwa yanayoweza kuponywa kwa mmea huo, na hata namna ya kuandaa dawa na dozi yake kwa ugonjwa husika. hivyo vitabu vipo. isak alikuwa akifudisha vipindi vya dini (sabato) pale songea ktk shule za sekondari.wakati huo alikuwa anafundisha bible na si haya ya tiba mubadala. nadhani hapo ndiyo alijifunza kuongea mbele ya watu. lakini anachokifanya sasa ni kutangaza vile vitabu vya tiba vya kisabato, ukienda kwake atakupatia hicho kitabu utasoma na wewe utaamua wapi kwa kwenda kupata hiyo aina ya mmea / tunda/mbegu a u hata majani kwaajili ya tiba. kama aina ya ugonjwa huijui isak hawezi kukusaidia na atakwambia hana cha kufanya nawe. yeye hafanyi diagnosis( hafanyi kutambua unaumwa nini) , ukijua unaumwa nini , anaweza kukuongoza kwenye tiba. ninauhakika kama kanisa la sabato litamgundua akifanya diagnosis watamfungia mara moja. faida yake ipo kwenye kutoa huo ushauri wa tiba, na pia anauza hivyo vitabu ambavyo vinatoa mwongozo wa tiba. hata ukienda baadhi ya maduka ya vitabu, utakuta hivyo vitabu vya tiba, na mtunzi siyo isak, ni watu wengine kabisa, yeye amefahamu kupitia kusoma hivyo vitabu. kwa lugha nyingine unaweza kwenda kwa isak na ukanunua kitabu chako ukajisomea namna ya kulinda afya yako.
umaarufu wa isak hautokani na uelewa mdogo wa watanzania bali unatokana na watu kujali afya zao. mtu akisema isak anazungumza juu ya machungwa na akadai mbona sote tunajua juu ya machungwa, tukumbuke hata tunapokwenda hosptali tunakuwa hatujui tunaumwa nini, hapo tunaambiwa chanzo cha ugonjwa na tiba , ambavyo utakuta ni vya kawaida kabisa. tuwaache wanaoumwa wahoji uwezo wa isak, lakini sisi wenye afya hatumhitaji isak mpaka tutakapo umwa
 
It was Tanzania bila ufisadi haiwezekani, now ni dini pia....!? Mungu atunusuru katika haya majanga
 
Namsikia huyu bwana anajitangaza kwenye Star TV na Redio Free Afrika, binafsi sijawahi kukutana na mtu ninayemfahamu aliyetibiwa na bwana huyu. Kwa imani naamini kwamba watu wenye vipaji vya kweli wapo labda naye ni mmoja wapo.

Tatizo ni miundo mbinu hafifu tuliyonayo kama nchi na mipango ya matumizi ya miundombinu hiyo. Ina kuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara pale ambapo anakuja mtu mmoja hata kama ni rais wa nchi watu wanashindwa kwenda makazini barabara zinakuwa zimefungwa hii inakinzana na jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. Hivyo kinachotakiwa kufanyika ni kwamba tupange namna bora za kutumia hii miundombinu michache tuliyonayo. Ili isijefikia wakati wananchi watakuwa wanachukia ujio wa viongozi katika maeneo yao kwa sababu inakuwa KERO.
 
Guyz..acheni kuponda vitu msivyokuwa na uhakika navyo, jamaa kauliza swali zuri afahamishwe kuhusu Dk. Ndodi, lakini hapa naona watu wanajibu lakini kwa hisia tu bila kujua ukweli, chuki binafsi. Mimi sijatumia dawa zake, ila wapo watu wengi wametumia dawa zake na zimewatibu na wanashuhudia hilo, dawa zake nyingi anatumia mchanganyiko wa matunda mbalimbali. Huo umaarufu unaouona na kwa sababu amekubalika sio kwa sababu ya kujua kuongea bali kwa tiba zake mbadala ambazo zimeponya wengi. Yeye haombei watu kama wengine wanavopotosha humu ndani, wala hafanyi miujiza kama wengine wanavosema, yeye ni dokta tu wa kawaida sema pia ni mchungaji wa makanisa ya kisabato, lakini safari zake hizo sio za huduma ya kichungaji. Hope wanaotaka kujua wameanza kupata mwanga, kwa wale wenye data zaidi watujuze zaidi.

Is he a Medical Doctor (MD)? Why opted to such method? Ni magonjwa ya aina gani anatibu hasa? Au hana specialization, anatibu kila kitu?
 
Guyz..acheni kuponda vitu msivyokuwa na uhakika navyo, jamaa kauliza swali zuri afahamishwe kuhusu Dk. Ndodi, lakini hapa naona watu wanajibu lakini kwa hisia tu bila kujua ukweli, chuki binafsi. Mimi sijatumia dawa zake, ila wapo watu wengi wametumia dawa zake na zimewatibu na wanashuhudia hilo, dawa zake nyingi anatumia mchanganyiko wa matunda mbalimbali. Huo umaarufu unaouona na kwa sababu amekubalika sio kwa sababu ya kujua kuongea bali kwa tiba zake mbadala ambazo zimeponya wengi. Yeye haombei watu kama wengine wanavopotosha humu ndani, wala hafanyi miujiza kama wengine wanavosema, yeye ni dokta tu wa kawaida sema pia ni mchungaji wa makanisa ya kisabato, lakini safari zake hizo sio za huduma ya kichungaji. Hope wanaotaka kujua wameanza kupata mwanga, kwa wale wenye data zaidi watujuze zaidi.

Una maana gani? Ni daktari mwenye taaluma ya udaktari au aliyejiita kwa sababu anatibu kwa mitishamba?
 
isak ndodi ninamfahamu sana, sijawi kupata tiba kotoka kwake. huyu bana ni muumini wa kanisa la sabato. mimi si msabato bali kama kuna walio wasabato ndani ya JF wanaweza wakaeleza yeye ( ndodi) ni nani. nilimfahamu ndodi huko songea, anachokifanya ndodi si jambo geni kwani hakusomea popote na siyo daktari kwa kuwa na degree ya medicine au daktari kama wale wanaoagua bagamoyo. nijuavyo mimi ndani ya kanisa la sabato wanautaratibu wa kuta elimu juu ya tiba asilia kwa kutumia mimea kutibu au kujenga afya ya mwili. kanisa la sabato lina vitabu vinavyoeleza aina ya mmea , magonjwa yanayoweza kuponywa kwa mmea huo, na hata namna ya kuandaa dawa na dozi yake kwa ugonjwa husika. hivyo vitabu vipo. isak alikuwa akifudisha vipindi vya dini (sabato) pale songea ktk shule za sekondari.wakati huo alikuwa anafundisha bible na si haya ya tiba mubadala. nadhani hapo ndiyo alijifunza kuongea mbele ya watu. lakini anachokifanya sasa ni kutangaza vile vitabu vya tiba vya kisabato, ukienda kwake atakupatia hicho kitabu utasoma na wewe utaamua wapi kwa kwenda kupata hiyo aina ya mmea / tunda/mbegu a u hata majani kwaajili ya tiba. kama aina ya ugonjwa huijui isak hawezi kukusaidia na atakwambia hana cha kufanya nawe. yeye hafanyi diagnosis( hafanyi kutambua unaumwa nini) , ukijua unaumwa nini , anaweza kukuongoza kwenye tiba. ninauhakika kama kanisa la sabato litamgundua akifanya diagnosis watamfungia mara moja. faida yake ipo kwenye kutoa huo ushauri wa tiba, na pia anauza hivyo vitabu ambavyo vinatoa mwongozo wa tiba. hata ukienda baadhi ya maduka ya vitabu, utakuta hivyo vitabu vya tiba, na mtunzi siyo isak, ni watu wengine kabisa, yeye amefahamu kupitia kusoma hivyo vitabu. kwa lugha nyingine unaweza kwenda kwa isak na ukanunua kitabu chako ukajisomea namna ya kulinda afya yako.
umaarufu wa isak hautokani na uelewa mdogo wa watanzania bali unatokana na watu kujali afya zao. mtu akisema isak anazungumza juu ya machungwa na akadai mbona sote tunajua juu ya machungwa, tukumbuke hata tunapokwenda hosptali tunakuwa hatujui tunaumwa nini, hapo tunaambiwa chanzo cha ugonjwa na tiba , ambavyo utakuta ni vya kawaida kabisa. tuwaache wanaoumwa wahoji uwezo wa isak, lakini sisi wenye afya hatumhitaji isak mpaka tutakapo umwa

Sasa we mzee wa kindimba juu uljiunza huko songea kwnye hyo shule ya Ndodi? unge wahi haka kaujaa mema !!
 
Back
Top Bottom