Is our president serious?

Mungu wangu jamaa ametuaibisha yani hii inaonesha hata sisi wananchi wake ni vilaza, hii sio issue ya lugha au kutokuwa na data ni kwamba hakuelewa swali kabisa. Ama kweli tulichagua sura!!
 
He proves his incapacity...and people allow this kind of a man to be their LEADER! He's uneducated, his w.i.f.e uneducated as well. What do they talk at home?
 
P53,
hapana mkuu sikukuweka nafasi moja na JK hata kidogo isipokuwa nilidhani mwenzangu unalo jibu zuri kuliko la JK..
Mkuu, hata mimi nimejiuliza swali hilo baada tu ya kumsikiliza Kikwete..Sikuwa na jibu kwa sababu sijasikia wala sijaona kitu kikifanyika ambacho kinatuandaa sisi watanzania kupambana na hali mbaya ya uchumi duniani..
Na hasa ukisoma Thread ya:- Stimulus Package for Tanzania? A case against -Utaona kwamba ndio kwanza hapa JF tunalijadili na hatuna jibu kwani nchi yetu inahitaji stimulus kila siku ya maisha yake..Hatuna kitu kinachozalisha kiasi kwamba kikianguka tutaanguka kiuchumi kwani tayari miaka kibao nyuma tumekwisha anguka..Uchumi wetu upo ktk recession miaka nenda miaka rudi..
Utajibu nini mkuu ndio maana nikasema Kikwete amejiuma uma kwa sababu hafiria kitu gani kafanya.. hakuona ndani..Hakuna alichofanya zaidi ya U - Vasco Da Gama na kajibu hivyo..
Point being, we have done nothing ktk kujiandaa wala kufikiria kujiandaa, hivyo hakuna jibu hapo na hakuna mtu Tanzania nzima anayeweza kujibu swali ambalo hatuna mkakati wowote dhidi ya hali mbaya ya Kiuchumi duniani labda huyo msanii Mkapa..
 
Mmmmmh inaogopesha....Huyu Muungwana anahitaji Msaada.Inatia aibu kumsikiliza,anakwenda nje kabisa ya swali...Upeo wa kuelewa wa Muungwana ni mdogo mno,inahitajika apigwe msasa kwa masuala mengi!!!
 
...mmmnnnh!? hebu muacheni raisi wetu bana! mijitu kibao humu ina 'mumusa mumusa' na maswali ya hapo kwa papo...

"Describe yourself!" utaanza sikia mtu ...'oooohh, mnnhhh, yuuu know mee!... itakuwa JK na maswali ya counter recession na deflationary spirals?

Give him a break!!!
 
P53,
hapana mkuu sikukuweka nafasi moja na JK hata kidogo isipokuwa nilidhani mwenzangu unalo jibu zuri kuliko la JK..
Mkuu, hata mimi nimejiuliza swali hilo baada tu ya kumsikiliza Kikwete..Sikuwa na jibu kwa sababu sijasikia wala sijaona kitu kikifanyika ambacho kinatuandaa sisi watanzania kupambana na hali mbaya ya uchumi duniani..
Na hasa ukisoma Thread ya:- Stimulus Package for Tanzania? A case against -Utaona kwamba ndio kwanza hapa JF tunalijadili na hatuna jibu kwani nchi yetu inahitaji stimulus kila siku ya maisha yake..Hatuna kitu kinachozalisha kiasi kwamba kikianguka tutaanguka kiuchumi kwani tayari tumekwisha anguka..
Utajibu nini mkuu ndio maana nikasema Kikwete amejiuma uma kwa sababu hafiria kitu gani kafanya.. hakuona ndani..Hakuna alichofanya zaidi ya U - Vasco Da Gama na kajibu hivyo..
Point being, we have done nothing ktk kujiandaa wala kufikiria kujiandaa, hivyo hakuna jibu hapo na hakuna mtu Tanzania nzima anayeweza kujibu swali ambalo hatuna mkakati wowote dhidi ya hali mbaya ya Kiuchumi duniani labda huyo msanii Mkapa..


Mkuu Mkandara nakuelewa.Sawa tuseme swali ni jipya masikioni mwa Mr.President,swali ni jipya masikioni mwetu watanzania.Lakini hoja iko palepale kwamba walau Mr.President angejenga argument nzuri ambayo ingemfanya aonekane yuko conscious of what is going on around the global now.Yeye ni mchumi;ameshindwa kutafuta vi terms vya uchumi kidogo vya kuzugia kwa mfano angesema tumepunguza matumizi yasiyo ya lazima kama serikali au tuna mpango wa kujikita kwenye kilimo zaidi ili tuongeze ajira kwa watu wetu yaani ku spin tu kwa jambo lolote ambalo serikali yake imefanya mpaka sasa ili aondokane na aibu ya kushindwa kujibu swali.
Vitu kama hivi ndivyo vinavyowafanya wakenya watucheke!!
 
P53,
Mkuu atatafuta vi term wapi wakati swali limekuja akiwa mezani?..Wala hili sio swala la usomi kuelewa swali bali ni kuelewa kinachotokea sasa hivi kina madhara gani Afrika na wewe umejiandaa vipi na hali hiyo sio kujiandaa na swali au lugha..Jk hakujiandaa kabisa na hakuna nchi hata moja Afrika imejiandaa na hali mbaya ya Uchumi dunani zaidi ya kuomba Mungu..

Hata huyo mzungu wa South hakujibu kitu kaulizwa South mnafanya nini ktk kujiandaa na hali hii ya Uchumi alichojibu ni mambo yanayotokea hivi sasa sijui ajira kupotea ktk migodi.. Umefanya nini - hana Jibu, ohh tutahakikisha kazi haziporomoki.. How? sikusikia jibu..hata kama alikuwa ametulia alipokuwa akijibu.. kwangu mimi hata huyo mzungu ni zuga tu msanii mwingine..

Mkuu kama nchi haijapata nafuu ktk gonjwa hili la Kiuchumi hata siku moja unafikiria tutafanya nini au tumefanya nini dhidi ya kirusi ambavyo kwanza hatuhfahamu zinatokana na kitu gani!!.. JK hadi leo hii hafahamu hata kwa nini Tanzania ni maskini, iweje afahamu tunaweza vipi kujiandaa na hali mbaya ya Uchumi dunania wakati yeye ndio yupo katikati ya matatizo!

Ni sawa na mgonjwa wa Ukimwi tena maskini ukamuulize anafanya nini kuhusiana na KINGA ya Ukimwi wakati huyu mgonjwa anategemea dawa toka Ulaya..sanasana kutumia Kondom na hata hiyo matumizi ya kondom hadi mzungu aseme..Huu ndio Uchumi wetu miaka yote ni maskini tunaosubiri Kufa hivyo uchumi wetu unakwenda kwa vidonge toka Ulaya kuongeza muda wetu wa maisha!..
Ndicho kilichotupeleka mkutanoni..kuomba msaada - hakuna mtu aliyekwenda pale izaidi ya kuomba msaada toka IMF, Uchumi wa nchi zetu upo ktk recession toka tupate Uhuru..Sasa wakiharibikiwa hao ambao nbdio watunzi wa elimu nzima ya Uchumi unafikiri Kikwete atajibu kitu gani.. sikuona mtu hata mmoja aliyejibu swali, labda kwa sababu sikusikiliza watu wote....i
 
sasa mlitaka anyamaze au aongee porojo zile zile alizozugia za maisha bora, wakat akihangaika kutafuta hiyo nafasi ya kupena mikono na mabos wa G.8 duniani?
 
Kwenye mark ya dakika 83-84 mbunge wangu John Momose Cheyo naye kajitutumia na kuuliza swali.....eheheheheheeeee
 
hata neno moja la mahana
jibu
kila siku watu wanapewa misamaha ya kodi basi ameshindwa kusema, come on mr president
"tax incentive" investors wanapewa msahama wa kodi ili kuwavutiwa

nilimuona ben mkapa hapa uk kwenye question time alijibu maswali mpaka tukampenda...
 
Semilong,
Kuna msamaha gani unatolewa leo hii kwa sababu ya hali mbaya ya Uchumi duniani..Mkuu JK has done nothing na hakuna haja ya kufanya kitu ikiwa tunasubiri mzungu atueleze jinsi..ndivyo tulivyofundishwa...
Mkuu utaweka tax incentive kama hawa wawekezaji wanazalisha, lakini kinachofanyika tanzania ni sokoni yaani hao wawekezaji wanakuja kuuza kile kilichotengenezwa Ulaya ambacho soko lake linashuka..Sana sana tunawasaidia wao uchumi wao ukuwe na ndio maana wamesisitiza sisi tufungue zaidi milango yetu wapate kuja wekeza..Hatuzalishi kitu na hatuna Miundombinu ya kutuwezesha kuzalisha..
Alichosema Ben UK ni kufurahisha baraza tu..kila alichosema ni kulingana na microeconomy inavyotakiwa..lakini kama ukimuuliza kesho ulifanya nini hana jibu zaidi ya kuzungumzia makusanyo ya tax ambayo hadi leo hii ni swala la makadirio..
 
tatizo sio kiingereza tatizo kikwete ni kihiyo kwa ajili kiingerza anachoongea ni kizuri kabisa bila matatizo yoyote
 
swali langu bado halijajibiwa
ni wapi JK aliwekwa kitimoto akatoka na majibu mazuri?manake hii ingekuwa kaanza leo tungesema aah swali gumu aahh kama kawaida yetu wabongo visingizio kibaao.sasa anayejua aseme ni wapi alimuona JK akipigwa maswali ya papo kwa papo halafu akajibu kiufasaha kabisa kama mtu mwenye kuelewa alichoulizwa?
 
p53,
Mkuu hakuna mahala JK kaweza kujibu swali vizuri hilo wazi...pengine domo zito kama mimi hapa Mkandara.. utacheka nikihojiwa..Lakini ktk swali alopewa hapo mkutanoni mkuu wangu ni aibu kwa Utawala mzima wa Tanzania na nchi za Kiafrika.. na kushindwa kwake kujibu haina maana kulikuwepo na jibu zuri kuwa nchi yetu imejiandaa hivi ama vile ktk kukabiri hali mbaya ya Uchumi duniani tena basi unakapo ulizwa MMEFANYA NINI?..Hapa huhitaji ujuzi wa lugha au elimu au Ujanja wa mjini ikiwa hujafanya kitu wala hukufikiria kufanya kitu..
Ndio maana nasema hakuna solution isipokuwa kuwaondoa CCM, hakuna haja ya kumnyooshea kidole JK wakati the all basket ni Uozo!..nilichojifunza mimi toka mkutano huo ni jinsi sisi tusivyofahamu tunakotoka wala tunakokusudia kwenda!..
 
Mmmh jamani Prezidaa ni mweupe kabisa. Jamani mbona maswali yenyewe yanawezwa hata kujibiwa na diwaniambaye atakuwa amekumbwa na msukosuko wa uchumi??????????? God this is so embarassing, yeah is the Prezidaa but mmmmh.
 
--------------------------------------------------------------------------------

Huyu mkku inaonekana hana idea ya kinachoendelea duniani au, hayupo in touch with reality......
__________________


YUKO BUSY NA EPA JAMANI MSAMEHENI!!!MMH LAKINI JAKAYA UNATUANGUSHA
 
Lord have mercy kwa hawa viongozi watu!!!!!!!!!!!!!!ni aibu tena kubwa kwa kiongozi wa nchi kushindwa kujua uchumi wa dunia upo kwenye ncha ya sindano kila mtu anazungumzia uchumi imekuwa wimbo hata siafu wanaelewa hilo.Viongozi wa bongo evening classes zipo available rudini shule kubrush hata language tu mnatutia aibu mweeh!!!!
 
Lord have mercy kwa hawa viongozi watu!!!!!!!!!!!!!!ni aibu tena kubwa kwa kiongozi wa nchi kushindwa kujua uchumi wa dunia upo kwenye ncha ya sindano kila mtu anazungumzia uchumi imekuwa wimbo hata siafu wanaelewa hilo.Viongozi wa bongo evening classes zipo available rudini shule kubrush hata language tu mnatutia aibu mweeh!!!!

Wewe je? Uko vizuri kwenye lugha? Hoja yangu hapa ni kila mtu anatakiwa kujitahidi kuwasiliana kwa uhakika. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kushindana kwenye soko la ajira na kupunguza mikanganyiko kwenye jamii. Sidhani kama Bw. Kikwete ana tatizo la lugha. Tatizo ni kwamba hakuwa na majibu ya maswali aliyoulizwa. Remember, he is not a native speaker of english and he's that much good. What else do you want from a non-native speaker of english? And I think the debate focused more on issues rather than mastery of the language. And who can claim to be good in language anyway?

I think it's more valuable to orient yourself to the key deliberations of the meeting rather than wasting your time addressing petty issues.
 
Back
Top Bottom