Is It Possible For a man & woman To be just Friends and Not Lovers for Appr. 5 years?

Iselamagazi

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,920
6,007
Hi! wana JF!

Hivi kuna uwezekano wa mwanaume na mwanamke kuwa ktk uhusiano wa kawaida kabisa kama marafiki tu bila kuwa wapenzi?
Kuna mkasa mmoja ambao naufahamu wa mwanaume na mwanamke ambao waliishi ktk ndoa kama mume na mke kwa takribani miaka 12 na baadae kulitokea kutoelewana kwa wana ndoa hawa na kupelekea kutalikiana kwa miaka mitano (5) sasa!


Wawili hawa nafanya nao kazi ktk ofisi mmoja. Kitu cha ajabu ni kuwa wana ushirikiano mzuri sana ktk masuala ya kazi na huwezi kujua kama kuna tofauti za kuachana kama tulivyo zoea ktk jamii zetu kuwa bibi na bwana wakishatengana ni nadra sana kukuta jambo kama hili. Si ofisini tu, ushikiano wao upo hata katika masuala ya kijamii mathalani, utawakuta wakiwa pamoja ktk misiba, harusi n.k.

Kurizuka rumours pale kibaruani kwetu kuwa hawa wawili wana kula mshedede kwa siri sana! Jamaa mmoja pale kibaruani alishawahi kumtania yule bwana mtalaka kuwa bado wanaendeleza kale kamchezo; yule bwana mtalaka alikataa kata kata kwamba yeye na mtalaka wake wamebaki kuwa marafiki tu wa kawaida na kwenye masuala ya kale kamchezo kila mtu kivyake na kwamba kama ana wasiwasi afanye uchunguzi anaojua yeye. Ilikuja thibitika baadaye kuwa ni kweli wawili hawa wamebaki kuwa marafiki tu.

Is it entirely possible for a man and woman to be friends and not be romantically interested for some reason?

 
Mkuu, kwa mujibu wa maelezo uliyotoa, inawezekana..
 
Naweza mkuu, na ninao marafiki wadada. Tena mmoja aliwahi kunipiga kibuti kabla hatujawa marafiki..
 
It is very possible and i enjoy being with my bestfrnd ambae ni mwanaume. Cha muhimu mjue lengo/mipaka ya urafiki wenu.once you knw that the bond becomes strong .
 
Inawezekana kabisa. Mi nnaye mmoja, mkenya, tangu mwaka 2000. Japo nia yangu ya mwanzo ilikua tofauti alipoona dalili akaniambia "tuwe friends tu hicho unachotafuta hutakipata" nikaheshimu tukawa marafiki tu. Mara moja ashaniokoa kuingia mkenge kwa msichana mmoja kabla sijaoa. Isipokua urafiki na wife wangu hataki japo wanafahamiana
 
Inawezekana kabisa. Mi nnaye mmoja, mkenya, tangu mwaka 2000. Japo nia yangu ya mwanzo ilikua tofauti alipoona dalili akaniambia "tuwe friends tu hicho unachotafuta hutakipata" nikaheshimu tukawa marafiki tu. Mara moja ashaniokoa kuingia mkenge kwa msichana mmoja kabla sijaoa. Isipokua urafiki na wife wangu hataki japo wanafahamiana

Siku akikuambia mfanyane utakataa?
 
Back
Top Bottom