Is it Ethical to monitor your spouse?

Kumspy mwenzio ni abuse ya kimahusiano unatakiwa umwamini naye akuamini,mambo ya kuchunguzana kuanza kucheki mikoba au mifuko ya suruari,briefcase,hii yote ni aina ya unyanyasaji,mtu anapaswa awe huru,kama ni mwaminifu atakuwa mwaminifu tuu na kama sio anafanya kwa siri hakuonyeshi atakuwa amekupunguzia presha.
Maswala ya kupekuana yanaleta viugomvi visivyo na sababu we fikiri kila siku kuwe na maswali hii simu ya nani ,nani huyu umemuandikia message,hii picha ya nani na hihi na hivi ,spying a patner is unethical
 
...ndio yale yale eti unamchunga sana mumeo ilhali nyumbani umemuacha na hausigeli... au umemuwekea ulinzi wa kumtosha mkeo, na hata kazi umemuachisha na kila anapokwenda dereva anampeleka... utasaidiwa 'naye' tu!

Ku cheat ni tabia ya mtu bana, 'Kunguru' hafugiki!
 
Duh inawezekana kweli? Hebu tupeni mbinu basi ya kuishi na mtu ambaye ana dalili za kutokuwa mwaminifu wengine tuna roho ndogo kweli kitu kidogo tu tunataka tukijue na usipokijua mood yote inaharibika na stimu zinakata hadi unashindwa hata kuzungusha kiuno!!

How to ignore? mimi nimekaa kimya hadi nahisi kuchoka sasa, the presha within me inakaribia kuburst
 
Kumspy mwenzio ni abuse ya kimahusiano unatakiwa umwamini naye akuamini,mambo ya kuchunguzana kuanza kucheki mikoba au mifuko ya suruari,briefcase,hii yote ni aina ya unyanyasaji,mtu anapaswa awe huru,kama ni mwaminifu atakuwa mwaminifu tuu na kama sio anafanya kwa siri hakuonyeshi atakuwa amekupunguzia presha.
Maswala ya kupekuana yanaleta viugomvi visivyo na sababu we fikiri kila siku kuwe na maswali hii simu ya nani ,nani huyu umemuandikia message,hii picha ya nani na hihi na hivi ,spying a patner is unethical

Froida aksante kwa angalizo.

Ni kweli wengi hapa tumehisi kuwa kufanya hivi ni unethical ni kweli kwa sababu in theory mwenza wako anatakiwa aheshimiwe, umtrust na kumwamini katika yote na kuanza kumfikiria maovu na kumshuku ni kumkosea sana. Lakini pia yeye ili atrustiwe ni lazima awe mwaminifu na aliye honesty. Vitu ambavyo in reality, katika maisha ya sasa kwa kweli ni wachache sana wenye sifa hizo. So ni kama kukalia bomu ukingoja likupasukie kisa unaogopa kulichungua wakati ile tickling clock unaisikia kila kukicha!

And I am telling you kuwa some people takes for granted hiyo trust anayokuwa amepewa. Anajua kwa kuwa natrustiwa, sichunguzwi basi s/he will never know kua am cheating so let me cheat kwa kwenda mbele.

Sasa bora ni lipi kuishi na mtu unayemfahamu fika kuwa ni cheater au kuishi na mtu ambaye hujui kama ni cheater but anakucheat?

Hebu tungeweza kupata shuhuda za wale wajane waliofiwa na waume zaio wapendwa waliotokea kuwaamini sana only to find out kuwa they have watoto wa nje siku ya msiba wa mume, nafikiri ingetusaidia sana kujua.
 
Nini mtazamo wako katika hili?

MJ1,

Naona umetumia maneno matatu (ku-spy, ku-monitor, na Kuchunguza (investigate?)) ambayo kimsingi yanaweza kuwa na majibu tofauti.

Ku-spy ni kuiba au kupata taarifa fulani kwa siri (mara nyingi taarifa kutoka kwa adui yako). Kwa msingi huu, sioni sababu ya kum-spy mwenza wako. It is really unethical especially kama hakuna enemity kwenye hiyo relationship. Ni matumizi mabaya ya preveleges zinazopatikana kwenye ndoa.

Ku-investigate (kuchunguza), hapa lengo ni kupata taarifa zaidi (details)juu ya jambo fulani mahususi ili kujua ukweli. Hii halihitaji kufanywa kwa siri. Inaweza pia kujumuisha mahojiano na muhusika. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi juu ya jambo fulani kabla ya kulifanyia maamuzi iwe ni katika ndoa ama katika mahusiano ya kawaida.

Ku-monitor, hapa unaangalia kama reality ina conform na expectations zako au makubaliano katika muda fulani kwa lengo la kurekebisha kama kuna unacceptable/intolerable deviations. Mara nyingi katika mahusiano 'monitoring' inatokea unconsciously (ingawa hata consciously kama kuna kitu maalumu mmekubaliana - kwa mfano kuacha pombe, sigara etc) na binafsi sioni kama ni mbaya.

Investigation inaweza kuanza kutokana na matokeo (feedback) ya monitoring. Kama kwa mfano expectations zako ni kuwa mume awe nyumbani by saa mbili usiku. Unconsciously, utakuwa unamonitor muda anaourudi,na endapo ataanza kuchelewa kurudi, tayari utapata feedback kuwa sasa anarudi baada ya saa mbili. Kama hili ni tatizo kwako unaweza anzisha uchunguzi wa kwa nini anachelewa kurudi. Uchunguzi unaweza kuwa kumuuliza tu kwa nini anarudi muda tofauti na zamani na unakwenda mbele kujaribu kuverify sababu atakazozitoa. Hili hulifanyi kwa siri ni lazima umwambie kutoridhika kwako na muda anaorudi pamoja na sababu anazozitoa.

Labda nimalizie kwa kusema kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka iwe ni katika ndoa ama kwengineko.
 
Last edited:
Wajameni wa jamvi hili la mapenzi na mazaga zaga yake leo kichwa changu hakifanyi kazi kwa hiyo nahofia kuchangia mada hii...nimeconcentrate kule kwa Mwakalinga kwenye siasa mule....siku 3 hizi hakuna kulala....:confused:
 
Sio ethical hata kidogo, kwani wakati mnakutana mara ya kwanza mpaka kuoana si kwamba ulimuamini?
 
spying is a hobby------kama upo kwenye ndoa unaweza kujua hili..........pia ni outcome ya fununu..kama amesiakia sikia au ameshawahi kukukamata kweupe bila ku-spy, then ataanza kuspy.............all in all is kama unataka kuendelea kuwa kwenye ndoa, bora kutofanya hivyo, kwani utakuwa hurt tuu basi, lakini kama unataka kutoka,,,,,,,endeleeeaaaa!!1
 
Haya mambo ya kuchunguzana yana ugumu wake. Ukiwa na wivu kiasi hicho hata kazi utashindwa kufanya inabidi kuaminiana tu, lakini hebu oneni haya ya wenzetu.

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=LEbkRLBoXOg&feature=PlayList&p=F045B8EABCD1D9A3&index=0&playnext=1"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=0uBhTcqXD8M&feature=PlayList&p=F045B8EABCD1D9A3&index=1&playnext=2&playnext_from=PL"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=TZtgqMvRC0k&feature=PlayList&p=F045B8EABCD1D9A3&index=2&playnext=3&playnext_from=PL"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=GkJKF2bg3xg&feature=PlayList&p=F045B8EABCD1D9A3&index=9"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
Last edited:
Utajiumiza mwenyewe kwa kumchunguza mwenza wako....yaani hapo kifo unakivuta ya nini.... ngoja nitarudi kuwapa real life experience
 
Kueni muache utoto, kwani wewe ndio wa kwanza kushiriki tendo la ndoa naye? aliyemwanza na waliokutangulia si wapo, je, wakitaka kukumbushia? anyway, kuchunguzana sio salama, acha mtu ajichunge mwenyewe, ukimfuatilia utaona uozo mwingi sana na ndani hakutakaklika
 
Ikiwa sababu ya kuacha kumchunguza mtu ni kuogopa kuuona uozo na hivyo unaamua kuishi kama vile uozo haupo unajidanganya. Unajua tunapokumbwa na masahibu wengine hukataa kuwa hayapo na hivyo kuishi katika utopia. Je mnataka tuishi katika utopia?

Ukiwa na sababu yoyote ya kufanya uchunguzi ni vizuri uufanye kwa siri na kwa wazi. Kwa nini? Hutaki kuishi na mtu mwovu ukiwa wewe si mwovu. Kwa mfano, lazima ujuue mwenzio hizo pesa mnazotumia anazipataje! Ndiyo. Kwa nini? Inawezekana ni jambazi na siku moja utaswekwa naye ndani kwa kuficha mwizi.

Mapenzi ni kitu mbovu. Watu wanafanya vitu vyao nje ovyo ovyo na hawako comfortable wenzi wao wakijua uchafu wao. Wanaishi katika utopia. Kukataa tabia zao. Ikiwa wewe ni muhuni utakuwa worried sana kama utachunguzwa. Ukiwa mwaminifu na transparent, utafurahia ukichunguzwa kwani unajua uchunguzi huo uta reveal jinsi ulivyo mwaminifu.

Lakini ukiwa mchafu, huwezi kuvumilia kuchunguzwa. Utakuwa mkali kweli na utalilia privacy. give me a break. Hakuna privacy kwenye ndoa. Ni privacy gani unayotaka mwenzio asijue? Akiwa na sababu ya kukuchunguza manake kuna kitu kastukia. Mwache achunguze openly na kwa siri.

Sasa unaposema eti ukimchunguza unajitia presha manake nini? Uishi na mwongo tena mnafiki anayekudanganya kwa sababu unaogopa ukijua kuwa ni mwongo roho itakuuma?? Are we for real au tunabwabwaja tu!!!

Yaani uko happy kuishi na mwizi provided hujui kuwa ni mwizi, really. Na hayo madhara ya wizi utayakwepaje? Uko tayari kuishi na changu, provided hujui kuwa ni changu. Na hiyo ngoma utaiepukaje? Please, mchunguze mwenzio hadharani na sirini. Tena kila siku. Kuna uchafu mwingi unaweza kuepukika tu ukistukia mwenzio anaweza kujua na kuna mengi unaweza kuepusha. Ila ikiwa hujali chochote, mtu kama mimi ni kila sababu ya kutilia mashaka uhusiano wetu.

Mimi nitamchunguza tu, apende asipende. Nilishafanya hivyo, nikasambaratisha uhusiano uliokuwa umeshaanza kuchipuka. Uhusiano mbovu. Ambao hatima yake ingekuwa balaa, si kwa ndoa tu bali kwa sisi wenyewe binafsi kama individuals.

Whatever happens kwenye mahusiano kina kuathiri moja kwa moja. Kuchunguzana ni kuwa makini na maisha yenu. Kama hamchunguzani, mnaweza kuwa hamna chochote in common. Kwa nini basi muishi pamoja? Tusijidanganye.
 
Ukivaa nguo chafu, hata kama ukijipulizia pafyum kuna watu watajua kuwa wewe mchafu. Ukiishi na mwongo, hata kama hutaki kuujua uongo wake, madhara ya uongo huo hutayakwepa. Mchunguze kila fursa inapopatikana. Mchunguze hasa, kila wakati uwe na uhakika unaishi na mtu unayetaka kuishi naye.

Kuishi na mwenzi mwongo si jambo la kutia presha tu, na jambo linaloweza kukuua. it is about your life.

Unayo haki ya kuishi na mtu uliyemchagua kwa sifa ulizomchagua. Ikiwa uongo ni mojawapo ya sifa unazozikubali, go ahead acha kuchunguza.

Binadam hubadilika. Kuna maovu mengi hufanyika kwa sababu opportunity ya kufanyika ipo. Ikiwa opportunity hiyo inazuiwa, makosa hayo yangeweza kuepukika.

Kuchunguza huondoa huo uwezekano. Lakini kuchunguza kunakusaidia kujua afya ya mahusiano yenu.

Kumbuka kujua si tatizo. Tatizo ni kile utakachofanya baada ya kujua. Lakini hata usipojua madhara bado yako pale pale, unaweza kuyachelewesha tu.

Ikiwa mwenzio ana nyumba ndogo we unasema simchunguzi. sawa madhara ya yeye kuwa na nyumba ndogo utayakwepa??
 
If you are not going to have the peace of mind and trust in your marriage, why marry in the first place?
 
...Mimi nitamchunguza tu, apende asipende. Nilishafanya hivyo, nikasambaratisha uhusiano uliokuwa umeshaanza kuchipuka. Uhusiano mbovu. Ambao hatima yake ingekuwa balaa, si kwa ndoa tu bali kwa sisi wenyewe binafsi kama individuals...

...duh, pole sana....

...Whatever happens kwenye mahusiano kina kuathiri moja kwa moja. Kuchunguzana ni kuwa makini na maisha yenu. Kama hamchunguzani, mnaweza kuwa hamna chochote in common. Kwa nini basi muishi pamoja? Tusijidanganye.

...ushawahi kusikia -once a cheater always a cheater-?
Huko unakosema wewe si kumchunguza, bali 'kujaribu' kumlinda/kumchunga!.
kumbuka tu, 'kunguru hafugiki'
 
Back
Top Bottom