Is CCM in shinyanga region dying softly

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Mkoa wote wa Shinyanga CCM ilishakufa na kama haijafa kabisa basi iko mbioni. Kilichobaki ni viongozi kupiga majungu. Chama mkoani kimegawanyika katika makundi makuu mawili, Magamba aka fisadi na kundi jingine "wavua magamba" aka mzee wa "kasi na viwango" Mwenyekiti na baadhi ya jumuiya za chama mkoani na sekretarieti zake wako upande wa magamba ndiyo maana pamoja na Maige kutoa kauli yake mbele ya Mwenyekiti wa mkoa, Body language ya Mwenyekiti wa mkoa ilionyesha kama anakubaliana na tuhuma hizi. Kama mtakumbuka, kuna kauli nyingi tu ambazo Mwenyekiti wa mkoa aliishazitoa za kumpinga Nape na kundi lake ("wavua magamba") na kusema utendaji na kauli zake zinaiua CCM.
Mbio za urais zinaitafuna CCM. Viongozi wengi wanatanguliza maslahi yao badala ya maslahi ya chama na wananchi. Kuondolewa uwaziri kwa Ezekiel Maige imeonekana kama ni ushindi katika ngome ya mzee wa "kasi na viwango" kwa vile inasemakana Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Ardhi, maliasili na Mazingira yuko upande wa mzee wa "kasi na viwango". Yetu ni macho na natumaini katika mwendo huu, tutasikia na kuona mengi.

We don't care, wananchi have other choices to choose. Mwalimu Nyerere alisema CCM siyo mama wala baba. Kwa kufanya hivi, hata vyama vya upinzani havihitaji kufanya kampeni kwa sababu mipasuko yao inasaidia kambi la upinzani hasa chama kikuu cha upinzani katika sakata la mavuno kisiasa.
Ooh my day, is CCM dying softly?.

 
Back
Top Bottom