Iringa kujengwa uwanja wa ndege wa kimataifa?

Nimesikia kuwa maelfu ya wakazi wa vijiji vya Nduli na Igingilanyi watahamishwa ili kupisha ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa. Uhamishaji huu utahusu kulipa fidia makazi, mashamba na kuhamisha makaburi. Mamia ya nyumba za makazi, shule, misikiti na makanisa yanatarajiwa kuvunjwa. Nimepata shida kuamini habari hizi kwani uwanja uliopo ambao ni wa lami unaonekana kukidhi mahitaji ya ndege zinazotua hasa ikizingatia kuwa miundombinu ya barabara imeboreshwa na hasa baada ya kujengwa kwa barabara za lami zinazouunganisha mkoa huu na mikoa mingine kama hii inayomalizika kujengwa sasa ya Iringa - Dodoma.

Hizo ndege kubwa ni za kupanda nani? Ni za kusafirisha mazao? Au za kupakia wanyama kutoka mbuga ya Ruaha? HIzi habari ni za kweli? Mradi huu upo katika ilani ya CCM au watu wanataka kutimuliwa kijanja ili waletwe wageni ambao wanaitwa ni wakezaji? Sasa Dodoma ndio mji mkuu hakujengwi uwanja mkubwa wa kimataifa badala yake wanataka kujenga Iringa. Je makao makuu yanahamia Iringa? Au Dodoma hakuna nafasi hivyo wakijenga Iringa watakuwa wanatua hapo na kwenda Dodoma na magari? Maswali ni mengi! Zamani watu walikuwa haishi hapo wakalazimishwa kuhamia hapo wakati wa vijiji vya ujamaa sasa tena wanaondolewa sijui watakwenda wapi?

Wewe utakuwa na matatizo ya akili yaani chizi
 
Itakuwa vizuri sana kwa wakazi wa iringa ikiwa uwanja huo utajengwa kwani kuna mbuga ya taifa RUAHA na pia Shughuli za kiuchumi zipo nyingi ni fursa kwa wana IRINGA na taifa zima ki ujumla....
 
Back
Top Bottom