Iringa kujengwa uwanja wa ndege wa kimataifa?

Mantombazane

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
572
356
Nimesikia kuwa maelfu ya wakazi wa vijiji vya Nduli na Igingilanyi watahamishwa ili kupisha ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa. Uhamishaji huu utahusu kulipa fidia makazi, mashamba na kuhamisha makaburi. Mamia ya nyumba za makazi, shule, misikiti na makanisa yanatarajiwa kuvunjwa. Nimepata shida kuamini habari hizi kwani uwanja uliopo ambao ni wa lami unaonekana kukidhi mahitaji ya ndege zinazotua hasa ikizingatia kuwa miundombinu ya barabara imeboreshwa na hasa baada ya kujengwa kwa barabara za lami zinazouunganisha mkoa huu na mikoa mingine kama hii inayomalizika kujengwa sasa ya Iringa - Dodoma.

Hizo ndege kubwa ni za kupanda nani? Ni za kusafirisha mazao? Au za kupakia wanyama kutoka mbuga ya Ruaha? HIzi habari ni za kweli? Mradi huu upo katika ilani ya CCM au watu wanataka kutimuliwa kijanja ili waletwe wageni ambao wanaitwa ni wakezaji? Sasa Dodoma ndio mji mkuu hakujengwi uwanja mkubwa wa kimataifa badala yake wanataka kujenga Iringa. Je makao makuu yanahamia Iringa? Au Dodoma hakuna nafasi hivyo wakijenga Iringa watakuwa wanatua hapo na kwenda Dodoma na magari? Maswali ni mengi! Zamani watu walikuwa haishi hapo wakalazimishwa kuhamia hapo wakati wa vijiji vya ujamaa sasa tena wanaondolewa sijui watakwenda wapi?
 
Wewe sio mzima wewe!
Yani unajipump mwenyewe.
Story utunge wewe, uipambe wewe, uulize maswali ya hayo mapambio wewe, ujijibu tena negatively mwenyewe halafu uombe mchango.
Kweli insanity has many levels.
Kwanza source kuwa uwanja wa KIMATAIFA unajengwa umepata wapi au ndio unauliza hapa? Na kama unauliza kwanini basi uendelee kumake remarks na conclusions kwa kitu usichojua na ni hypothetical.
You must be suffering from a form of hysteria aisee. Hata kama CCM tumeichoka haimaanishi kufanya misuto ya vijiweni na imbecilic (not an actual word) kama hii!
 
Sina uhakika kama ni uwanja wa kimataifa maana sijui standard gani inatakiwa mpaka uwanja uitwe wa kimataifa... Ila ni kweli uwanja wa nduli unajengwa tena kwa ufadhili wa wold bank... Lakini nasikitika kusema kuwa mkandarasi aliyepewa hiyo tenda hana uwezo wa kujenga viwanja vya ndege na hana uzoefu.... Hajawahi kujenga popote na hiyo ndo itakuwa mara yake ya kwanza kufanya hivyo... Tuombe mungu asitoe goko....... Kampuni iliyopewa hiyo tenda ni ya gs construction ya geofrey mungai....
 
EA Feb 04 13 Tanzania and Investors.jpg ....... Kampuni iliyopewa hiyo tenda ni ya gs construction ya geofrey mungai....
As usual corruption at work
 
Sina uhakika kama ni uwanja wa kimataifa maana sijui standard gani inatakiwa mpaka uwanja uitwe wa kimataifa... Ila ni kweli uwanja wa nduli unajengwa tena kwa ufadhili wa wold bank... Lakini nasikitika kusema kuwa mkandarasi aliyepewa hiyo tenda hana uwezo wa kujenga viwanja vya ndege na hana uzoefu.... Hajawahi kujenga popote na hiyo ndo itakuwa mara yake ya kwanza kufanya hivyo... Tuombe mungu asitoe goko....... Kampuni iliyopewa hiyo tenda ni ya gs construction ya geofrey mungai....

Gs is another company and Gephrey Mungai has his own company dont mix up things

Company needs experience in business and construction is just an engineering
 
Uongo mtupu kampuni ya huyo jamaa haiitwi GS construction umechemka? Na swala la kuwa na uzoefu ni kichekesho si kila kitu kina mwanzo? Kama ni mtaalam wa kutengeneza barabara si ilibidi aanze siku moja ndio ili awe mzoefu mumpe na barabara zingine?
Either way sijui kama kampuni ya jamaa imehsafika level hio, waswahili acheni kutunga nakupakiziana tu mambo kijinga. Itafika mda hata mtu akisema ukweli atapuuzwa!
 
ndo tatizo la nyie watanzania... yawezekana ni kweli nimekosea jina lakini nina uhakika asilimia 100 kuwa gefrey mungai ndo kaewa hiyo tenda...... bahati mbaya hatufahamiani lakini fuatilia ndo useme sijui mambo ya kutunga... we unafikiri kila mtu anapenda kuandika uongo kama wewe?
 
Gs is another company and Gephrey Mungai has his own company dont mix up things

Company needs experience in business and construction is just an engineering

nakubaliana na wewe yawezekana nimekosea lakini kampuni iliyopewa tenda ni ya geofrey mungai na nauhakika
 
ndo tatizo la nyie watanzania... yawezekana ni kweli nimekosea jina lakini nina uhakika asilimia 100 kuwa gefrey mungai ndo kaewa hiyo tenda...... bahati mbaya hatufahamiani lakini fuatilia ndo useme sijui mambo ya kutunga... we unafikiri kila mtu anapenda kuandika uongo kama wewe?
Haya bwana kwahio jina la kampuni yake hujui lakini una uhakika asilimia 100 kua kapewa yeye. Kwahio umekosea ila hujadanganya? Unajua kuwa Gs ni kampuni ingine kabisa?
OK. Ila bado hakuna tatizo, kwanza sijawahi kusikia kashfa ya huyu jamaa kwenye ujenzi, halafu namsifu sana unajua hata form 4 hakumaliza ila akaunti inasoma kwenye billions. He is a businessmind.

Anyways nafikiri inatosha, tuone ata perform kwa kiwango gani lakini sio kum crush wakati hakuna evidence ya ulipuaji huko awali.
 
we jamaa bwana.... hapo juu nimekuambia kuwa yawezekana nimekosea jina la kampuni ila nimekuambia ni yeye, wewe bado unaleta habari ya kuwa gs siyo kampuni yake....... pia mi sijasema kuwa anakashfa zozote.... namfahamu na anatenda nyingi mno hasa mkoa wa dodoma sasa hivi kawashika sana.... hofu yangu ilikuwa ni kwamba kwasababu ndo mara yake ya kwanza kwa yeye kujenga uwanja wa ndege sidhani kama utakuwa bora sana.. lakini vinginevyo nampongeza kwa kuthubutu na nawapongeza waliompa tenda mwana iringa mwenzetu kwasababu pesa ile itawanufaisha wengi kuliko angepewa mgeni.... ila tuasifanye ujanja ujanja akatuharibia uwanja wetu
 
Hapa ndugu umechemka usafiri wa Ndege ndio usafiri wa haraka ambao teknolojia imetupa kuweka vikwazo na hoja dhaifu kupinga ujengaji wake ni ujinga.

Nimesikia kuwa maelfu ya wakazi wa vijiji vya Nduli na Igingilanyi watahamishwa ili kupisha ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa. Uhamishaji huu utahusu kulipa fidia makazi, mashamba na kuhamisha makaburi. Mamia ya nyumba za makazi, shule, misikiti na makanisa yanatarajiwa kuvunjwa. Nimepata shida kuamini habari hizi kwani uwanja uliopo ambao ni wa lami unaonekana kukidhi mahitaji ya ndege zinazotua hasa ikizingatia kuwa miundombinu ya barabara imeboreshwa na hasa baada ya kujengwa kwa barabara za lami zinazouunganisha mkoa huu na mikoa mingine kama hii inayomalizika kujengwa sasa ya Iringa - Dodoma.

Hizo ndege kubwa ni za kupanda nani? Ni za kusafirisha mazao? Au za kupakia wanyama kutoka mbuga ya Ruaha? HIzi habari ni za kweli? Mradi huu upo katika ilani ya CCM au watu wanataka kutimuliwa kijanja ili waletwe wageni ambao wanaitwa ni wakezaji? Sasa Dodoma ndio mji mkuu hakujengwi uwanja mkubwa wa kimataifa badala yake wanataka kujenga Iringa. Je makao makuu yanahamia Iringa? Au Dodoma hakuna nafasi hivyo wakijenga Iringa watakuwa wanatua hapo na kwenda Dodoma na magari? Maswali ni mengi! Zamani watu walikuwa haishi hapo wakalazimishwa kuhamia hapo wakati wa vijiji vya ujamaa sasa tena wanaondolewa sijui watakwenda wapi?
 
we jamaa bwana.... hapo juu nimekuambia kuwa yawezekana nimekosea jina la kampuni ila nimekuambia ni yeye, wewe bado unaleta habari ya kuwa gs siyo kampuni yake....... pia mi sijasema kuwa anakashfa zozote.... namfahamu na anatenda nyingi mno hasa mkoa wa dodoma sasa hivi kawashika sana.... hofu yangu ilikuwa ni kwamba kwasababu ndo mara yake ya kwanza kwa yeye kujenga uwanja wa ndege sidhani kama utakuwa bora sana.. lakini vinginevyo nampongeza kwa kuthubutu na nawapongeza waliompa tenda mwana iringa mwenzetu kwasababu pesa ile itawanufaisha wengi kuliko angepewa mgeni.... ila tuasifanye ujanja ujanja akatuharibia uwanja wetu
Sawa nimekuelewa mnyikungu .
Ila kwa ajili ya kujadiliana tu, unafikiri kama mtu asipopewa chance ya kufanya kwa mara ya kwanza itakueje? Yani kama tukilenga kumpa mtu kazi endapo tu ameshawahi kufanya hio kazi sehemu ingine tutafanya lolote kweli.
Sikubishii mkuu, ila naona ni vyema kutoangalia specific experience tu, ila kwa mfano kama mtu kehajenga barabara ya kiwango cha lami vizuri basi hatuna budi kumpa tenda ya uwanja wa ndege.
Kama mtu alimanage dispensary vizuri, ukimpa health center nayo a manage sio kosa. Na wa health centre akachukua hospital.
Sema tu kama ulivyo toa tahadhari tuombe tu rushwa haizidi mpaka ku athiri kiwango cha uwanja!
 
Wewe sio mzima wewe!
Yani unajipump mwenyewe.
Story utunge wewe, uipambe wewe, uulize maswali ya hayo mapambio wewe, ujijibu tena negatively mwenyewe halafu uombe mchango.
Kweli insanity has many levels.
Kwanza source kuwa uwanja wa KIMATAIFA unajengwa umepata wapi au ndio unauliza hapa? Na kama unauliza kwanini basi uendelee kumake remarks na conclusions kwa kitu usichojua na ni hypothetical.
You must be suffering from a form of hysteria aisee. Hata kama CCM tumeichoka haimaanishi kufanya misuto ya vijiweni na imbecilic (not an actual word) kama hii!

Sasa mkuu mbona unakuwa mkali hivyo utadhani nimekwapua pesa za EPA? Hata kama nimekosea si utumie lugha ya kiungwana tena laini? Sasa ukishachanganya na kakiingereza kako hako ndio kuonesha kuwa unakazia lugha kali? Jamani kuweni makini mnapopingana na wenzetu, kuna siku utajikuta unamfokea mkweo bila kujua na wakati ukiwa mbele yake unajifanya mlokole lakini ukija JF wewe ndiye mwenye matusi ya kiingereza na kiswahili. Haya mugoyo, ve winaluhala, nene ndi mupuva. Va Sekanyongo de una bahati naelekea Dodoma kupokea katiba pendekezwa vinginevyo nilisha amua kujitundika kwa jinsi ulivyo nidhalilisha. Kamba nimeihifadhi kusubiri kuombwa radhi vinginevyo nikirudi najiondoa! Swela hela Inguluvi yilukagula!
 
Mantombazane hehehe. Bahati mbaya sijui kihehe! Ningependeje niombe msamaha kwa kihehe! Ila usijitundike be!
 
Last edited by a moderator:
Mantombazane hehehe. Bahati mbaya sijui kihehe! Ningependeje niombe msamaha kwa kihehe! Ila usijitundike be!
Kugaya lukani mugoyo yaani hakuna shida mkuu. Kwa kihehe kusema sorry unasema "Nyongisee!" Na mtoto wa kihehe ukishampa mistari akakwambia "Niangusage, sambi sako mwenyewe" unaererwa? Hamia Iringa, raha tupu. Watu wapole na wakarimu sana
 
Back
Top Bottom