IRINGA: Askari aliyemuua mwanahabari Daudi Mwangosi afungwa miaka 15 Jela

15 ni 15 tu. Kwamba atatumikia nusu ni habari za vijiweni. Jela,siku moja ni siku moja
Kuna watu huku mitaani wanakaririshana ujinga...Kitu watu wanatakiwa wajue Mfungwa akifika Jela kuna kitu wanaita Admission Mwaka wa Jela ni miezi 8 badala ya 12 sasa huku wanaambiana eti....usiku na mchana
 
Heee kuna kijana sijui alikutwa na mirungi Moshi akalambwa miaka sijui 29 ,mimi sheria huwa sizielewi ni kama uchawi fulani hivi ....
 
View attachment 371858 kati ya askari wote hawa kahukumiwa mmoja? Vipi kuhusu aliewatuma?

Eti ndugu inashangaza. Kama inavyoonekana kwenye picha, katika genge lote hilo la askari wanaoonekana dhahiri kuwa na dhamira ya kummaliza kabisa Mwangosi au kumdhuru vibaya amehukumiwa mmoja tu? Tena kwa kuua bila kukusudia? Picha inaonesha kabisa walikusudia. Kimsingi, prosecutors wameharibu hii kesi kwa makusudi. Na kwa misingi hiyo, hawatakata rufaa. Ni nini kinaweza kufanyika bila kuwategemea public prosecutors ili kuhakikisha haki inatendeka? Kwa jinsi hiyo kesi ilivyooendeshwa, hao public prosecutors wanapaswa kushtakiwa pia. Kama kweli Magufuli ana nia ya dhati ya kuona haki za wanyonge hazipotei, aisaidie familia ya Mwangosi na Watanzania kwa ujumla kwa kuitisha upya hii kesi. Aweke mawakili wazuri wa serikali, waianzishe upya hiyo kesi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wote wanaoonekana kwenye picha pamoja na wakubwa wa polisi waliokuwa wanashuhudia tukio wakiwa kwenye gari + aliyeagiza polisi kutoka nje mkoa kwa ajili ya tukio dogo tu la kufungua ofisi ya kijiji wanajibu mashtaka ya kuua kwa kukusudia. Intention ya kuua inaonekana wazi tangu wanaagiza polisi kutoka nje ya mkoa. Pengine polisi wa Iringa walikataa maelekezo ya kuua kwa kuwa walimfahamu Mwangosi. Wakaamua kuchukua polisi wa Dodoma.
 
Mimi sijaridhika kwa kweli ningekuwa mwanasheria ningekataa rufaa, hasa kwa kipindi hiki alicho chini ya magereza, kipindi ambacho wanaozuia asipigwe picha na kuandikwa habari zake hawako naye tena
 
Ilifaa ahukumiwe adhabu ya kifo anyongwe mpaka kufa.
Ilishapangwa hii sinema pale tu aliposhtakiwa kwa kuuwa bila kukusudia hii ni Man Slaughter haina adhabu ya kifo, hata yule Lulu wa Kanumba pia walimpa Man Slaughter ila sijui kesi yake imeishia wapi! Na hata Ditopile alipewa Man Slaughter pia.

Ukisikia mtu amepewa Man slaughter hata mahakama ikija kumuachia huru wala usishangae kabisa.
 
Back
Top Bottom