IRINGA: Askari aliyemuua mwanahabari Daudi Mwangosi afungwa miaka 15 Jela

IMG_0168.JPG
kati ya askari wote hawa kahukumiwa mmoja? Vipi kuhusu aliewatuma?
 
Haki itaonekana imetendeka kakamilifu pale makamanda wa polisi walioamuru hayo mauaji yafanyike watakapoletwa mbele ya sheria.
Mimi ni mmoja wapo aliyesikitishwa mno na kifo cha Mwangosi sana.Ila piani muhimu kuwa wakweli. As he was alive after just one second akawa amefariki so sad kwa wazazi, kwa mke, watoto, na familia yake kwa ujumla. Tuseme ukweli hamna hata mmoja anayemzungumzia kamanda anayeonekana pichani akiwazuia polisi wengine wasimpige let alone kumuua. Hivyo haiingii akilini kusema kuwa kuna makamamnda waliamrisha auawe. Ni sababu gani sijui ya kufikiria kuwa kuna watu waliotuma auawe. Marehemu Mwangosi alikuwa humble sijui kosa gani lingefanya mtu aseme auawe. Ni uzembe mkubwa sana na kitu kibaya sana alichofanya yule askari ambaye anaonekana alijiamulia tu mwenyewe na siamini kabisa kama alitumwa na mtu. R.I.P Mwangosi na polisi wahakikishe jambo hili halijirudii kwani hamna kitu kibaya kama kutoa roho ya mtu tena alikuwa heless na wala haikutakiwa nguvu kubwa kiasi kile katika kumdhubiti.
 
Hukumu kwa Askari aliyekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Mwandishi Mwangosi ni leo tarehe 27/7/2016.

Hukumu hiyo ambayo hasa itahusu adhabu anayostahili Askari husika itasomwa na Jaji Kihwelo wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa.

========= Updates ========

MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa leo imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27) aliyemuua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi wa kituo cha Chanel Ten.

View attachment 371781
Loo! Ndugu zake wakate rufaa. Huu ni utani. Mbona yeye tu? Waliotoa mari vipi?
 
Wanaojiita watetezi na wanaharakati wa haki za binaadamu wajitokeze kuikatia rufaa hukumu hii, Tujifunze kwa hukumu ya kesi ya Oscar Pistorius na sio harakati kila siku kuzielekeza sehemu moja ya politics....

R.I.P Daud Mwangosi
 
Hukumu kwa Askari aliyekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Mwandishi Mwangosi ni leo tarehe 27/7/2016.

Hukumu hiyo ambayo hasa itahusu adhabu anayostahili Askari husika itasomwa na Jaji Kihwelo wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa.

========= Updates ========

MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa leo imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27) aliyemuua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi wa kituo cha Chanel Ten.

View attachment 371781
Mbona kweny tukio wapo weng kwann atajwe mmoja?
 
Mimi ni mmoja wapo aliyesikitishwa mno na kifo cha Mwangosi sana.Ila piani muhimu kuwa wakweli. As he was alive after just one second akawa amefariki so sad kwa wazazi, kwa mke, watoto, na familia yake kwa ujumla. Tuseme ukweli hamna hata mmoja anayemzungumzia kamanda anayeonekana pichani akiwazuia polisi wengine wasimpige let alone kumuua. Hivyo haiingii akilini kusema kuwa kuna makamamnda waliamrisha auawe. Ni sababu gani sijui ya kufikiria kuwa kuna watu waliotuma auawe. Marehemu Mwangosi alikuwa humble sijui kosa gani lingefanya mtu aseme auawe. Ni uzembe mkubwa sana na kitu kibaya sana alichofanya yule askari ambaye anaonekana alijiamulia tu mwenyewe na siamini kabisa kama alitumwa na mtu. R.I.P Mwangosi na polisi wahakikishe jambo hili halijirudii kwani hamna kitu kibaya kama kutoa roho ya mtu tena alikuwa heless na wala haikutakiwa nguvu kubwa kiasi kile katika kumdhubiti.

Hebu nioneshe hapo pichani nani anaemkataza huyo muuaji kumuua mwangosi
 
Hakika huu ni utani, kwanza ilipinduliwa toka mauaji ya kukusudia mpaka mauaji ya bila kukusudia. Ni bora wangemuachia huru tu huyo askari ili nyoyo za wale waliomtuma zizidi kufurahi.
Kwanza mi nashangaa hii kesi miaka yote hiyo duuuu!!!
 
Miaka 15? hapo ramani ya maisha yake na yeye imeshapotea. Ni vyema watumishi wa umma mkajifunza kufanya kazi na kujihurumia ninyi na familia zenu msidhani mtakua watumishi for good

Ni faraja kidogo kwa Familia ya marehemu kuona haki imetendeka,japo inaonekana ni adhabu ndogo lakini itakua fundisho kwa hawa wengine wanaonyanyasa Raia kila kukicha kwa amri ambazo wanapokea sijui kutoka wapi....

Hatimae haki imetendeka, miaka 15 si haba. Shukrani sana mitandao ya kijamii, mashirika ya haki za binadamu kwa kulipigia kelele hili suala.
Wengi bado hamuelewi ni kwa nini Mrema kapewa bodi ya Parole licha ya kukosa sifa ya kijaji, soon mtaelewa sisemi mengi.
 
adhabu ni ndogo sana, angefungwa maisha au kunyongwa kabisa kwa sababu umeua mtu tegemezi ktka familia alafu wewe unaomba mahakama ikuhurumie kisa unasomesha.
 
Haki itaonekana imetendeka kakamilifu pale makamanda wa polisi walioamuru hayo mauaji yafanyike watakapoletwa mbele ya sheria.

Na hilo haliwezekeni kwenye huu mfumo tulionao wa chama kimoja mpaka tutakapo kubali kwa dhati mfumo wa vyama vingi.
 
Tunasema kila siku.. Kazi ya polisi si kupiga raia. Kama kuna mtu anawafundisha polisi wetu mafunzo ya kupiga raia wasio na hatia, huyo ndiye anapaswa kufungwa miaka 15. Kazi ya polisi duniani kote ni kulinda usalama wa raia. Huwezi kulinda usalama wa raia kwa kuwapiga na kuwaumiza au kuwaua. Polisi wana wajibu wa kumkamata mtu na kumfikisha katika vyombo vinavyohusika kama wanaona ana makosa. Wanasiasa wetu wanapaswa kuwa waangalifu sana na matendo ya kulichochea jeshi letu la polisi kupiga na kuumiza raia katika matukio ya kidemokrasia kama maandamano ya amani. I really sympathize na huyu askali. Si kosa lake, ni mhanga wa kupokea amri mbovu zinazotokana na mashinikizo ya wana siasa. Huwezi kumpiga na kumuua raia kisa tu amekaidi amri ya polisi ya kutofanya mkutano, au ameandamana bila kibali....! (Hata Mungu hawapi adhabu ya kifo wanaokaidi amri zake), kama ingekuwa rahisi kutoa hukumu za namna hiyo, basi kwa kosa la kumwua Mwangosi, askali huyu angepewa adhabu gani???
 
Back
Top Bottom