Iran to 'hit Tel Aviv' if attacked

Viongozi wote waliowekwa na Bush Huko Iraki ni MASHIA AMBAO NDIO IRAN!

Na wakati wanafanya plans za kuivamia Iraki..walikuwa wamejificha Iran na wakisaidiwa na Muiran pamoja na BUSH!

Sasa wamechukuwa madaraka...Na kuna mmoja wao(Ambaye ndiye alikuwa apewe urais wa Iraki) alivamiwa huko iraki baada ya Saddam kuanguka na FBI kwani walidai anawapa wairan siri za USA...Huyu anakwenda kwa jina la Ahmad Challabi!

Lakini yeye kushtukiwa haina maana nawengine hawafanyi hivyo!

Na sidhani kama watapokea AMRI kutoka washington kwani sasa wanapokea amri kutoka Tehran na USA wanajuwa hilo kwani Iran inawapa kina Alsadr zile IED ambazo zinapenya kwenye humvee za wamarekani licha ya wao kutumia mabilioni ya dola kuzifanya zisipenyeze mabomu!

Hivyo basi...Kama vita ikianza...Iraki na Iran zitajiunga..Na lebanon!

Muisrael na yeye ana Nyuklia hivyo options zote ziko mezani!

Lakini hiyo haimaanishi kwamba watashinda kiulaini!
 
..its all about oil wakuu msijifanye hamjui,mafuta ya waarabu ndio Economy engine ya America,hata american highways & infrastructure zina exist kutokana na mafuta ya waarabu (angalia gas tax inayokwenda kwenye highways construction na employment kwenye oil industry ndio mtajua),na sasa Iraq wameshaiweka mfukoni na ni kama koloni lao na juzi nasikia wall street companies through state depts wamekula contracts za mafuta Iraq zitakazowapa almost 50 yrs sasa hapo mjue mafuta ya Iraq sasa ni ya wamarekani na saudis hao tunajua mwenye mali pale ni EXXON & American companies tuu,Kuwait ndio kabisa wala msiseme maana huko ndio kuna jeshi kubwa sana la US na hawatatoka mpaka mafuta yaishe,sasa Iran na Chaves walijifanya kupeg mafuta yao na currency nyingine badala ya dollar sasa hapo ndio walimwingiza kichaa mmarekani kwa kutaka kucheza na mighty petrodollar,one thing for sure najua soon or later Iran atapigwa na hawa watu kwa kisingizio chochote kile....akitaka asipigwe aharakishe kuunda nuclear bomb lake la sivyo fate ya saddam inawasubiri na labda Obama awe President anaweza asiwapige lakini naye kumbuka ni hao hao.
 
Chalabi ana akili sana na ni kinyonga.

Ni mmoja ya watu wajanja sana, na kwa kuwa alikwenda US akiwa teenager, basi kila kinachofuata kuhusu huyu jamaa ni kwamba haaminiki.

Halafu alidhani kwamba kurudi Iraq kungempa urais na akaishia kuambulia patupu bila hata kura moja kwenye uchaguzi.
 
Chalabi ana akili sana na ni kinyonga.

Ni mmoja ya watu wajanja sana, na kwa kuwa alikwenda US akiwa teenager, basi kila kinachofuata kuhusu huyu jamaa ni kwamba haaminiki.

Halafu alidhani kwamba kurudi Iraq kungempa urais na akaishia kuambulia patupu bila hata kura moja kwenye uchaguzi.

Marekani wali msideline kwasababu alikuwa akishirikiana na Ahmedinejad na kumpa siri za marekani!
Na sasa wakampa Al Maliki ambaye na yeye ni damu damu tu na Iran sema hajionyeshi wazi!
Hiyo ni baada ya ALAWI ambaye na yeye ni kama Saddam tu!
Na Alsadr na yeye ana nguvu sana na hataki kabisa marekani waendelee kuwepo Iraki!
Huyu yeye hata kujificha ni huko IRAN!
Lakini sasa hata wa marekani wameshaanza kugwaya kwani wanajuwa kuwa kuwasaidia mashia kisilaha na kimafunzo ya kijeshi kama walivyokuwa wakifanya ni mbaya kwani wanaweza kuwageuka kama vita ikianza na Iran.
Na kwa sababu hiyo basi...Walianza kuwashirikisha wale watu wa Saddam na wengine waliokuwa Alkaeda!
Sasa hata Mshia asipomsapoti...Basi mmarekani atamsadia msunni tena illi kuweza kumshinda mshia!
Tatizo ni kwamba situation ni tofauti sana na kweli MOTO UTAWAKA kama vita ikianza ni BALAA!
 
Chalabi ana akili sana na ni kinyonga.

Ni mmoja ya watu wajanja sana, na kwa kuwa alikwenda US akiwa teenager, basi kila kinachofuata kuhusu huyu jamaa ni kwamba haaminiki.

Halafu alidhani kwamba kurudi Iraq kungempa urais na akaishia kuambulia patupu bila hata kura moja kwenye uchaguzi.

....sijui hata kama wanamkumbuka na kazi yake ilishakwisha na si unakumbuka alivyoleta kidomo domo wakamwambia aliwapa false intelligence huku wakijua alikuwa ni kibaraka wao tuu,hata saddam alikuwa daring wa Washington na walimpa silaha zote zilizoua almost 2 million Iranians,usicheze na maslahi ya hawa macapitalist watakumaliza...dawa ni kuendelea tuu na kuwa na nguvu kama wao si unaona hawasemi chochote juu ya mchina au Russia maana wanajua firepower waliyonayo au unda nuclear bomb!
 
Asilmia 70 ya wairaki hawawataki wamarekani tena waendelee kukaa Iraki.
Na ukitaka kujuwa kuwa serikali ya Iraki iliyowekwa na Mmarekani inamsikiliza Muiran...Leo hii serikali ya Iraki insema kuwa hawataki tena wamarekani waendelee kuwa hapo Iraki unless wanatowa ratiba kamili ya ku withdraw!
Sasa na wao kwanini watoe uamuzi huo wakati huu kama si wasiwasi kuwa sasa ni Brother ya Muiran Anapangiwa namna?
Wao pia ni mamluki na hawana haja ya kusikilizwa!
Yani Walimshindwa Saddam wakasaidiwa na Bush na sasa wanamgeuka Bush?
Kaazi kweli kweli.
 
Mwanakijiji,

naomba ni kujibu kwa swali, Hivi unadhani marekani ingempiga Iraq ingekuwa peke yake bila msaada wa majeshi ya Ulaya
 
Hivi kweli kuna mtu anaamini kabisa kuwa Iran inaweza kusimama dhidi ya Marekani kijeshi?

Kwani sasa wanafanya nini IRAKI?

Kama wameshinda vifo vya nini vya wanajeshi na wananchi?

Hivi hata hujui kuwa GREEN ZONE NDIO IRAKI YAO?

Hao viongozi wenyewe hata mtaani hawapajui! Kila kitu ni huko greenzone na ni kama ngome iliyokatikati ya jiji la Baghdad ikiwa imepitiwa na mto safi unaotiririka maji na hapo ndio maana panaitwa green!

Hapo ndio kuna nyumba zote za maofisa wote,serikali,balozi na kila kitu na ikulu zote za Saddam zilikuwa maeneo hayo ya kifahari!

Ni kama vile maeneo yote ya oserbay na maeneo yote mazuri ya jirani yapigwe ngome na kufunguliwa mahoteli na jiji ndani ya jiji ama NGOME KUU!

Mpaka MC DONALDS,STARBUCKS,BURGER KING NA KILA KITU...!

YANI HAPO GREEN ZONE NI MA US NA MAUROPA!


Ni ngome kama kijiji na jeshi lote linalinda hapo!

Kama wanaokufa ni wale askari wanaokwenda ku patrol na wananchi wanaoukumbwa either kwenye crossfire ama suicide bomb uko mtaani ambapo hakuna visima vya mafuta wala serikali wala hata mmarekani mwenyewe.

Wao wanaonekana kwenye tv tuuu!

Na wanapokwenda mahali nje ya green zone ni kwa siri na ulinzi wa halli ya juu!

Kama ni kwa wazi basi jeshi la marekani linatanda angani na kila mhali!

Je vita vikianza na Iran...Watapigana upande wa marekani kama walivyofanya walipomtoa Saddam?

We unafikiri hakuna mgawanyiko jeshini na hata CIA?

Kuna mtu hajui kuwa hata pesa za kupigana Iraki wanakopa China?

Kuna mtu hajui kuwa hapa si suala la ushindi tu bali ni vita kuendelea tu na mwenye kunufaika ni nani zaidi ya muuza silaha?
 
Hivi kweli kuna mtu anaamini kabisa kuwa Iran inaweza kusimama dhidi ya Marekani kijeshi?

Watu wanasahau kabisa kuwa:

(a) Silaha za nyuklia zililetwa hapa na wamarekani.

(b) Iran ni kama jimbo moja tu la Marekani.

(c) Bajeti ya ulinzi ya Marekani ni kubwa kuliko ncho yoyote duniani: soma hapa.

Binafsi niliwahi kufanya kazi za mikataba na Pentagon ambapo kwenye porject yetu walikuwa wameweka dola milioni 600 kwa kipindi cha miaka mitano. Sisi tulikuwa ni vitishari tu wa kutafuta teknolojia mpya za kupigana vita ambao tulikuwa tunaruhusiwa kuandika matokeo ya utafiti wetu kwa dunia nzima; je unadhani wale ambao walikuwa hawaruhusiwi kabisa kuandika matokeo ya tafiti zao walikuwa wanajua nini?

Mgogoro wa kijeshi wa US huko Irak watu wanauona kwa mtazamo fupi sana. wanasahu kuwa marekani haikushindwa vita ile, walichoshindwa ni kuistabilize Iraki baada ya vita. Kwa upande wa vita waliisambaratisha kabisa nchi ile kwa muda wa mwezi mmoja tu. Ni dhahiri kuwa haitachukua muda wa zaidi ya mwezi mmoja kama wakilazimika kuisambaratisha Iran bila kujali namna ya kuistabilize. Ni raia wa kawaida kama mimi na wewe ndio watakoumia zaidi endapo vita ya namna hiyo itatokea ingawa viongozi wa kisiasa wanaweza kunyongwa pia.

Swala la Iran linaweza kuwa gumu sana kwa vile wairan wenyewe hawaaminiani. Huko Marekani na Australia kuna wairan wengi sana ambao hawana imani na kabisa na mfumo huu wa siasa uliopoa Iran ambawo ulisimikwa na Ayatollah Khomenini miaka takriban 30 iliyopita baada ya kumpindua Shah. Bado kuna msugunao kati ya wairani wa Ayatollah na wale wairan wa Shah.
 
Fuatilia news kuwa their military is stretching thin!

Tatizo jeshi la USA liko kila mahali duniani wengine wanaishi kwenye zile battleships kila bahari hapa duniani na karibia kila nchi hapa Duniani.
So tatizo ni ku stretch thin.
 
Hivi kweli kuna mtu anaamini kabisa kuwa Iran inaweza kusimama dhidi ya Marekani kijeshi?

Si hao Wairaq pamoja na kuwa walikuwa na vikwazo vya kiuchumi kwa miaka mingi ambavyo viliwafanya washindwe kununua 'silaha za kisasa' mpaka kesho kutwa wanawatoa kamasi nyembaba. Vita ambayo Wamarekani waliambiwa ingetumia $30 billion mpaka sasa hivi imeshatumia $650 billion and counting.

Hawana jeshi sasa hivi watu hawataki kujiandikisha na waliokuwepo wengi wameonja chungu ya vita na wengi hawako tayari kushiriki vita nyingine. Na uchumi wa US sasa hivi hauwezi kustahamili vita nyingine maana utaporomoka kabisa mpaka chini na itachukua miaka 20 au zaidi kuujenga upya 'kama itawezekana' kuujenga.

Hivyo 'Taifa kubwa' kelele nyingi tu lakini wakikutana na watu jeuri basi ubavu wao wala si wa kutisha kiasi hicho.
 
we gonna opt for a MASSIVE pre-emptive strike if iran keeps on threatening us.they cant stand us, no arabic country will ever do_Our population is just over 7 million WORLDWIDE but still we will never be defeated, ever.Jer-USA-lem will never fall again..................................we shall overcome.......x 3
 
Hivi kweli kuna mtu anaamini kabisa kuwa Iran inaweza kusimama dhidi ya Marekani kijeshi?

Ni dhahiri kwamba Iran ni vigumu kusimama man to man na Marekani na kuishinda, lakini tatizo la vita huwa haliishii pale vita inapotangazwa imeisha, athari zake zinaweza kuendelea vizazi na vizazi, mathalani itakuwaje kuhusu maslahi ya Marekani katika mashariki ya kati?, iran si anaweza kuzivuruga vuruga kwa missiles?, itakuwaje kuhusu Uchumi wa Marekani iwapo itaamua kui engage katika "full war?", Je Marekani akiamua kujiingiza katika hii vita huku mchina na Mrusi wanaendelea kuimarisha majeshi yao ni ipi itakuwa position ya jehi la marekani kuweza kuhimili muziki wa mahasimu hawa wawili?, Je usalama wa Wamarekani na rasilimali zao popote pale duniani utakuwaje iwapo itaamua kujiingiza katika vita?.
 
Humu ndani kuna watu wanaongea kama vile hawaishi kwenye sayari hii. Hawaijui kabisa Marekani na na watu wake. Inawezekana kuwa kuna ndugu zetu wa kuzaliwa ambao ni raia wamarekani. Ukifika mji kama San Francisco unaweza ukafikiri uko China ama India ama Uarabuni ama hata Uswahilini kwa jinsi watu walivyochanganyika. Kuna maeneo ya Wakikuyu wa asili ya Kenya na maeneo ya Waetria wa asili ya Ethiopia.

Marekani wana mipango mpaka ya miaka 50 ambayo tayari inatekelezwa. Kwa ufahamisho tu ni kuwa marekani ni nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta kuliko nchi zote za kiarabu lakini kwa nini wachafue mazingira wakati mafuta bado yanapatikana Iran, Venezuela na kwingineko. Je katika miaka 20 ijayo nishati mbadala itakuwa haijapatikana pamoja na technology inayobadilika kukicha. Je kuna yeyote amejiuliza kwa nini wanaitumia Iraq kama testing ground kwa askari wao wa miguu wakati wana uwezo wa kuangamiza kwa dakika moja bila kushuka ardhini kama walivyofanya Hiroshima na Kagashaki. Kama unaamini kwamba Osama kawashinda unaota kwa sababu akipatikana Osama sasa hivi watakuwa na sababu gani ya kuendelea kukaa Afghanistan na Iraq karibu na Iran na Urusi.

Kumbuka walivyompamba Sadam Hussein pamoja na mother of all battles, elite guards na silaha za moto za kuangamiza. Lakini bado walisafiri maelfu ya maili kwenda kumpiga nyumbani kwake. Kuna waliotabiri ungekuwa mwisho wa dunia kama wanavyotabiri sasa Iran ikishambuliwa. North Korea wamesalimu amri, itakuwa Iran. Kumbuka unapoishambulia Marekani unashambulia watu wote wa dunia. Marekani italipuliwa na Marekani yenyewe.
 
... Hawa jamani msiwa under estimate kiasi hicho. Jueni wako kimya wanajitayarisha kwa vita, na Irani wanajua hilo. Na Irani anajua anayo kazi kweli. Myahudi si mzaha jamani. Waarabu wanajua hili acha propaganda zetu hapa jf.

Sasa achaneni na kelele za Irani. Watu hawapigani vita kwa kelele wanazofanya Irani, hapana. Hii yote ya kutangaza habari ya makombola sijui na nini ni tisha nyau tu...!!

Statement ya karibuni ya waisraeli....

".... Hatujui kuongea sana, Hatukujaliwa kuwa hivyo..tumejaliwa kufanya kile kinachotakiwa kufanyika...Tutafanya kile kisichotegemewa kufanyika...."

.. We will do what must be done.. we will do the impossible...
 
"IRAM attacks could be very tragic against us," said Col. William B. Hickman, the commander of the 2nd Brigade Combat Team of the 101st Airborne Division, which operates in northwestern Baghdad. "We take them very seriously."
As the number of U.S. soldiers in Baghdad has begun to drop with the end of the "surge" of additional forces, U.S. military officials are placing a higher percentage of their troops in small outposts in densely populated neighborhoods. U.S. military officials say this is crucial to ensure the continued training of Iraq's security forces, win the trust of the capital's residents and improve local governance. But deployments in small outposts - some are manned by just one platoon - also have made soldiers more vulnerable.
To counter the threat posed by rocket-propelled bombs, soldiers have stepped up patrols around outposts, fortified their buildings and offered tens of thousands of dollars for information about networks that use the weapon.

NB:Sasa kwani hawajui hiyo ni kazi ya Muirani?
Hivi Bush alipoambiwa ni ukichaa kumtoa Saddam madarakani alifikiri wengine ndio vichaa?
Kama kweli walikuwa hawataki Irani iwe hatari..Kwanini walimwondolea mtu ambaye aliweka balance pale middle east?
 
Binafsi ninaamini hakuna Mungu mtu dunia hii.. si Marekani wala China.. Kinachotangulia ni nani ameshambuliwa!..
Kama Israel itaishambulia Iran vita hii itakuwa kubwa sana na siwezi kusema Israel atashinda... Iran yuko nyumbani ana kila uwezo wa kujilinda na matokeo yakawa tofauti. Hezboullah wa Lebanon waliweza kumsimamisha Israel sio mara moja as a fact walimfukuza Lebanon. Vietnam waliweza kumfukuza Marekani, Afghanstan walimfukuza Mrusi na leo hii bado wanapambana na majeshi ya jumuiya ya NATO.

Lakini nchi hizo hizo haziwezi kusimama hata dakika moja kama watazishambulia Marekani, Israel ama Urusi.
Kwa hiyo jamani tusitake ku under estimate matokeo ya vita!...Ni kitu ambacho tusitake hata siku moja kuombea.. Vita sio Olimpiki wala mashindano ya mpira, hizi ni roho za watu...
 
Mwanakijiji,

naomba ni kujibu kwa swali, Hivi unadhani marekani ingempiga Iraq ingekuwa peke yake bila msaada wa majeshi ya Ulaya

Mkuu, si kwamba Marekani alishindwa kumpiga Irak peke yake; Jeshi la pamoja la Ushirika ni sehemu ya propaganda tu kuionyesha dunia kuwa Mbabe (USA)hajamwonea Mnyonge (Irak) bali ni kuonyesha kuwa dunia (Magharibi) yote iko kinyume na Saddam kwa hiyo lazima apigwe.

Kama Maerekani angekosa support ya Allies wa Magharibi dunia yote ingekuja kinyume cha Marekani.
 
Back
Top Bottom