Iran kuleta madaktari 1,000 Tanzania

Itabidi serikari iwaajiri na wakalimani maana sisi wa kipato cha chini hata kiswahili hatujui. Hicho kiiran tutaelewana kweli na hao madaktari?
 
source press tv
serikali ya iran imejitolea madaktari 1000 kuja nchini tanzania na hawatalipwa chochote hadi hapo mgomo utakapopata suluhisho na iran imesema yenyewe imepiga hatua sana kwenye sekta ya afya na haiwezi kuona serikali rafiki yake inaangamia
Waende zanzibar..bara hatuwataki!
 
Hawa Madokta wa Irani wafanye haraka kuja, maana wagonjwa wanateseka kwa kusitishwa huduma
 
Hivi kwa nini Iran inajipendekeza hivi kwetu!? hapo kuna kitu lazima! is it a pay back after the embargo??

Hakuna cha kujipendekeza hapo. Cuba iliwahi kumsihi mwalimu apeleke jivana wengi Cuba wakasomee udaktari - wanaojifanya fani hii ni ya wateule wakaipiga vita na kuendelea kubana hata RMAs, MAs wasisonge mbele kitaaluma kwa vile fani hiyo ni ya wateule wachache. Hakuna mtu aliedhania kuwa Nurses wanaweza soma hadi degree level. Hapa pana nadhalia ya balance ya demand na supply. Tungekuwa na supply ya huduma ya madaktari kuliko au sawa na kuhitajika kwao yasingetokea haya kwa kiwango hiki - kila kituo cha afya kikawa na MD - jambo ambalo lingewezekana

Kikwete anza upya kama Mwalimu alivyoanza upya kulijenga jeshi letu la wananchi - hawa ni madaktari mamluki hawatufai. Kumbuka kikwete hata mwalimu alipata msaada wa Nigerians kuilinda nchi hii. potelea mbali wapewe hayo madini kuliko kuendelea na watu wauwaji wamevaa makoti meupe na kutunyolinyolisha wanashuhudia maisha ya watu yakipotea hivi hivi.

TO HELL!!
 
Walivyo wadini wale sijui. Wanaume wote mjiandae kufuga ndevu na kuvaa vipedo na wale akina dada zangu kuweni macho. Anzeni kutafuta mabaibui ule wakati umewadia sasa.
 
looh!kwa mtindo huu si kulaumu tena ila watanzania yatupasa sasa kuingia kwenye maombi ya kuombea nchi yetu,,jk ameshawachoka watanzania
 
Ni hatua nzuri kuna wagonjwa wengi wapo hoi wanaitaji kutibwa Iran tunashukuru sana na nchi zingine zitaiga mfano wa Iran.
 
source press tv
serikali ya iran imejitolea madaktari 1000 kuja nchini tanzania na hawatalipwa chochote hadi hapo mgomo utakapopata suluhisho na iran imesema yenyewe imepiga hatua sana kwenye sekta ya afya na haiwezi kuona serikali rafiki yake inaangamia

Are they experienced in tropical medicine? Hawa akina Pinda wanafanya mchezo na medicine!!! Compatibility na manesi wetu did they take it into considerations!!
 
Kuna tetesi kuwa nchi ya Iran imejitolea kuleta madaktari 1000 kukabiliana na mgomo wa daktari nchini. Madaktari hao hawatalipwa posho wala mishahara mpaka madaktari wa tz watakapositisha mgomo. Kama kuna mtu ana habari zaidi atujuze
 
Kwa sababu za kiusalama na uhai wa hili taifa ningeshauri hawa madaktari toka Iran wasije. Wabunge wa CCM wana responsibility ya kulinda uhai wa hili taifa, wapo wengi bungeni, na ndio wenye serikali. Ni jukumu lao kuhakikisha hii nchi inabakia salama, na ujio wa madaktari utatuweka kwenye mtihani mkubwa.
 
Watafanya kazi na wasaidizi gani?pia suala la lugha na utafsiri itakuwaje hasa vijijini?hizo gharama zi wangenunulia vifaa na kuboresha mazingira??
 
Back
Top Bottom