Iramba magharibi mbioni kwenda upinzani?

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Tathmini za kisiasa zilizofanyika ndani ya wiki tatu zilizopita na mfululizo wa matukio ya woga na kujihami, zinaoneka kuupa upinzani nafasi kubwa ya kulitwaa jimbo la Mheshimiwa Mwigulu, hii ni baada ya mkakati mkubwa wa kisiasa uliopangwa na CHADEMA wa kuanza kuyashambulia majimbo ngome ya CCM kuvuja, na makada wa Ccm kuamua kuanza kuuzuia kwa kila njia ikiwemo kubambikiza kesi na matukio ya kutengeneza ya fujo.

Mheshimiwa Mwigulu naye ameanza kuwalalamikia kichinichini baadhi ya makada wenzie kumwachia mzigo mwenyewe na kuvujisha kwa makusudi
mikakati ya ndani ya secretariety kama vile vita ni ya kwake mwenyewe wakati ni jukumu la viongozi wote wa chama kusisima pamoja naye.

Chadema wao wanadaiwa kwenye mpango wao kusema kuwa kwa sasa wanaweza kuchukua jimbo lolote Tz bara kama wakiamua tu kuwekeza muda, rasilimali na nguvukazi yao kwa pamoja kwenye jimbo husika na wakiwa na mgombea mahsusi,

Mkakati wao huo kuelekea 2015 ni Kuendelea na operation zao za M4C na Sangara ambazo zimeonesha mafanikio, target yao ikiwa ni majimbo ya; Iramba magharibi, Mtera, Igunga, Tabora mjini, Nzega, Morogoro mjini, Kilombero, Kibaha mjini na vijijini, Kondoa, Dodoma mjini, Mtwara mjini, Lindi mjini, Mbeya vijijini, Songea mjini, Ulanga, Mkuranga, Nchinga, Masasi, Namtumbo, Tanga mjini, Korogwe, majimbo yote ya mikoa ya: Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba, Dar, Manyara ,Kigoma , Shinyanga, Rukwa, Iringa na Mara.

SOURCE: KADA MWANDAMIZI
 
Nawashauri magamba wakimbilie kenya maana hiyo kasi ya m4c balaa!hilo chemba badala litetee masikini waliojaa iramba analeta taarabu na ukada,shame on him
 
Iramba Magharibi litakwenda kwa WAJINA lake Dr. Kitila MKUMBO. Hata huyu Mkumbo (Lameck) aiyesaliti jina lake anajua hivyo.
 
Tujitahidi kupigania maendeleo na uwakilishi wenye tija Bungeni. Nafikiri umefika wakati wa kuacha siasa za majina na majivuni. Tunachotaka kuona sisi wananchi tuliowachgua ni maendeleo ya kuonekana na si takwimu tusizozielewa.
 
Back
Top Bottom