''ipo siku itakuwa kweli''

Mar 2, 2012
52
5
...Jana Profesa Ibrahim Haruna Lipumba alirejea kutoka Marekani. Nilijaribu kufuatilia vyombo mbalimbali vya habari na kuangalia "coverage" ya mapokezi yake. Star TV walionyesha "live" hata hivyo walikuwa "somehow" selective...taarifa ya habari ya saa 2.30 usiku (Radio Free Africa) hawakutoa taarifa ya mapokezi yale; TBC1 waliiweka habari ya mapokezi yale kwa uzito wa pili na walitangaza kwa chini ya dakika tatu (3); ITV (skiuitazama - umeme ulikatika, Morogoro kutokana na mvua kubwa)...kwenye mitandao ya kijamii: wanabidii (hakuna thread yoyotokezi yale iliyoanzishwa na au kuchangiwa sana); mabadiliko (kama ilivyokuwa kwa wanabidii)...kwenye magazeti ya leo: Mtanzania (cover story) habari ya kwanza; Tanzania (cover story) habari ya pili (kwa picha ya mapokezi); N...ipashe (habari ndogo ukurasa wa mbele...habari kamili ukurasa wa 4); Mwananchi (habari ndogo na picha kubwa ukurasa wa mbele)...habari kamili ukurasa wa 4; UHURU ukurasa wa mbele hakuna habari yoyote wala picha ya mpkezi ya Prof. Lipumba...habari ya kizushi (ukurasa wa 3: Wafuasi wa CUF wamdhihaki Slaa); DIRA (ukurasa wa mbele na za ndani zote hakuna habari za mapokezi ya Prof. Lipumba); na Habari Leo habari ya mapokezi uzito wa pili (habari kamili ukurasa wa 4) habari picha ukurasa wa kwanza.

Kwa ujumla, nimegunda kwa sehemu fulani kuna "vita vya habari" dhidi ya CUF. Inawezekana hii ni "deliberate move" ya wanaoihujumu CUF au ndio mwnedo wa uandishi wa habari za siasa unaozingatia weledi wa habari na jisni zinavyotokea; sidhani! Hata hivyo, kwa taathira ya jinsi nilivyofuatilia mapokezi yale na jinsi vyombo vya habari (ukiachilia mbali gazeti la Mtanzania) nadhani kuna "hila" na au "mizengwe" ya makusudi iliyosukwa katika KUIHUJUMU CUF na siasa za visasi au ukosefu wa ukomavu wa demokrasia. ''IPO SIKU ITAKUWA KWELI'' Facebook
 
Back
Top Bottom