Ipo hivi kwa wengi kila wakati...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Ukiwa na mpenzio/ mume/mkeo mwatembea mmeambatana, mara inapotokea jozi (pea) nyingine ya wapendanao mkapishana nayo, jaribu kuchunguza kwa makini...

Wengi ya wapendanao huwa wanapoteza kabisa kwa muda hisia zao juu ya wenzi wao...

Kwa kawaida baadhi ya wanaume huwa na jicho la kasi la tathimini, waweza hata kugeuza shingo kwa staili kumtizama mwanamke wa wenzie..huku akifikiri moyoni labda kuna vitu anavikosa.... Pengine kama utabahatika, unaweza kukuta kumbe na mwanaume mwenzio nae huko nyuma alikuwa akimkata jicho wa kwako akiwa na fikra zinazofanana na wewe!!.

Kwa wanawake, wao si rahisi sana kukuta anageuka, ila baadhi yao anaweza kuanza kuwaza moyoni mambo mengi ikiwemo tofauti iliyopo katika yake na mwanamke mwenzie au kati ya mwanaume alie nae na yule wa mwenzie.. tofauti ya mavazi,ulembo na harufu ya manukato yake na yale ya mwenzie..atatamani au kukereka nafsini, kwa nini ipo vile kwa wengine na sio kwake...

Ukiwa makini sana unaweza kuyabaini haya kwa vitendo, ..wengi ya wanawake, anaweza kuguna,kuanza kujifuta uso, kulamba midomo, kurekebisha nywele, kuweka vizuri pochi, mavazi yake nk au pia kuanzisha maongezi yeyote tu juu ya wale mliopishana nao.. kama si kuwaponda basi kuwasifia.

....kama hakuwa amekushika mkono, bega au kiuno, na akiona hizo pea nyingine wameshikana, atafanya kila jitihada ya kuhakikisha nae anakukaribia, au pengine ikiwa ni mwanaume unamkwepa kwa kuwa ndae mbali, atazungumza tu "ona wenzetu/wenzio wanaojua mapenzi"...

Kwa asili, wengi wetu huwa twapenda kutamani au kuchukia kitu kikiwa kwa mwenzio..mengine yanatufundisha na mengine yanatuharibia kabisa...
 
Ni moja ya vitu ambavyo mimi nimeviingiza kwenye kundi la involuntary reflexes! Mie ni lazima nitazame na kwa kweli hupenda kujifunza kutoka kwa pea nyingine yale yote ambayo naona ni mema.
 
Ila wakati mwingine huyo uliyenaye asiwe mkorofi, maana wengine wanaweza kuanzisha zogo kwa nini umegeuka wakati upo nae!
 
Ni moja ya vitu ambavyo mimi nimeviingiza kwenye kundi la involuntary reflexes! Mie ni lazima nitazame na kwa kweli hupenda kujifunza kutoka kwa pea nyingine yale yote ambayo naona ni mema.

pengine unaweza kujikuta umejikwaa au unazabwa kibao..
 
Inatokea hata kama uko mwenyewe ukakutana na wapenzi wameongozana, jana nimepishana na couple mahali nikawaza wamependeza nikageuka kuangalia tena nikakuta nagongana na macho ya mwanaume nikajiuliza kwa nn amegeuka?
 
Hila kwa Dar utatokwa na kucha nylamsingi ingi maana kila mtaa.....disgn tofauti.......utachemka tulia nawako sikia kengele!!!!
 
Lazima uchungulie kidogo ati....hata hiyo couple itakua imewachungulia na nyie...
Ishu ni jinsi ya kuchungulia...usikamatwe!
 
Hila kwa Dar utatokwa na kucha nyingi maana kila mtaa.....disgn tofauti.......utachemka lamsiningi tulia nawako sikia kengele!!!!

Hila kwa Dar utatokwa na kucha nyingi maana kila mtaa.....disgn tofauti.......utachemka la msiningi tulia nawako sikia kengele!
 
hilo kwa kweli ni la kawaida, hata shemeji yenu analijua maana hata saa nyingine kama sijaona ananistua niangalie, maana mara ya kwanza nilikuwa naibia kumbe alikuwa ananichabo tu, sasa ikatokea siku tulipishana na kapo na kabla sijageuka nilimtupia jicho kwanza nione yupo wapi na kabla sijakaa sawa akaniuliza leo ugeuki kuangalia hao jamaa, na kuanzia hapo ikawa kama ni joki tu lakini ndio hivyo, lazima niangalie lakini sasa bila kificho
 
hilo kwa kweli ni la kawaida, hata shemeji yenu analijua maana hata saa nyingine kama sijaona ananistua niangalie, maana mara ya kwanza nilikuwa naibia kumbe alikuwa ananichabo tu, sasa ikatokea siku tulipishana na kapo na kabla sijageuka nilimtupia jicho kwanza nione yupo wapi na kabla sijakaa sawa akaniuliza leo ugeuki kuangalia hao jamaa, na kuanzia hapo ikawa kama ni joki tu lakini ndio hivyo, lazima niangalie lakini sasa bila kificho

Mkuu kuna kisa kimoja, jamaa mkewe aliamua akaongezee "makalio ya kichina"..kwa kuwa mzee alipenda sana kupiga kijicho/ chabo pindi akiona "waliojaaaliwa makalio" wanakatiza karibu yake.

Hakika kwa akina mama wengi upenda kutimiza yale ambayo yatawazuia wenzi wao kufikiri tofauti. Hali hii ndio inapelekea kupitiliza katika vibwagizo vya miili yao ikiwemo kujiongezea "ulaini na un'gavu wa sura zao ikiwemo kujichubua/kupiga deki sura; kujiongezea makalio na nyonyo, na wengine hata udiriki kutumia zile soap za kichina za kubana/ kuirejesha ujanani "bustani ya Eden" ilimradi kuwafurahisha wapenzi wao pasipo kufahamu maradha yake..
 
Ngoshwe,trust me!wanawake pia huwa tunageuka.ila kwa style flani,kwa hiyo huwezi kugundua!:bowl:
 
Kiasili binadam hatosheki na wala haitafika siku akatosheka. Si ajabu wanaopishana wangependa kubadilishana wenza kuona ni kitu gani mwenzake anafaidi nae anakikosa. Ndio maana wazungu wanafikia hatua ya ku swap wenza. Sasa kwa hisani ya watu wa marekani tusifike huko
 
Back
Top Bottom