Ipi sahihi ktk kiswahili sanifu.kati ya thumni au sent hamsini?

Zote ni sahihi. Tofauti yake ni kwamba thumni ni sarafu moja yenye thamani ya senti hamsini. Kwa hiyo senti hamsini inaweza kuwa katika sarafu moja (thumni) au sarafu nyingi zenye thamani ya jumla ya senti hamsini. Inaweza kuwa sarafu tano za senti kumikumi au sarafu kumi za senti tanotano au sarafu hamsini za senti mojamoja.
Nadhani nimeeleweka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom