Ipi ni sahihi katika mahusiano?

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,554
Alinitamkia kuwa ananipenda, kipindi penzi likiwa motomoto, kwa mdomo wake tukiwa kwenye mtoko beach tumejiachia alinambia hivi "Sweety ninavyokupenda hivi, ikitokea ukaniacha nitaumia sana, kwa hali hiyo nitajitahidi mi ndo nitangulie kukuacha" Nilimwangalia sikupata kumwelewa, badala yake nilihama mada tukaendelea na mambo mengine hadi mda ulipofika tukaagana. Tangu siku hiyo nimekuwa nakaa naye tu ila akidemand mambo fulani namwambia bado natafakari maneno alonambia tukiwa kwenye mtoko. Amekuwa akiwatumia marafiki zangu wanibembeleze niweze kumsamehe kwa kosa la kauli yake . . . . ukweli nami naogopa kuendelea naye. Marafiki wanasema nimtamkie, wengine wanasema niache hivyohivyo. Ipi ni sahihi? Nimwambie basi au niendelee kumyuti hadi kieleweke?
 
Duh! Msamehe aisee wengine huwa wanaongea tu bila kufikiria impacts zitakazotokea.
 
Kiongozi sijisifu ila ukweli ni kwamba nikimtamkia m2 kuwa nimekupenda nakuwa namaanisha. Sasa inapotokea aka-miss behave tena kwa kauli - huwa naudhika sana. Ulimi uumba.
 
Du kaka,samehe kaka, kama unampenda kweli hiyo kauli haiwezi kuwa sababu ya kumuacha. Otherwise utakuwa ulipanga tu kuwa uhusiano mfupi-just to pass time and now that ameongelea 'kuanza kukuacha' unataka umtangizie.
 
Bibie, sitaki nimtangazie, mpango wangu kuwa nutral, akinipigia cm nampokea, akitaka tuonane tunaonana, jambo moja tu ni ku xxxxx hadi hapo atakaponambia alikuwa na maana gani. Huduma zote anapata kama kawaida kasoro hiyo ya xxxx
 
Kiongozi sijisifu ila ukweli ni kwamba nikimtamkia m2 kuwa nimekupenda nakuwa namaanisha. Sasa inapotokea aka-miss behave tena kwa kauli - huwa naudhika sana. Ulimi uumba.
ulimi hauna mfupa. Hilo ni jambo dogo sana la kufanya livunje uhusiano wenu labda kama ana tabia zingne za ajabu au wewe unamtaftia sababu.
 
mbona sioni tatizo hapo? inatokea sometimes unamwmbia mtu: ukifa nitaumia sana bora nife mimi. haimaanishi kua nitajinyonga kwa kukimbia maumivu ya msiba. vile vile hajamaanisha kua atakuacha kwa kukimbia maumivu ya kuachwa ila angekua na uwezo angependa yeye ndio aamue kukuacha kabla hujaamua. sasa unavo chukulia kauli yake so serious unapunguza hata kiwango cha penzi na next time hata kwambia vingine kwa uoga wa reaction yako.
 
Next time ya wapi? Ok mawazo yako nitayafanyia kazi ila .... huoni kwamba tukirudi kwenye mahusiano kama awali atatimiza agano lake ili aniumize? Kuachwa wakati unapenda ni maumivu makali sana ndg yangu,
 
ulimi hauna mfupa. Hilo ni jambo dogo sana la kufanya livunje uhusiano wenu labda kama ana tabia zingne za ajabu au wewe unamtaftia sababu.
Uongo mbaya hana tabia mbaya, anakubalika hata kwa washkaji zangu, sikuwahi kusikia neno baya kwake, si kilema, si tegemezi kwangu, umbo la kiafrika - Si unajua viumbe wa Kizinza, nisiongee mengi jamani.
 
sasa si umsamehe. Na yeye akibadili maamuzi imekula kwako.
 
Du kaka,samehe kaka, kama unampenda kweli hiyo kauli haiwezi kuwa sababu ya kumuacha. Otherwise utakuwa ulipanga tu kuwa uhusiano mfupi-just to pass time and now that ameongelea 'kuanza kukuacha' unataka umtangizie.
daughter umesema kweli. mie binafsi sioni tatizo kubwa na hiyo sentensi aliyosema, ni kweli si nzuri sana masikioni lakini ndugu yangu ukiwa unachunguza na kuitafakari kila sentensi inayozungumzwa na mwenzi wako basi mapenzi yatabaki kuwa ndoto kwako. ushauri wangu mueleze ukweli kuwa kauli yake hiyo ilikukera na kukuvunja moyo sana, naa baadaa ya hapo muendelee na mapenzi yenu kama kweli bado una nia nae nawe ni binadamu kuna mengi utakuja kuongea yatamkera lakini si yakufikia kuachana. unless uwe ulishaamua kumbwaga ndio umepata sababu!
 
Ningekuwa sijamsamehe ningekuwa nimekata mawasiliano na yeye! Pili yeye mwenyewe anaomba msamaha tu lakini hanambii alikusudia nini aliponitamkia maneno yale - badala yale analia. Narudia tena - naogopa isije kuwa danganya toto nikajiingiza kwenye hot love tena then yeye akachomoa nikauumiza moyo wangu. Kwa sasa hata akichomoa sitaumia kwa sababu nimejipanga kuachwa. Niko tayari kuamia kwenye fani zingine badala ya mambo ya mahusiano ya kimapenzi. Zingatia hili - usione mtu amebadilika kutoka life style flani na kuingia nyingine ukamshangaa.
Naangalia mbele ndg yangu... kuachwa noma.
 
mkuu mbona sikuelewi, tatizo lipo wap hapo? Anamaanisha YUPO TAYARI KUJIUA NA KUPOTEZA MAISHA YAKE KWA AJILI YA PENZI LAKO. Usiwe na maana moja, ruhusu ubongo wako upapase!
 
Khaaaa! msamehe mwenzako jamani..nahisi alikuwa anaongea kama story nyingine mlizokuwa mnaongea na sidhahani kama aliongea akijua atakukwaza...! Samehe bwana shemeji
 
Back
Top Bottom