Ipi lugha sahihi

Mkuu!
Mimi siyo mtaalam wa kiswahili ila kula chungwa nahisi ni sahihi,katika kula ndo kuna kitendo cha kulinyonya.
Halafu unaweza kusema kunywa juisi ya chungwa siyo kunywa chungwa.
 
Mkuu!
Mimi siyo mtaalam wa kiswahili ila kula chungwa nahisi ni sahihi,katika kula ndo kuna kitendo cha kulinyonya.
Halafu unaweza kusema kunywa juisi ya chungwa siyo kunywa chungwa.

Hapo si mtaalam wa kiswahili ukaweza kupatia vizuri hivyo! Fikiria ungekuwa mtaalam..! Any way umemjibu vizuri ingawaje na mimi siyo mtaalam.
 
Hapo si mtaalam wa kiswahili ukaweza kupatia vizuri hivyo! Fikiria ungekuwa mtaalam..! Any way umemjibu vizuri ingawaje na mimi siyo mtaalam.

Ni kweli ukiacha kiswahili tunachoongea pia kuna wataalam zaidi waliosomea na kubobea katika lugha yetu hii. Tunajitahidi kurekebisha na kujifunza maneno kadhaa kwenye jukwaa hili.
Asante mkuu!
 
kwa utaalamu, chungwa huwa linaliwa pamoja na ile nyama yake nyeupe ambayo ina virutubisho vingi sana sema watu hawajui au wanaona kula ile nyama ni kuendekeza njaa. hapo ndipo linapokuja neno kula chungwa
 
Tafadhali tuhifadhi roho ya kilugha tukitumia "maji ya chungwa" badala ya "juisi". Nakiri ndio "juisi" limeenea sana lakini ..... si lazima hata kidogo liwepo.
 
Tafadhali tuhifadhi roho ya kilugha tukitumia "maji ya chungwa" badala ya "juisi". Nakiri ndio "juisi" limeenea sana lakini ..... si lazima hata kidogo liwepo.

Kiswahili ni Sharubati, lakini pia neno Juisi ni sahihi kwa kuwa limetoholewa toka Kiingereza, Juice.
 
Kula chungwa,
kunywa chungwa,
kunyonya chungwa.Ipi lugha sahihi?
Mimi ninavyo ona yote matatu ni sahihi, inategemea na wakati na kitendo unchofanya.

i.e Ikiwa umelikata chungwa vipande vipande na unachukua ukitafuna basi "unakula chungwa".
Ikiwa ume li-squeeze au umelikamua maji yake ndani ya glass, hapo ndio "unnakunywa (maji ya) chungwa"
Na ikiwa umelimenya na ukalikata vipande viwili na ukaanza na kimoja kukikamua mdomoni hapo utakua "unanyonya chungwa".

Thanks.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom