Ipi kauli ya Lowassa kuhusu waliowekewa mabilioni huko Uswisi - inawezekana naye mmoja wao?

Kwani nchi hii lazima Lowasa awe RAis. Ana guarrantee na Watanzania kuhusu Urais. HAkuna watu wengine pasipo yeye tu.
 
Lini ulikutana naye akakueleza kuwa anautaka Urais?Acha umbeya,na uache uvivu...fanya kazi kwa bidii na wewe utatajirika,ukiedekeza majungu na husuda utaishia kuamini kuwa shida zako zimesababishwa na Lowassa na hakika utakufa maskini!

Tutajie kazi au biashara iliyomtajirisha Lowasa,nasi tuelewe na kumtetea lowasa
 
Taabu ya humu jamvini, ukimtaja tu bwana aliyejiuzuru Lowassa, watu mimacho inawatoka, wanaacha kujadili mada na wanaishia kukuponda kama si kukutukana! Haya bana mi mtazamaji tu!

Amelaaniwa mtu amwambiaye mtu mwovu wewe una haki. jamii itamlaani taifa litamchukia. Mithali 24:24-25
 
Tukiachilia suala hili za mabilioni ya vigogo yaliyowekwa huko Uswisi, Lowassa hata siku moja hajazungumzia ufisadi hapa nchini, hata siku moja sijamsikia. Hii bila shaka ni kutokana na jinsi yeye mwenyewe kubeba tuhuma nzito za ufisadi hivyo kutokuwa na ujasiri wa kulizungumzia kutokana na woga wa kusutwa.

Sasa iwapo anataka urais, au kuna watu wangependa awe rais, hivi kweli anaweza kuishughulikia kansa hiyo kwa nguvu zake zote? Au itakuwa kama vile vile chini ya JK?
 
Watanzania watakuwa wajinga sana iwapo wataamua kumuingiza jamaa huyu Ikulu! Kwa lipi?
Lakini anaweza akatinga Ikulu kwa njia za kifisadi tu -- maana tunaona jinsi anayomwaga pesa hovyo -- makanisani, misikitini, kwa waandishi wa habari nk nk.

Anajua bila ya hivyo hana nafasi.
 
Kwani ni lazima Lowasa atusemee?
Ni lini mtajitambua kuwa nyinyi ndiyo serikali, yaani mpaka aseme lowasa ndiyo jambo liwe limesemwa!!!! Haishangazi kusikia mnagombana kuchagua rais, hamgombanii kuchaguliwa "Rais" kama sheria inavyoelekeza. Usitushawishi kwa ujinga tafadhali NDEVU SI MZIGO.

Ni kwa sababu anataka kiti kikuu cha URAIS wa JMT hapa ndiyo tatizo, angekua nyumbani tu wala...na kiti kile kwa sasa wananchi wamechoka misheni town na mitandao yao ya namna hiyo wanataka watu watakaotokomeza hizi dili na 10% na maslahi binfasi yanayokwanmisha miradi mingi ya maendeleo na maamuzi muhimu ya kitaifa itakayonufaisha taifa.

FYI Ufisadi ndiyo hot topic toka 2010 mpaka hapo uchaguzi utakapoisha 2015 hamna lingine, ili kua relevent washauti hawa akina lowassa, membe etc wadokezee haya mambo, tuelewa wanasimama wapi kwenye hili jinamizi la mamendeleo yetu
 
Back
Top Bottom