Ipi bora...kuonja au kukosa kabisa.......

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,884
Hili swali huwa najiuliza kila siku....
Kama unapata mtu anakuvutia sana lakini
kuna risk kubwa ya kuvunjwa moyo....
Mfano labda huyo mtu yupo kwenye ndoa ,au labda
hajavutiwa na wewe kiwango sawa,au sababu yeyote itakayosababisha
mapenzi yasidumu......je ni bora kuanza mapenzi na huyo mtu...ili uonje ujue
utamu wake bila kujali maumivu yake mtakapoachana????????
Au
ni bora kukaa mbali kabisa toka mwanzo usijue ulichokikosa?????????????
 
Kaa mbali kabisa; unajua huwezi onja nyama ya binadamu usiiirudie.................I can prove that!
 
hapo ndio yale mapenzi ya kupelekeshwa, yaani itabidi ufanye lolote ili kulinda penzi, na mtu akijua una unampenda kuliko yeye anavyokupenda tegemea kuburutwa sana tu...mwisho wa cku moyo wako ndio utaamua kujilipua japo unajua utaweweseka kwenye mapenzi.
 
Kwani ni lazima kuonja? wakati unajua kabisa siku za baadae utatupiwa virago? MI NAONA NI BORA UKAE KANDO TUU, mambo ya mapenzi sio kuumizana bwana! ni maridhiano ya moyo!
 
kwani ni lazima kuonja? Wakati unajua kabisa siku za baadae utatupiwa virago? Mi naona ni bora ukae kando tuu, mambo ya mapenzi sio kuumizana bwana! Ni maridhiano ya moyo!

inategemea na jinsia yako...
Kwa sisi wanaume huwa tuna kuwa na imani kuwa
nitaweza kubadilisha msimamo ili uwe wangu wa milele.
Tabu inakuja ukishindwa kumbadili mtu msimamo.akaamua
tu yaishe....maumivu yake...........
 
Hili swali huwa najiuliza kila siku....
Kama unapata mtu anakuvutia sana lakini
kuna risk kubwa ya kuvunjwa moyo....
Mfano labda huyo mtu yupo kwenye ndoa ,au labda
hajavutiwa na wewe kiwango sawa,au sababu yeyote itakayosababisha
mapenzi yasidumu......je ni bora kuanza mapenzi na huyo mtu...ili uonje ujue
utamu wake bila kujali maumivu yake mtakapoachana????????
Au
ni bora kukaa mbali kabisa toka mwanzo usijue ulichokikosa?????????????

Hivi unapovutiwa na mwanamke na kumtongoza.... unakuwa na Malengo gani??? Hao wa kwenye ndoa wanaotongozwa/kutongoza na wakakubaliana il hali mmoja au wote wako kwenye ndoa... wanakuwa na malengo gani??
 
Sasa unahangaika kuonja cha nini kama una wasiwasi kabisa hutadumu nacho? Achana nacho! Maumivu utakayopata mkiachana yatakuumiza kuliko raha uliyoipata.
 
Mkuu bora uonje kwanza hata ukijaachwa potelea mbali. Utajisifia chenga nimemla ila kibuti kakupiga hahaha!
 
hivi unapovutiwa na mwanamke na kumtongoza.... Unakuwa na malengo gani??? Hao wa kwenye ndoa wanaotongozwa/kutongoza na wakakubaliana il hali mmoja au wote wako kwenye ndoa... Wanakuwa na malengo gani??

labda kwa kuwa wewe ni askofu unaweza usielewe..
Kwa wengine mapenzi ni upofu....bila kujali ni mke wa mtu au mume wa mtu....
 
Hivi unapovutiwa na mwanamke na kumtongoza.... unakuwa na Malengo gani??? Hao wa kwenye ndoa wanaotongozwa/kutongoza na wakakubaliana il hali mmoja au wote wako kwenye ndoa... wanakuwa na malengo gani??

KUMEGANA (period):closed_2:
 
Hivi unapovutiwa na mwanamke na kumtongoza.... unakuwa na Malengo gani??? Hao wa kwenye ndoa wanaotongozwa/kutongoza na wakakubaliana il hali mmoja au wote wako kwenye ndoa... wanakuwa na malengo gani??

Askofu unauliza jibu? Lengo ni ngono zembe..just for fun!!!
 
Hili swali huwa najiuliza kila siku....
Kama unapata mtu anakuvutia sana lakini
kuna risk kubwa ya kuvunjwa moyo....
Mfano labda huyo mtu yupo kwenye ndoa ,au labda
hajavutiwa na wewe kiwango sawa,au sababu yeyote itakayosababisha
mapenzi yasidumu......je ni bora kuanza mapenzi na huyo mtu...ili uonje ujue
utamu wake bila kujali maumivu yake mtakapoachana????????
Au
ni bora kukaa mbali kabisa toka mwanzo usijue ulichokikosa?????????????

Mimi nilidhani unazungumzia kuonja vyenye vikwazo vya kuonjwa kama vile binamu nyama ya hamu, mke wa bosi wako, binti wa bosi wako na kadhalika....Kumbe unazungumzia kuonja vitu vya kamawaida kabisa, hakuna hata risk hapo...!!!
 
mimi nilidhani unazungumzia kuonja vyenye vikwazo vya kuonjwa kama vile binamu nyama ya hamu, mke wa bosi wako, binti wa bosi wako na kadhalika....kumbe unazungumzia kuonja vitu vya kamawaida kabisa, hakuna hata risk hapo...!!!

mkuuu...
Nazungumzia kuonja vile ambavyo ni vigumu kuvimiliki
mfano kama huo mke wa boss wako au wa kaka yako...
Au shemeji yako......
 
labda kwa kuwa wewe ni askofu unaweza usielewe..
Kwa wengine mapenzi ni upofu....bila kujali ni mke wa mtu au mume wa mtu....

Inawezekana kweli sikuelewi... kwa sababu mtu ni mke/mume wa mtu, ukampenda... kwa nini usijizuie ukaachana naye moja kwa moja?? kwa sababu tayari ana mtu wake na hakuna jinsi mtakuja kuwa pamoja.... hata kama mkiwa pamoja, lengo litakuwa kubanjuana tu and nothing else..
 
inawezekana kweli sikuelewi... Kwa sababu mtu ni mke/mume wa mtu, ukampenda... Kwa nini usijizuie ukaachana naye moja kwa moja?? Kwa sababu tayari ana mtu wake na hakuna jinsi mtakuja kuwa pamoja.... Hata kama mkiwa pamoja, lengo litakuwa kubanjuana tu and nothing else..

nahisi hatuelewani kweli..
Inawezekana mke wa mtu lakini mkapendana kweli
mpaka akamuacha mumewe na kuwa mkeo...
Usisahau sio kila mke wa mtu ana furaha na ndoa yake..
Wengine huwa wameshashindwa na ndoa zao,hawajapata mtu wa kumbadilisha
wanasema all is fair in love and war..........
 
Dah... anaweza akamuacha mume/mke akaenda kwenye worse place...

Sijui haya mapenzi yenu yakoje jamani...
 
inategemea na jinsia yako...
Kwa sisi wanaume huwa tuna kuwa na imani kuwa
nitaweza kubadilisha msimamo ili uwe wangu wa milele.
Tabu inakuja ukishindwa kumbadili mtu msimamo.akaamua
tu yaishe....maumivu yake...........
Ni kweli kabisa The Boss huwa kuna imani hiyo ya pengine nitambadilisha awe wangu milele- Unfortunately kwa wanawake walio wengi hii ni kubwa zaidi. Afadhali wanaume ambao wao wanawezakuwa na imani hii iwapo tu mwanamke anayefikiriwa hajaolewa. So kama anaye boyfriend wanaume alio wengi huwezaamua kumtokea ili ajaribu bahati yake ya kupindua mashua kuelekea upande wake. Ni vigumu kukuta mwanaume anayemtamani mke wa mtu akafanya hivyo kwa nia ya kumpindua mwenye mashua bali anafanya hivyo ili tu ashee na mwenye mashua kama free rider kasia ashike mwenye mashua yeye ah ajivinjari na mashua -ndio maana ya msemo wa wanawake walioolewa hawana gharama. Ni ngumu sana kwa mwanaume anayetoka na mke wa mtu kuja kumwoa na kumweka ndani kama ataachika kwa mumewe- wengi huwa wanajiuliza kama nilifanikiwa kumrubuni akaondoka kwa mumewe nina uhakika gani kama kwangu hatarubuniwa pia na mtu mwingine?

ila kwa wanawake walio wengi ni rahisi sana kukuta mtu anakwenda kwa mume wa mtu na kujibidiisha ili tu awe naye (haijalishi kama kaoa) imani kubwa ni kuwa nitamnjonjoisha hadi amwache mkewe wa ndoa na kunioa mimi. Nadhani hapo ndo tunapotofautiana na wanaume wengi.

But mimi nadhani ni vema kama unahisi uhusiano unaotamani kuuanzisha hautadumu ni bora ukauepuka kabisa.
 
Back
Top Bottom