Ipi bora - kati ya gari hizi

YoungCorporate

JF-Expert Member
Apr 30, 2010
391
113
Waswahili husema mchagua nazi huibukia.....Sasa nahitaji kijiusafiri kwa misele ya hapa na pale. Kutokana usawa wa mafuta machaguoa yangu yameangukia huku kwenye Toyota IST, Carina TI my road (cc 1500), Corolla Sedan na Mitsubishi colt. Mwenye uzoefu naomba anipatie insights kidogo kati ya gari izi ipi bora kwa nyanja zote....
 
Kama ni mafuta basi nakushauri uangalie ukubwa wa engine lakini pia na uimara wa gari hasa kwa barabara zetu za kibongo. Kwa ujumla toyota model ni nzuri zaidi kwa roads za kibongo. Hata hivyo kwa issue za mafuta angalia yenye ukubwa mdogo wa injini. hapo kama kuna lenye injini ya chini ya 1500 cc, say 1300, 1000 au 960, you can go for it.

Regards!
 
IST poa ila je mko wangapi maana naycho kigezo kwenye familia zetu za kiafrika
 
Achana na IST chukua carina Ti kwa kuwa ni imara na bodi gumu sana, fuel kiasi tu,mie nayo mwaka wa tatu bado iko fresh.
 
Mimi natumia Carina Si 1.8 nayo pia ni nzuri kwa matumizi ya mafuta try you will enjoy
 
Mitsubishi usiguse unaweza ukaepuka matumizi ya mafuta lakini spare parts hazishikiki ni bei juu sana ukilinganisha na magari mengine ya kawaida
 
Waswahili husema mchagua nazi huibukia.....Sasa nahitaji kijiusafiri kwa misele ya hapa na pale. Kutokana usawa wa mafuta machaguoa yangu yameangukia huku kwenye Toyota IST, Carina TI my road (cc 1500), Corolla Sedan na Mitsubishi colt. Mwenye uzoefu naomba anipatie insights kidogo kati ya gari izi ipi bora kwa nyanja zote....

Hii rangi nyekundu mkuu
 
KAMA ISSUE NI UDOGO WA INGINE BASI KAMATA KI-BAJAJ SINGLE STROKE.... NA UKIONA UCHUMI UNASUMBUA UNAKIINGIZA SOKONI KUOKOTEZA KIASI CHA MBOGA...ILA KAMA NI KWA GARI ILI UUZE SURA KITAA KWAKO KAA NDANI YA VITZ MKUU...FULL TANK UNAGONGA TRIPS ZA KIMARA -POSTA MPYA MWEZI MZIMA... ILA MILIMA NA MABONDE YA KIMARA MPAKA NALIONEA HURUMA GARI LENYEWE.... BASI KAMATA CARINA...kwanini usiwasiliane na RITZ-1 akupeleke kwa washkaji zake uwege unaazima "magari ya washkaji-mi-hummer na mi-vogue na mi-Q7 audi"?... fanya maamuzi magumu mkuu nakuaminia...
 
wakuu vipi kuhusu subaru forester 2.0 ccnataka kuangukia je inafaa?
sasa naona unataka kuanza mazoezi ya formula-01... HAYA SI MAGARI YA MASHINDANO KWELI?... MIE SEIELEWI BANA NGOJA WATAALAMU WAKUSHAURI ZAIDI.... MAANA NASIKIA STORY KIJIWENI ETI YANATUMIAGA JET FUEL SASA SIJUI UTANUNUA WAPI MAFUTA
 
nakushauri nunua Honda Fit badala ya IST. Nunua Honda CIvic badala ya Carina. HOnda Fit itakufaa sana kwenye nyanja zote, udogo wa injini, uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na utanashati kitaani. jaribu kucheki sifa za gari hizo kwenye mitandao ya wenzetu, utagundua kwa nini HOnda Fit zinauza sana Japan kuliko hizo Vitz, IST, Carina na Corolla
 
Haya magari ya Toyota yameshaanza kuporomoka sana na adui wake mkubwa ni HONDA. Honda ni gari zuri kwa kiwango cha Toyota, na wako makini sana katika kulinda soko lao, maana Toyota walishavimba kichwa saa wanalipua na magari yao ya mwakajana na mwaka juzi yalikataliwa katika soko la Marekani kwa sababu ya hitilafu nyingi tu za kifundi.

Honda ni nzuri, na kama uko makini kubadilisha oil kwa wakati utalichoka mwenyewe kwa kutaka chuma kipya, maana ni kwenda kwa mbele tu.
 
Mitsubishi usiguse unaweza ukaepuka matumizi ya mafuta lakini spare parts hazishikiki ni bei juu sana ukilinganisha na magari mengine ya kawaida

Natumia Mistubishi, japokuwa spare zinabei lakini ni genuine, ukinunua umenunua na mwisho wa siku unakuta Toyota inagharama zaidi ya Mistubishi, maana Spare moja ya Toyota unaweza kuinunua zaidi ya mara mbili kwa mwaka wakati Spare ya aina hiyo ya Mitsubishi utainunua mara moja tu

kila mtu na mtazamo wake , mi ningeenda kwa Mitsubishi
 
Nunua Mercedez Benz bwana. Nilikuwa na 190E nilidunda nayo miaka 5 bila ya homa. Muhimu ni kuifanyia service kwa wakati wake, na hakuna spares feki.
 
Back
Top Bottom