Interview with Jakaya Kikwete, president of Tanzania

Ndugu zangu wana-JF, tunakubaliana kimsingi kwamba raisi wetu ni "PUMBA". He is very shallow in his answers to very complex and sensitive questions and this can very well imply that he's shallow in his understanding, processing and thinking of these issues - garbage in - garbage out.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba, si wantanzania wengi wanaotafakari na kuchambua uwezo wa huyu Rais in teh way that we (wanaJF) do, kwa hiyo kwa waTanzania wengi huyu jamaa bado ni genius, bado ni Einstein kwao. This speaks a million kuhusu uwezo wa kiakili na kifikra wa waTanzania wengi. Kama umma una uwezo kifikra, then umma huo utatoa kiongozi mwenye upeo wa juu kama wao. Lakini kama umma ni primitive, then even their leaders(KIKWETE et al) pia watakuwa na primitive and unpolished way of analysing issues.

This maybe offensive to some, but it is the naked truth kuhusu nchi yetu ya Tanzania. We are far, far behind not only katika economic development lakini pia in social development, which is crucial for realising development in other sectors.

DISCLAIMER: 255Texter is a Tanzanian right wing nationalist residing in Tanzania
 
Wasomi,
Kama wewe ni kiongozi wa Tanzania leo hii Utafanya vipi kujiandaa kupambana na Financial crisis iliyopo..
Ningependa sana kusikia JIBU ambalo Kikwete alitakiwa kuwa nalo na kashindwa.. hii itatusaidia sisi na hata yeye Kikwete (kama kitaka) kujipanga kwani shida hii sio yake peke yake..

Swali: Tujipange vipi watanzania ktk hali hii mbaya ya Kiuchumi duniani!..
naomba kuwakilisha!

Mkuu Mkandara,

Sisi kwetu hali mbaya ya uchumi iko kila siku, hata wakati wenzetu walikuwa wanafaidi globalisation na kazi kibao kwa raia wao, sisi bado watu wetu wengi wanaishi kama omba omba.

Mimi naamini uchumi wa Tanzania kwa sehemu kubwa utaokolewa na Watanzania wenyewe hasa through small and medium enterprises (SME). Mahali popote hili ndilo kundi linaongoza ku create jobs na pia kulipa kodi kwa faida ya nchi.

Huwezi kuwa na hili kundi kama hakuna mabank ya uwekezaji ambayo yako tayari ku support SME. Waulize Watanzania wafanyabiashara wangapi wameweza kukopa pesa bank? percentage haizidi 10%. Mikopo ya bank ni ya wanasiasa na middle class ambao wengi wanaitumia kwenye ulaji na sio uzalishaji.

Kundi la pili ni kwenye infrastructure kama mabarabara, reli na bandari. Mahali palipo na biashara, maendeleo hufuata. Mtindo wa sasa wa kutumia wageni kwenye miradi mingi ya namna hii hautusaidi sana. Inatakiwa kuwa na phase ya kusaidia makampuni ya Watanzania ambapo katika kila kampuni ya nje ingetakiwa angalau 25 ya kazi ifanywe na kampuni ya Tanzania kwa lengo na kujifunza ili baada ya miaka kama 10, makampuni yetu yawe na uwezo wa kushindana na makampuni ya nje.

Kundi la tatu ni kwenye kilimo ambapo nguvu kubwa iwe kwenye wakulima wadogo wadogo pamoja na mkulima mkubwa mmoja au wawili kwa kila sehemu. Hawa wakulima wakubwa wawe source ya utaalamu, soko na hata funds kwa hawa wakulima wadogo wadogo.

Hizi pesa za kuendeshea hizi kazi zinaweza kupatikana kwa kupunguza matumizi ya serikali hasa kwenye ulaji wa posho, safari, magari na gharama zingine za serikali. Technology inaweza kutumika kusaidia kupunguza ukubwa wa serikali. Misaada michache na mikopo kutoka mabank ya dunia vinaweza kusaidia kuziba pengo katika matumizi yetu. Interests za mikopo zikishushwa kutoka 20% ilivyo sasa mpaka kwenye 10%, SME nyingi zitapata faida na kulipa tax inayotakiwa.

Kwa Tanzania jambo muhimu liwe ni ku create jobs ili hao wananchi ambao wanajiita ni wakulima wengi wapate kazi za kuajiriwa na kuacha kilimo kwa asilimia kama 30% ya Watanzania. Kilimo kilivyo sasa hakiwezi kuzalisha ziada kwasababu uzalishaji uko chini na watu wanaotegemea kilimo wako wengi mno.
 
You are contradicting yourself here - "...a huge opportunity for the opposition and wagombea wa siku zote wakae pembeni...", sasa how does this come come? Wagombea wa zamani ndio hao hao wameshajiweka mkao wa kula na hakuna jipya. Vijana wa oposition kama akina Zitto Kabwe wanajiengua wenyewe kivyaovyao. Frankly speaking I don't see much coming out of the opposition camp - they are becoming a joke. Ule msemo unasemaje: heri jini ulijualo kuliko jini usilolijua......you damn skippy!

Say whaaaat!!! Are you for real? On what proof are you basing this on, an interview in the Financial Times? Give me a break!

Gelange Vidunda, mkuu salamu, usione wengine tunacomment humu ndani ukaja na viji-attitude vyako!
Nani amekwambia I base my view on the interview of Financial Times? Sijaanza leo kumkosoa JK, hata kabla hajawa rais, nilijua he is ZEROO! He did nothing to prove otherwise.
Kuhusu opposition, I did not contradict myself. A huge opportunity for opposition na wagombea wa siku zote wakae pembeni are not in contradiction au we unejua opposition = wagombea wa kila siku?
Kama kwa maoni yako wagombea wa kila siku wameshakaa mkao wa kula that I have no comment on, I was voicing my opinion kwani naona kama akina Lipumba wanatuchosha kugombea kila wakati.
You say the opposition is a joke, well CCM is a bigger joke including your precious president na CCM wanatia kichefuchefu. Maana wao ni maharamia, wezi! CCM wameongoza nchi hii kwa takriban miaka 50 na hivi sasa tunarudi katika ujima! Hakuna maendeleo na tuna watawala siyo viongozi, inabidi tuanze upya kudai uhuru.
Kheri tuchague upinzani lakini hatuwezi kuendelea na upumbavu huu wa sasa na watawala ambao hawana hata idea wanafanya nini wako hapo kujishibisha tu! Mwisho wake utakuwa mbaya!
 
Mkuu MTANZANIA, very good observation naomba niulize hivi unataka kuniambia JK alishindwa kupata washauri kama wewe wasaidie kudessa kidogo kabla ya mkutano. I am sure that this question was to be expected ukiita IMF nchini kwako eti wafanye mkutano na mawaziri wa fedha wa Afrika kuhusu global economic downturn.
 
Wasomi,
Kama wewe ni kiongozi wa Tanzania leo hii Utafanya vipi kujiandaa kupambana na Financial crisis iliyopo..
Ningependa sana kusikia JIBU ambalo Kikwete alitakiwa kuwa nalo na kashindwa.. hii itatusaidia sisi na hata yeye Kikwete (kama kitaka) kujipanga kwani shida hii sio yake peke yake..

Swali: Tujipange vipi watanzania ktk hali hii mbaya ya Kiuchumi duniani!..
naomba kuwakilisha!

mkandara, swali lako ni muhimu sana.

japokuwa mimi sio mmoja wa wasomi bali mpanga nyanya flani hivi :)

naona jk kajitahidi kutaja effects za financial crisis kama ionyeshavyo hapa chini

"One of biggest worries about the current economic problems is of course demand, where we are losing markets for our commodities; prices of commodities are falling; we are losing [foreign] investments, we are seeing postponements, withdrawals of commitments made; another big danger is tourist arrivals coming down."

export market za commodities zinapokuwa mgogoro inabidi nchi izifanyie kazi hizo commodities zake na kuziongezea ubora (badala ya kuuza raw kahawa unauza kahawa ya makopo) japokuwa na hili utakumbana na vizingiti katika masoko ya nje lakini itasaidia industrialization.

aidha inabidi tuimarishe service oriented industries na kupanua uwigo wa "tourism" badala ya kupromote utalii wa kuangalia wanyama tuangalie uwezekano wa kuimalisha utalii wa historia yetu.

nadhani ni wakati muafaka wa kuangalia soko la ndani. tuanze kujiuzia wenyewe mali tunazozalisha na kuimarisha production capacity yetu.

financial institutions zetu na financial regulations zetu ziimarishwe ili ziweze kuwawezesha wanachi kuzitumia kwa manufaa. nadhani bado mabenki yetu yanaona kama yanatoa msaada kwa wateja na sio huduma. wananchi wa kawaida bado tunaogopa kwenda kukopa benki.

hiyo ndio senti hamsini zangu
 
Mkuu MTANZANIA, very good observation naomba niulize hivi unataka kuniambia JK alishindwa kupata washauri kama wewe wasaidie kudessa kidogo kabla ya mkutano. I am sure that this question was to be expected ukiita IMF nchini kwako eti wafanye mkutano na mawaziri wa fedha wa Afrika kuhusu global economic downturn.
Susuviri,
Shida ya JK si kwamba hana washauri. Hata kama Mtanzania angekuwa mshauri wake angekuwa ameshachoka. Unawezaje kumshauri much know?
 
Mtanzania,
Mkuu shukran sana nadhani michango kama hii ndiyo inahitajika sana hapa JF... hasa pale ulipogusia Small and medium Business...it's a wake up call...
Lakini mkuu tutaweza vipi ikiwa benki zetu haziwezi kulazimishwa kumkopesha mtu ambaye hana credit record na tutaweza vipi kuwalaumu ikiwa hata hao viongozi wenye Uwezo wanayaibia mabenki haya haya kwa hila za nguvu ya dola!..Ni policies zipi zijengwe kuhamasisha benki zetu ktk kutoa mikopo kwa wananchi Wajasiriamali ikiwa hata rais wa nchi anadai kuwa mmoja kati ya hao..

Kafara,
nadhani ni wakati muafaka wa kuangalia soko la ndani. tuanze kujiuzia wenyewe mali tunazozalisha na kuimarisha production capacity yetu.

financial institutions zetu na financial regulations zetu ziimarishwe ili ziweze kuwawezesha wanachi kuzitumia kwa manufaa. nadhani bado mabenki yetu yanaona kama yanatoa msaada kwa wateja na sio huduma. wananchi wa kawaida bado tunaogopa kwenda kukopa benki
Mkuu wangu umeupoza moyo wangu hasa uliposema tuangalie soko la ndani na uwezo wetu kuzalisha..Ni jibu fupi na lenye uzito mkubwa kwa mwenye kuelewa nini kinatokea sasa hivi na wapi tunakoenda..Isipokuwa kulingana na mazingira yetu ambayo yamejengwa na mifumo mibaya ya kiuchumi nashindwa kuelewa tutaanzia wapi..
Benki haziwezi kutoa mikopo kwa watu wasiokuwa na record nzuri ya kulipa madeni na wananchi hawawezi kuonyesha uwezo wa kulipa kama hawapewi mikopo..
Pili Benki haziwezi kutoa mikopo kwa wananchi ambao hawana hata utaratibu wa vitambulisho,, ikiwa na maana mtu akiingia kizani through vitambulisho na ajira atapatikana tu kwani vitambulisho vinabeba maelezo mengi muhimu ikiwa ni pamoja na address, uwezo wa kukataliwa kazi au kufungua kampuni kama huna kitambulisho na mengine mengi sana yatokanayo na vitambulisho..
Halafu, kinachonitisha mimi ni hiyo mila na desturi ya Mdanganyika.. kwamba kitu kinachotoka nje ndio mali..toka wataalam, lugha, waume/wake ktk ndoa au mapenzi hadi culture ikiwa ni pamoja na chakula...Kizuri na chenye soko ni kile kilichotoka nje..
Je, kweli kuna uwezekano wa sisi wenyewe kutengeneza kitu au vitu na vikapata soko la ndani hasa ktk wakati mgumu wa kiuchumi kama huu.. Naogopa kusema sioni ndani zaidi ya Bia, sigara na nyama choma!.. Sisi (maskini) kwa desturi zetu wakati wa shida na matatizo mazito ndio kwanza kuzidisha kujitanua tukidai tunaondoa mawazo!
 
mimi naona rais anafaa kuendelea hata kwa miaka kumi anajitahidi vya kutosha na kama kuna uwezekano awe rais wa maisha.anaonyesha jitihada ya kutosha kwa wananchi wake viva kikwete na ccm juu tawala milele hamna kama sisi.

Mkuu Mohamed Salum 200 umesema kweli,
Wanadamu wengi huwa hatuangalii mazuri 9 aliyoyafanya mwenzetu bali tuna angalia baya 1 alilolitenda.

Viva Kikwete
CCM ni namba wani.
 
Susuviri,
Shida ya JK si kwamba hana washauri. Hata kama Mtanzania angekuwa mshauri wake angekuwa ameshachoka. Unawezaje kumshauri much know?

Mkuu Jasusi,

Mimi na ushauri wapi na wapi. Mimi nipeleke kule Ileje kwa walala hoi kuwa katibu kata ndio kunanifaa. Nikishindwa na kuzidiwa nitakunywa kimpumu kupunguza mawazo.

Unajua wengine tunatukanwa sana huku nje kuhusu umaskini wa Afrika. Wazungu wanafikiri tatizo la Afrika ni kukosa wasomi, kumbe sivyo. Kuna wasomi wamejaa na wanatoa ushauri unaotakiwa lakini wanaishiwa kuchekwa. Kilichobaki Afrika ni kwa wasomi kuamua kufanya kweli. Chagua hata lengo dogo ambalo unaweza kulitekeleza, tuachane na haya mawazo ya nafasi kubwa za kutoa ushauri maana hata ukitoa, huo ushauri hauwezi kuzingatiwa.

Kuna mfaransa aliwahi kuniambia hivi wewe kule kwenu ambako hakuna wataalamu si unaweza kufaa zaidi kuliko kusaidia huku Europe kuliko endelea? Unaishia kukuna kichwa tu maana kakupasha ukweli. Kitu ambacho hawajui ni kwamba matatizo ya Afrika ni zaidi ya kutokuwa na wasomi. Mimi nakubaliana na Nyani Ngabu kwamba sisi Miafrika ndivyo tulivyo. Hivi kweli inahitaji ushauri gani kujua kwamba Kagoda wanatakiwa kuwa jela? Inahitaji ushauri gani kujua kwamba tunaibiwa mamilioni na investors ambao hawalipi hata kodi huku wanachota kila tulicho nacho?

Ukimsoma rais Obama kuhusu babake na frustration alizopata babake kule Kenya, unaelewa matatizo ya Africa. Hiyo ndio challenge ya wengi, je kuendele kuishi kwa raha mustarehe huku Ulaya na kufaidi yale ambayo wenzetu walijitolea kuyafanya kwa faida ya watu wao au kuamua kurudi kusaidia nyumbani na kuishia kuwa frustrated mpaka kuishia kubugia gongo?

Binafsi sina jibu, ni kuomba mungu hawa viongozi wetu angalau mungu awape utu waweze kuelewa kwamba hakuna binadamu anayetakiwa kuishi kwenye umaskini ambao watu wetu wanaishi. Kwamba wakiamua kufanya kweli, kuna nafasi ya nchi kubadilika.
 
Viva Kikwete!!!! kwa kipi alichokifanya!? Naona una faidika kwa namna moja au nyingine na ufisadi na uzembe uliojaa serikalini hadi utake Rais ambaye kazi imemshinda eti awe Rais wa maisha!!!! Mtu mzima hovyooo!!!! Kazi kweli kweli!!!! Kigumu chama cha mafis.....! Kigumu!

Ninaamini kuwa huu ni uwanja wa kila mwana JF kutoa maoni yake bila kuvunja sheria.
Sio vizuri kumwita mwenzako aliyetoa maoni yake kuwa ni 'hovyo'
Wewe tukikupa kiti cha kikwete kwa muda wa siku 100 utajiuzulu. Tuheshimiane kwa tofauti zetu.
 
Nyie vipi bana? Msimlaumu Kikwete...wa kulaumiwa ni hao Financial Times kwa kuuliza maswali magumu yasiyofuata protocol....
 
Susuviri,
Shida ya JK si kwamba hana washauri. Hata kama Mtanzania angekuwa mshauri wake angekuwa ameshachoka. Unawezaje kumshauri much know?

Jasusi, washauri kwenye kila kitu? Why? Kwani yeye Kikwete anajua nini? Au hajui lolote na chochote kiasi cha kutegemea washauri kwenye kila kitu? Jamani jamani...this is scary y'all...
 
Ndiyo Susuviri, maana kuna Wachumi na mchumi. Anaweza kabisa kuwa ni 'mchumi' maana kila mwaka pale UDSM alikuwa anaingia darasa jipya tu bila kujua chochote alichokifanya mwaka uliopita. Hata hotuba zake za kiswahili zina walakini mkubwa sana. Miaka mitano inamtosha kabisa kurudi bagamoyo kulima minazi.

Jamani mwacheni JK anajitahidi kufanya kazi yake vizuri, amekaa foreign affairs miaka kumi, hivyo yeye kutoa focus pia kwa mambo mengi ya nje pamoja na ziara ni kwa ajiri a maendeleo ya nchi maana tanzania ikisimama yenyewe haiwezi kwenda mbali lazima kushirikiana na nchi nyingine na mashirika mbalimbali.

Tatizo nini??????

kama kuna makosa ni ya kibinadamu ambayo isingewezekana hata kama ungekuwa wewe lazima ungefanya makosa ya kwako pia. kikubwa ni je ana-deliver??? jibu ni ndiyo kwa zaidi ya 50%
 
Mtanzania,
Mkuu wala sina la kuongezea na hakika kama viongozi wetu wanasoma maelezo kama haya na wakaweka ahadi ya kutimiza hata madogo yanayojitokeza.. basi huo ndio utakuwa mwanzo mzuri...shukran, niseme tena shukran na chukua 5...
 
Ninaamini kuwa huu ni uwanja wa kila mwana JF kutoa maoni yake bila kuvunja sheria.
Sio vizuri kumwita mwenzako aliyetoa maoni yake kuwa ni 'hovyo'
Wewe tukikupa kiti cha kikwete kwa muda wa siku 100 utajiuzulu. Tuheshimiane kwa tofauti zetu.

Ladslaus Modest, ni kweli wote tuna haki lakini utakuta kuna wanaJF wageni ambao wamekuja hapa kwa lengo la kumpamba JK na wanabaki kukutukana ukimkosoa. Pia hapa utakuta kuna wasomi wengi wa siku nyingi (Home of Great thinkers)ambao they do not tolerate mediocrity. Kuja kupiga propaganda za chama si mahala pake, kwani CCM mna nafasi hiyo nyingi huko mitaani, muendelee kuwadanganya wananchi lakini siyo kuja hapa kusema eti CCM oyeee! We umeshawahi kuona kuna mtu hapa anasema Chadema oyee, au NCCR oyee? We need critical thinkers we have enough sheep crowd mentality leaders in the form of our current leaders.

Alafu FYI unasema mwenzako angepewa kiti cha Kikwete angejiuzulu bada ya siku 100 basi ujue Bubu angefanya kazi mara milioni 1 better kuliko JK. Ye JK ingetakiwa awe ameshajiuzulu baada ya siku ya 1. Kwani kuendelea kuitwa rais is just a sham, he has abdicated powers a long time ago, ndo maana ameamua kuwa Vasco Da Gama na amewaachia nchi akina Rostam. Hebu nieleze JK amekuwa na mpango gani original tokea amechukua madaraka? Hana mkakati hata mmoja anabahatisha tu na sasa utumbo wake umeanza kuonekana kimataifa.
 
Jasusi, washauri kwenye kila kitu? Why? Kwani yeye Kikwete anajua nini? Au hajui lolote na chochote kiasi cha kutegemea washauri kwenye kila kitu? Jamani jamani...this is scary y'all...

My friend Nyani, I was scared since JK won the nomination in Dodoma, and my fear has increased exponentially since then,....
 
Susuviri,
Shida ya JK si kwamba hana washauri. Hata kama Mtanzania angekuwa mshauri wake angekuwa ameshachoka. Unawezaje kumshauri much know?

Kazi ya kumshauri Rais inapatikana vipi? Unaweza kuiomba anytime au inatangazwa, au Rais huchagua mwenyewe?

Kwa mwenye ufahamu na hili naomba kujua.
 
Back
Top Bottom