Interval ya uchaguzi ni ndefu sana

sijuikitu

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
286
12
Kwa mara ya kwanza naona kama vile miaka mitano ni mingi sana kusubiri kufanya uchaguzi mwingine.

Kwa nini tusianze na kupunguza mwaka mmoja iwe minne kama US.....maana duh, watanzania wapole sana, kugoma hatuwezi, kuandamana wanaoweza wachache......yaani wengi wetu masharobaro tu, tunaishia kupost comments JF
 
Kwa kuwa maji yametufika shingoni, ni vyema kufikiria hivyo, lakini "interval" ndogo ya uchaguzi si ufumbuzi wa matatizo yetu. Sio tu tuko wapole, hatuwezi kugoma wala kuandama, bali pia nina wasiwasi kuwa hatuwezi hata kuchagua kiongozi tunayemtaka. Kuna sababu nyingi.
1) Kushindwa kwa vyama vya upinzani kuungana kwa dhamiri moja, hata katika majimbo ambayo chama kinajuwa wazi kuwa chengine kina nguvu zaidi.
2) Kukosekana elimu ya uraia. Bado tunaendelea kuchagua chama na sio watu, tunachagua bora viongozi na sio viongozi bora.
3) Tabia ya viongozi wetu wa upinzani kukubali kushiriki katika uchaguzi huku wakielewa kuwa mazingira na fursa za uchaguzi haziko sawa. (rejea katiba yetu na matukio yanayotokea wakati na baada ya uchaguzi)
4) Kama haitoshi, kukubali kutia saini na kukubali matokeo ya uchaguzi yaliyochakachuliwa
5) Tukirejea namba 1 juu, hata baada ya uchaguzi, upinzani kuendelea kubezana, kubaguana na hata kutukanana
.........................
.........................
.........................
Tukitafakari hayo na mengine, hata tukiwa na vipindi vya miaka 4, bado hatutakuwa tumetatua kasoro zetu. (Sijui kama Ufaransa wamebadilisha katiba, lakini walikuwa na kipindi cha miaka saba kwa uchaguzi wa rais, sio Waziri Mkuu).

Kwa maoni yangu ni kuwa tunahitaji kubadilika, mabadiliko ya mawazo kwa ajili ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom