Internet inapunguza nguvu za kiume?

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Utafiti uliofanywa na
wanasayansi toka Marekani na
Argentina umeonyesha kuwa
wireless internet kwenye
laptop ina madhara kwa
viungo vya uzazi vya mwanaume kwa kuharibu
ubora wa mbegu za kiume au
kuziua kabisa. Utafiti
uliofanywa kwa
kuweka mbegu za kiume chini
ya laptop inayotumia wireless internet ulionyesha kuwa
mbegu za kiume zilipungua
ubora wake na hivyo
kupunguza chansi ya
mwanaume kupata mtoto.
Utafiti huo ulifanywa na timu ya wanasayansi toka taasisi
ya Nascentis Centre for
Reproductive Medicine iliyopo
Cordoba, Argentina kwa
kushirikiana na wanasayansi
wa Marekani wa taasisi ya Eastern Virginia Medical
School. Mbegu za kiume za
wanaume
29 wenye afya njema wenye
umri kati ya miaka 26 na 45
zilikusanywa na kugawanywa makundi mawili. Kundi moja la
mbegu za kiume liliwekwa
chini ya laptop inayotumia
wireless internet na jingine
liliwekwa mbali na laptop
zinazotumia wireless internet. Matokeo ni kwamba robo ya
mbegu za kiume zilizowekwa
chini ya laptop yenye wireless
internet ziliuliwa ndani ya
masaa machache. Vinasaba au
DNA ya mbegu za kiume nazo ziliharibiwa. Kwa upande wa
pili, mbegu za
kiume zilizowekwa mbali na
laptop hazikuonyesha
kupatwa na madhara yoyote
zaidi ya kupungua kidogo sana kwa spidi ya kuogelea ya
mbegu za kiume. Wakati huo
huo, mbegu za
kiume zilizowekwa chini ya
laptop ambayo haikuwa
imeunganishwa kwenye internet hazikuonyesha
kukumbwa na uharibifu
mkubwa kama uliotokea pale
zilipowekwa chini ya laptop
iliyounganishwa kwenye
wireless internet. "Utafiti wetu unaonyesha
kuwa kutumia wireless
internet huku ukiwa
umeiweka laptop karibu na
viungo vya uzazi hupelekea
kuharibika kwa ubora wa mbegu za kiume", alisema Dr
Conrado Avendano, ambaye
ndiye aliyeongoza utafiti huo.
"Kwa sasa hatujui kama
madhara haya yapo kwenye
laptop zote ziliounganishwa kwenye wireless internet au
la". Sababu ya kuharibika kwa
mbegu za kiume huenda
ikawa inasababishwa na
miale ya electromagnetic
inayotolewa na wireless internet. Matokeo ya utafiti
huu
yamewekwa kwenye jarida la
mwezi huu la Fertility and
Sterility journal, ingawa dokta
Avendano amewataka wanaume wasipaniki kwani
tafiti zaidi zinaendelea
kuhusiana na suala hili.
 
Back
Top Bottom