International Medical and Technology University (IMTU) - Special thread

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Hii ni SPECIAL THREAD kwa ajili ya wale wenye maswali juu ya chuo cha IMTU (International Medical and Technology University).

Maalum kwa ajili ya maswali, ufafanuzi na taarifa kadhaa juu ya Chuo.

Ili kurahisisha, tumeitenga hoja hii irahisishe mawasiliano kwa wadau ili kupata ufumbuzi wa mambo kadhaa. Tutakuwa tuna-update 1st post endapo kutakuwa na hoja mpya ambayo inahitaji kupewa attention kwa wakati husika.

Asante

==========

Taarifa za awali juu ya suala la Matumizi ya Dola chuoni:

Wakuu nani anayejua detail za chuo cha IMTU amwage hapa jamvini.

Nasikia kinatoa degree ya MBBS nashindwa kujua ni nini tofauti kati ya Degree ya MBBS na MD (Medical doctor) kama wanayotoa pale MUHAS.

Na vipi kuhusu ubora wa chuo hiki katika Elimu ya sayansi ya tiba? Vipi mazingira ya kujifunza?

Niliwahi kudokezwa kiliwahi kufungiwa na TCU miaka ya nyuma kwa kutokuwa na ubora, mwenye ufahamu anijuze wakuu.
Kumekuwa na mgomo katika chuo cha IMTU sasa ni siku ya nne wanafunzi hawaingii madarasani mgomo una madai ya msingi kabisa hasa suala la malipo ya ada kwa fedha za kigeni ambalo limekuwa likipigiwa kelele na wanafunzi na wazazi sasa muda sasa lakini serikali imekaa kimya, uongozi wa chuo umekaa kimya hakuna hatua yoyote inayochukuliwa hili suala la malipo ya fedha za kigeni ndani ya nchi yetu halafu fedha hizo zina ingizwa katika benk ya BANK OF INDIA pale mtaa wa Indila Gandh halafu zinapelekwa Canada nchi inabaki haina kitu.

Yaani hazihifadhiwi hapa ni mambo ya ajabu kabisa,serikali yetu sasa iwajali wanafunzi wazawa kwani hawa ndio watakao baki nchini na kuwahudumia Watanzania sasa mkataba wa hawa wahindi wenye chuo umeisha tangu mwezi JUNE 2011, na hata hivyo haujafanyiwa review muda mrefu.

Tunataka sasa ufanyiwe review upya na mambo mabovu yote yarekebishwe hiki kigugumizi serikali inakipata wapi na wao ndio wanaingia hii mikataba mibovu.
Kuna habari kuwa wanafunzi wa chuo cha afya IMTU wametakiwa kuhamia vyuo vingine vya afya vilivyoko Ifakara na Songea kwa sababu ya kushindwa kulipia tuition fee ambayo hulipwa kwa dola za kimarekani.

Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya wanafunzi, chuo na serikali imeamuliwa wale wanafunzi wasio na uwezo kifedha wahamie vyuo vya bei nafuu ili kuendelea kupata ufadhili wa serikali....

Nawasilisha!!

Kama moja ya mbinu za kutatua ufumbuzi wa matatizo yaliyojitokeza na kusababisha mgogoro mkubwa baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo cha udaktari cha IMTU (International Medical and Technological University); Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliiamuru TCU (Tanzania Commision for Universities) kufanya Academic Audit Report.

Mbona mpaka leo kimya?

Serikali yapiga ‘stop' matumizi ya dola IMTU

Aziza Masoud | Mwananchi - Nov 10, 2011

SERIKALI imeuagiza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba (IMTU) kuacha kutoza ada kwa fedha za kigeni na badala yake itoze kwa shilingi ya Tanzania.

Hatua hiyo ya Serikali imekuja kipindi ambacho kumekuwa na malalamiko kutoka kona mbalimbali za nchi kuhusu matumizi holela ya dola badala ya shilingi katika biashara na manunuzi.

Jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Hamisi Dihenga alitangaza hatua ya Serikali kuzuia matumizi hayo katika chuo cha IMTU akisema ada za chuo hicho zimekuwa juu ikilinganishwa na ada za vyuo vingine nchini.

Kwa muda mrefu wanafunzi wa IMTU wamekuwa wakilalamika na kuingia kwenye mgomo wakipinga kutozwa ada kwa kutumia viwango vya dola badala ya shilingi

Profesa Dihenga alisema kushuka kwa thamani ya shilingi mwaka hadi mwaka kumesababisha ada kupanda mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Profesa Dihenga ada ya mwaka 1996 ilikuwa Dola 4,500 za Marekani sawa na Sh2.7 milioni wakati kwa kiasi hicho mwaka 2011, ada ni Sh7.2 milioni.

"Hivyo wizara imeamua malipo yote yafanywe kwa shilingi ya Tanzania na TCU ifuatilie kwa uangalifu utekelezwaji wa mwongozo wake," alisema Profesa Dihenga.

Alisema mwongozo wa TCU unahimiza vyuo vyote kutoza ada kwa kutumia shilingi ya Tanzania kwa wanafunzi Watanzania.

Aidha chuo hicho kimetakiwa kufuata kanuni za udahili wanafunzi na hasa uwiano kwa wanafunzi wa ndani na wa nje ya nchi (25:75) kama ilivyo katika hati idhini za chuo hicho.

Mgogoro huo uliodumu kwa takribani miezi mitatu ulikuwa unahusisha uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na kusababisha kufungwa kwa chuo hicho Agosti 23, mwaka huu na ulisababishwa na utaratibu uliokuwa ukitumiwa na chuo hicho wa kulipa ada kwa Dola za Marekani.

Katika hatua nyingine, wizara imeitaka TCU kufanya ukaguzi wa kitaaluma na kiutawala kwenye chuo hicho ili kubaini ukweli wa malalamiko ya wanafunzi wa kutoridhishwa na mfumo wa uendeshaji na utoaji wa taaluma chuoni hapo ili kuweza kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
=============

Wanaohitaji msaada, maelekezo na ushauri juu ya IMTU:

I hv been selected to join B.Sc Medical Laboratory Technology at IMTU.

So, I'd like to know if there is any other JF members selected there so that we can exchange ideas and information about joining instructions, prospectus, challenges of the course we have been selected etc ...

And also if there are those who currently study there or alumni ill appreciate some welcome advice ...

Thanks
 
Wakuu nani anayejua detail za chuo cha IMTU amwage hapa jamvini.

Nasikia kinatoa degree ya MBBS nashindwa kujua ni nini tofauti kati ya Degree ya MBBS na MD (Medical doctor) kama wanayotoa pale MUHAS.

Na vipi kuhusu ubora wa chuo hiki katika Elimu ya sayansi ya tiba? Vipi mazingira ya kujifunza?

Niliwahi kudokezwa kiliwahi kufungiwa na TCU miaka ya nyuma kwa kutokuwa na ubora, mwenye ufahamu anijuze wakuu.
 
Kumekuwa na mgomo katika chuo cha IMTU sasa ni siku ya nne wanafunzi hawaingii madarasani mgomo una madai ya msingi kabisa hasa suala la malipo ya ada kwa fedha za kigeni ambalo limekuwa likipigiwa kelele na wanafunzi na wazazi sasa muda sasa lakini serikali imekaa kimya, uongozi wa chuo umekaa kimya hakuna hatua yoyote inayochukuliwa hili suala la malipo ya fedha za kigeni ndani ya nchi yetu halafu fedha hizo zina ingizwa katika benk ya BANK OF INDIA pale mtaa wa Indila Gandh halafu zinapelekwa Canada nchi inabaki haina kitu.

Yaani hazihifadhiwi hapa ni mambo ya ajabu kabisa,serikali yetu sasa iwajali wanafunzi wazawa kwani hawa ndio watakao baki nchini na kuwahudumia Watanzania sasa mkataba wa hawa wahindi wenye chuo umeisha tangu mwezi JUNE 2011, na hata hivyo haujafanyiwa review muda mrefu.

Tunataka sasa ufanyiwe review upya na mambo mabovu yote yarekebishwe hiki kigugumizi serikali inakipata wapi na wao ndio wanaingia hii mikataba mibovu.
 
Wazir wa afya, aliulizwa hili swali, majibu yalikuwa yale yale ya mchakato,mpango!
 
Hii inchi iko shimoni isha pigwa chata la sold matangazo ndo hayo yanatoka kwa vitendo wananchi hatuna chetu.
 
Tatizo ni hao wanaosababisha uchumi wetu kusuasua. Thamani ya shilingi yetu inavyoshuka kila siku - hata mimi ningekuwa na uwezo nigeuza huduma zangu kwa dola.
 
Mgogoro chuo cha IMTU kunaharufu ya rushwa na chuo chafungwa kihuni jana tarehe 23/8/2011.
 
Inasikitisha sana kuona madaktari wetu wajao wanavyoteseka na swala la ada.

Hivi kwa mtindo huu huduma zitakuwa ni nzuri maana elimu wanapata kwa mateso milioni saba na laki mbili si mchezo hapo hajkula hajui atalala wapi wala kitabu.

Hebu serikali ingila kati na pia kwa upande wangu naona hata uongozi wa hapo haufai maana kama miaka yote hawajashughulikia matatizo ya wanachuo nao wanatakiwa wawajibishwe kwa kuondolewa wajivue gamba, madaktari mshikilie hapo hapo Mungu atawapigania zaidi ya hapo.

Solidarity forever
 
Ipo likizo ya miaka kama 100 watu wanafanya watakavyo,hiyo IMTU ndo nini tena eti?
Ni chuo kikuu cha sayansi ya tiba(International and medical Technological University) kipo pale Interchick barabara mpya ya bagamoyo kumetokea mgomo wa kufa mtu pale wa wanafunzi mpakasasa chuo kimefungwa.Wanafunzi hawataki kulipa ada kwa dola za kimarekani.
 
chuo wanarudisha kwa makundi but hakuna kurudi hiyo tarehe maana hakuna dai letu lililojibiwa,wanaftufanya ni kichwa cha mwendawazimu chakujifunzia kunyoa,umoja wetu ndiyo silaha yetu wanatumia njia mbalimbali watumalizie ila kuna nguvu ya mungu, wanatafuta mrudi wametuma meseji kwa wazazi na wafadhili ili watushawishi ila nao waliowatumia meseji wanasikitika maana uongozi tena wawazawa unadiliki kuwasaliti watanzania wenye umasikini,wanachuo msiporipoti watu hawana kazi ndiyo maana watuma meseji za kutisha ,mgomo huu una baraka zote.

SOLIDARITY FOREVER ,TOGETHER WE CAN.
 
Kuhusu sakata la chuo kikuu cha tiba na teknologia, IMTU tunaomba Rais uliingilie kati utoe tamko moja maana ukimya wa vyombo husika utaleta mtafaruku wa hali ya juu kuna ufisadi ndani yake.

Baba Kikwete tunategemea sasa ni wakati wako wakutoa tamko rasmi kuhusu imtu maana wizara ya elimu kwa swala hili limeshikwa na viongozi wasiowaaminifu wasiojali hali ya mtanzania ila kilio chetu kimesikia na Mungu atatenda.

Twaamini sasa kimbilio letu baba kikwete ndani yakipindi kichace utatoa hilo tamko kuhusu hizo dola na uendeshwaji wa chuo kwa upande wa uongozi wa chuo hauridhishi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki IMTU, Mungu bariki madaktari wote, amen!
 
huna cha kuuliza ?ngona siku ukiumwa ndiyo hayo maneno yako umuulize daktari inaonyesha huji dunia inakwendaje mungu akusamehe
 
Serikali yapiga ‘stop' matumizi ya dola IMTU

Aziza Masoud | Mwananchi - Nov 10, 2011

SERIKALI imeuagiza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba (IMTU) kuacha kutoza ada kwa fedha za kigeni na badala yake itoze kwa shilingi ya Tanzania.

Hatua hiyo ya Serikali imekuja kipindi ambacho kumekuwa na malalamiko kutoka kona mbalimbali za nchi kuhusu matumizi holela ya dola badala ya shilingi katika biashara na manunuzi.

Jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Hamisi Dihenga alitangaza hatua ya Serikali kuzuia matumizi hayo katika chuo cha IMTU akisema ada za chuo hicho zimekuwa juu ikilinganishwa na ada za vyuo vingine nchini.

Kwa muda mrefu wanafunzi wa IMTU wamekuwa wakilalamika na kuingia kwenye mgomo wakipinga kutozwa ada kwa kutumia viwango vya dola badala ya shilingi

Profesa Dihenga alisema kushuka kwa thamani ya shilingi mwaka hadi mwaka kumesababisha ada kupanda mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Profesa Dihenga ada ya mwaka 1996 ilikuwa Dola 4,500 za Marekani sawa na Sh2.7 milioni wakati kwa kiasi hicho mwaka 2011, ada ni Sh7.2 milioni.

"Hivyo wizara imeamua malipo yote yafanywe kwa shilingi ya Tanzania na TCU ifuatilie kwa uangalifu utekelezwaji wa mwongozo wake," alisema Profesa Dihenga.

Alisema mwongozo wa TCU unahimiza vyuo vyote kutoza ada kwa kutumia shilingi ya Tanzania kwa wanafunzi Watanzania.

Aidha chuo hicho kimetakiwa kufuata kanuni za udahili wanafunzi na hasa uwiano kwa wanafunzi wa ndani na wa nje ya nchi (25:75) kama ilivyo katika hati idhini za chuo hicho.

Mgogoro huo uliodumu kwa takribani miezi mitatu ulikuwa unahusisha uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na kusababisha kufungwa kwa chuo hicho Agosti 23, mwaka huu na ulisababishwa na utaratibu uliokuwa ukitumiwa na chuo hicho wa kulipa ada kwa Dola za Marekani.

Katika hatua nyingine, wizara imeitaka TCU kufanya ukaguzi wa kitaaluma na kiutawala kwenye chuo hicho ili kubaini ukweli wa malalamiko ya wanafunzi wa kutoridhishwa na mfumo wa uendeshaji na utoaji wa taaluma chuoni hapo ili kuweza kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

My take:

Hongera serikali kwa uamuzi makini kumbe serikali ikiamua inaweza. Msiwaonee IMTU tu kuna private school nyingi Tanzania na Universities na other higher learning institution zinatoza ada kwa dola hasa jijini Dar,na Arusha. Madukani tunanunua vitu kwa US dollar, Kodi za nyumba na maofisi tunalipa kwa dollar hivi nauliza US dollar ndio sarafu iliyoruhusiwa Benki Kuu kama sarafu halali ya Tanzania? This needs to stop.
 
Back
Top Bottom