Intern Doctors-Wapangiwa vituo vya kazi.

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,598
1,539
Mara baada ya Heka heka za migomo ya madaktari nchini na kusababisha huduma za Afya kusua sua mara baada ya zaidi ya madaktari 300 kufukuzwa na wengine wengi kuacha kazi serikali pamoja na kukimbilia nchi za jirani, Serikali ilitoa tamko Bungeni kusema inasubiri madaktari "700" kutoka vyuo vikuu na shirikishi vya Afya na Tiba.

Katika kutekeleza hilo, Wizara ya Afya imeanza kuwapangia madaktari hao vituo vya kazi sehemu mbali mbali, ikiwa ni utaratibu tofauti na ule wa awali yaani(mwaka jana na miaka mingine nyuma), ambapo daktari aliomba katika hospitali husika na kisha kupeleka barua wizarani.)

Source:info kutoka Wizarani.
 
Wasisambazwe kabla hawajaiva sawasawa lakini - ambalo ndilo lengo la internship. Haitakiwi ikatishwe.
 
Wasisambazwe kabla hawajaiva sawasawa lakini - ambalo ndilo lengo la internship. Haitakiwi ikatishwe.

wamekwisha maliza mkuu ila sio wengi kiasi hicho "700"..na utaratibu huu wa kupunguza migomo kwa kuwapangia kwenda kokote..wakisema ni ORDER tofauti na zamani kuomba hospitali mwenyewe, sijui kama tutapata madaktari wa kutosha..
 
Sujui kama mimi ndo sijaelewa,ima maana hata wale waliofukuzwa wamepangiwa kazi?
 
Wasisambazwe kabla hawajaiva sawasawa lakini - ambalo ndilo lengo la internship. Haitakiwi ikatishwe.

hawa viongozi wanapoipeleka nchi ni pabaya sana ! AFYA ZA WATANZANIA ziliwekwa rehani miezi miwili na hawa viongozi wetu tulio wachagua.kwa mfano , imagine madaktari wote wangefutiwa leseni ingekuwaje, ina maana kwamba tungekaa bila huduma kwa miezi miwili bila huduma ya afya, inatisha!! sawa, madaktari wanakosa la kugoma lakini serikali ni JUKUMU lake kuhakikisha hakuna kasoro yeyote kwenye afya! moja yasababu kwanini viongozi wetu they do not care ni kwamba KAMA HAWANA UCHUNGU WA KUPIGANIA MALI ZINAZOBEBWA NA MAFISADI BASI HAWANA UCHUNGU NA KUPIGANIA NA AFYA ZA WATU!! raisi anatubuthu kuwatoa mhanga madaktari lakini hayuko teyari KUWAFUTIA LESENI ZA UONGOZI WA KINA sumaye ,lowassa , MKAPAna mergi( +plus wengine wengi). hii nchi ni uonevu wa WATAWALA kwa raia wa chini ambao wanalilia haki zao!
 
Back
Top Bottom