Intern doctor kwa Tanzania...

Mhubiri

Senior Member
Feb 12, 2008
180
21
Dada yangu amemaliza masomo yake ya udaktari wa binadamu mwezi huu,nchi moja ya Ulaya.Kuna nchi nyingine amepata nafasi ya kufanya internship lakini mwenyewe amesema,anapenda zaidi kuja kufanya internship yake Tanzania ili apate uzoefu zaidi kwa vitendo kwavile kuna wagonjwa wengi na madaktari ni wachache.

Ana maswali yafuatayo:
1.Kama atakuja mwezi ujao wa November,itamchukua muda gani mpaka atakapoanza kufanya hiyo internship?Yaani mchakato mzima wa kutuma maombi,kukubaliwa nk huwa unachukua muda gani?

2.Ni wapi pazuri kufanya internship na kujifunza zaidi kati ya Muhimbili na hospitali za Wilaya za Dar kama Mwananyamala au Temeke au Hospitali za Mikoani na Wilayani?

3.Kwa siku intern doctor anatakiwa afanye kazi kwa masaa mangapi?Ni jumatatu mpaka Ijumaa au hata weekends?

4.Je kuna posho/mshahara?Ni shilingi ngapi kwa mwezi?

5.Atapata likizo?Kwa mwaka ni wiki ngapi?

Madaktari na wakuu wengine mnaofahamu,naomba majibu tafadhali
 
Back
Top Bottom