Intelijensia ya Chadema inazidi kukidhoofisha chama

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,903
32,312
Wanabodi.

Chadema wanadai eti Intelijensia yao imenasa habari za kuwindwa na kuwawa wanasiasa watatu Slaa, Mnyika, Lema, pamoja na mtambo wa mawasiliano...madai ya aina hii mbali ya kuwa ya uwongo pia yanaonyesha kwamba hiyo Intelijensia wana tatizo kuu la kukosa uelewa na wamepotoka kwa kiasi kikubwa bila kujielewa.

Chadema wanadhani wanafanya makubwa kumbe wanajidanganya wenyewe wanaonyesha pia hawaelewi kabisa jukumu la Idara ya Usalama wa Taifa wanadhani ni chama cha siasa ni wapinzani wao wanaweza kurushiana vijembe na maneno mengine ya kipropaganda.

Intelijensia ya Chadema ndio ilimletea habari Dr Slaa na kuwa alishinda uchaguzi wa rais na kumwangusha Jakaya Kikwete hata hivyo shutuma zao dhidi ya Usalama wa Taifa hazikupokelewa kwa uzito maana matokeo waliyoyakubali ya ushindi wa wagombea Ubunge yaliifanya hoja yao ionekane dhaifu. Watanzania wale wale waliokuwa wakipiga kura za kumchagua rais, ndio hao waliopiga kura za kuchagua wabunge..

Intelijensia ya Chadema inashindwa kuelewa nchi yoyote duniani yenye usalama huwa ni kutokana na sera ya nchi hiyo ya Ulinzi na Usalama na utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi...maantiki ya kawaida inasababisha liibuke swali la msingi kwamba ikiwa Chadema ina viongozi wengi inakuaje wanne tu watake kuuwawa.

Chadema mbinu zenu za kutaka kuonewa huruma na wananchi na kupitia Intelijensia yenu inazidi kukidhoofisha chama chenu.
 
KWELI WATANZANIA TUU MAITI..WAKWANZA NI WEWE...haya bwana uliyelala tusikuamshe tusije lala sisi..napita tuu
 
Usitake kujihami na kujitetea, wewe ndio mhusika wa hiyo mashine umeshikwa pabaya, ccm vilaza nyie hamwezi shindana na cdm
 
Mlikataa mafisadi wakati ule Mwembe Yanga,
Sasa hivi ufisadi ndo unawatafuna kimya kimya ndani ya CCM,
CCM hawawezi kufa kikondoo hilo tunalijua wazi,
Watapiga mateke ya farasi sana na kutoa mayowe ya kishetani,
Watajikojolea na kujinyea hovyo hapo ndipo mauti itakuja.

Wako wengi wasio na hatia watavunjika mbavu,
wengine kung'olewa meno na kuvunjika mataya,
Wako watakao pigwa mateke na kuvunjwa nyonga,
CCM itaonja radha ya KUFA KUNOGA kwa uchungu,
Hata makada wake wataikimbia kwani kifo cha CCM ni lazima.

When Time comes,It will be unbearable to keep CCM alive even fo a second
 
Rhetoric questions ambazo umecontrust wewe mwenyewe na una majibu yako. Kawaulize ambao wamekuwa accused watakwambia kwa nini wanne na sio wengine. Sasa unakuja na maswali hayo ya ajabu ikiwa ina maana unataka majibu ya kina kutoka kwa wachangiaji au wewe unayo majibu. Kama sio wanne ili tuhuma za CDM zionekane hazina maana ni alzim wazidi hiyo numba iliyotajwa. Je, wakipungua au kuongezeka hilo linapunguza ukubwa tuhuma au linaongeza udogo wa tuhuma? Hata kamaunataka kuwasafisha watuhumiwa sio kwa hoja nyepesi kiasi hicho.

Halafu msingi na ubora wa CDM ni wa hitikadi inayolenga kuwakomboa watu toka aina zote za unyanyasaji. Ni hitikadi tu na hija zinaweza kukidhoofisha chama wala sio kauli. Msingi huu wa CDM umezama ndani na unazidi kukua ndio maana kinapendwa na kuenena sehemu ntingi za nchi hii na katika nyanja muhimu. Ni pale hitikadi itakapopitwa na wakati na CDM itadhoofika lakini wakati hilo linatokea Tanzania itakuwa imelomlewa katika kandamizo la muda mrefu wa kutawaliwa na CCM
 
Wanachofanya Chadema kinanikumbusha maneno ya Gobbles aliyekuwa Waziri wa Propaganda wa utawala wa Adolph Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia 1939-1945 alisema jambo lolote ukitaka lienee na likubalike upesi litangaze na ulikariri mara kwa mara...lakini viongozi wa Chadema wanashindwa kujua kuwa watanzania wa sasa si wajinga wa kuamini kila neno la mwanasiasa.
 
Wewe ni dhaifu sana Kama walivyo
Viongozi wako.endelea na usingizi
Wako sie tulishaamka kitambo hizo cd cheza Wewe
 
..maantiki ya kawaida inasababisha liibuke swali la msingi kwamba ikiwa Chadema ina viongozi wengi inakuaje wanne tu watake kuuwawa.

Chadema mbinu zenu za kutaka kuonewa huruma na wananchi na kupitia Intelijensia yenu inazidi kukidhoofisha chama chenu.
Kuna madaktari wengi ilikuwaje Dr. Ulimboka mkataka kumuua....kwanini kombe mlimuua?
 
Rhetoric questions ambazo umecontrust wewe mwenyewe na una majibu yako. Kawaulize ambao wamekuwa accused watakwambia kwa nini wanne na sio wengine. Sasa unakuja na maswali hayo ya ajabu ikiwa ina maana unataka majibu ya kina kutoka kwa wachangiaji au wewe unayo majibu. Kama sio wanne ili tuhuma za CDM zionekane hazina maana ni alzim wazidi hiyo numba iliyotajwa. Je, wakipungua au kuongezeka hilo linapunguza ukubwa tuhuma au linaongeza udogo wa tuhuma? Hata kamaunataka kuwasafisha watuhumiwa sio kwa hoja nyepesi kiasi hicho.

Halafu msingi na ubora wa CDM ni wa hitikadi inayolenga kuwakomboa watu toka aina zote za unyanyasaji. Ni hitikadi tu na hija zinaweza kukidhoofisha chama wala sio kauli. Msingi huu wa CDM umezama ndani na unazidi kukua ndio maana kinapendwa na kuenena sehemu ntingi za nchi hii na katika nyanja muhimu. Ni pale hitikadi itakapopitwa na wakati na CDM itadhoofika lakini wakati hilo linatokea Tanzania itakuwa imelomlewa katika kandamizo la muda mrefu wa kutawaliwa na CCM

Mbowe amenukuliwa akisema taarifa za uhakika zilizoangukia mikononi mwa intelijensia ya chama hicho zinathibitisha dhamira ya vigogo hao kuwadhuru viongozi wao...nayo hii ni kauli ya ajabu inaonyesha kiwango fulani cha ufahamu wa Chadema.
 
Long time ujaanzisha uzi ulikuwa unachangia za vijana wako naona leo umeingia mzigoni mwenyewe vipi end of moon umekaribia. Uzi wako uko chini sana hangover za mbio mnazokimbizwa na CDM sasa kama intelijesia ya CDM iko vizuri kuliko ya serikali ya magamba unategemea nini!Ni kama kutumia AntiVirus ambayo haiko updates for ten years.

Mytake: M4C Elimu ya Uraia vijijini ndiyo mpango mzima kwasasa propoganda za Mwigulu hazitunyimi usingizi
 
Wewe ungekuwa ni great thinker wa ukweli ilibidi u-refute hiyo claim ya Chadema kwa evidence; yaani uoneshe kuwa hiyo mitambo haipo sokoni, pili ni science fiction, tatu studies zinaonesha assassinations ufanywa kwa viongozi wote wa chama wa ngazi zote na haijawai kutokea kwa kiongozi mmoja tu!!!!
 
Ninachojiuliza kwa hawa CHADEMA kila taarifa ya kiintelijensia ina msemaji wake? mara SLAA , mara Mnyika , mara Marando na wakati mwingine Mbowe Mwenyewe. Hizi si ni dalili za uongo na upotoshaji mkubwa?
 
Wanachofanya Chadema kinanikumbusha maneno ya Gobbles aliyekuwa Waziri wa Propaganda wa utawala wa Adolph Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia 1939-1945 alisema jambo lolote ukitaka lienee na likubalike upesi litangaze na ulikariri mara kwa mara...lakini viongozi wa Chadema wanashindwa kujua kuwa watanzania wa sasa si wajinga wa kuamini kila neno la mwanasiasa.

Kizazi cha kukariri kimepita labda kizazi cha baba yako ndo kizazi cha kukariri.

Hiki kizazi cha kuhoji,kufikiri na kung'amua mambo.Wape hai wote mnaendeleza kizazi cha kukariri.
 
nilikuwa sijajua ni wewe mtoa mada wacha ni:flypig:zangu sitaki chochochoko kila siku cdm cdm inawaumiza kichwaee au baba zenu huwatuma kupunga upepo wawananchi?? hamulali ati kha karibu jukwaa la MMU NA CHIT CHAT UONDOE SUMU KWENYE AKILI YAKO HIYO NI SUMU MBAYA SANA HEBUU MUULIZE Bishanga Kongosho Mtambuzi Kaizer HorsePower BADILI TABIA MwanajamiiOne cacico wakupe siri kwanini hawakomalii siasa kiviiile
 
Back
Top Bottom